Hakuna kinachodumu milele

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,220
HAKUNA KINACHODUMU MILELE

Moja ya siri kubwa unayopaswa kuijua ili kupata uhuru kwenye maisha ni kwamba hakuna kinachodumu milele.Kama vile ambavyo sisi binadamu hatutadumu milele, siku moja utafikia mwisho, utakufa.

Ndivyo ilivyo kwa kila kitu kwenye maisha, kuna wakati kitafika mwisho.Matatizo uliyonayo hayatadumu milele, kuna wakati yatafika mwisho, labda wewe mwenyewe uamue kutafuta matatizo mengine tena.

Hata kazi unayofanya sasa haitadumu milele, kuna siku itafika mwisho, utafukuzwa, kupunguzwa au kustaafu.Biashara unayofanya sasa, hautaendelea kuifanya hivyo hivyo milele. Mambo yatabadilika na kama wewe hutabadilika utaachwa nyuma.
Mafanikio uliyonayo sasa hayatadumu milele, unahitaji kujifunza mbinu za kuendelea kuyaongeza kila siku.

Kwa kujua kwamba hakuna kidumucho milele, unaweza kujiandaa kwa nyakati ambazo ulichonacho sasa hakitakuwepo. Kushindwa kujiandaa ndio unajikuta kwenye wakati mgumu, kwenye matatizo makubwa.

Ndugu zangu kifupi tujipange kwa Mwaka unaokuja haijalishi ni changamoto gani tumekumbana nazo mwaka huu, Inuka Shtuka na Usonge Mbele.

Tambua Masikini wa Leo ni Tajiri wa Kesho.
 
Last edited by a moderator:
Ha ha ha ha

Eti masikini wa leo eti tajiri wa kesho

Misemo mingine sio ya kuitia akilini tangu nimeanza kuusikia naona haufanyi kazi
 
Ha ha ha ha

Eti masikini wa leo eti tajiri wa kesho

Misemo mingine sio ya kuitia akilini tangu nimeanza kuusikia naona haufanyi kazi
Msemo haufanyi kazi bila wewe kuuamini na kuufanyia kazi mkuu, lakini uangalie tatizo si msemo ni namna kazi unayoifanya kama ina tija ama la, badili shughuli utaona badiliko la kimaendeleo toka chini kwenda juu!
 
Msemo haufanyi kazi bila wewe kuuamini na kuufanyia kazi mkuu, lakini uangalie tatizo si msemo ni namna kazi unayoifanya kama ina tija ama la, badili shughuli utaona badiliko la kimaendeleo toka chini kwenda juu!
Asante kwa kumuelewesha.
 
Back
Top Bottom