Hakuna kanuni ya kufanikiwa, ni mipango yako tu

Jiwe limerushwa gizani, tunasubilia sauti tu.😃😄
chief, humu kuna watu naona wanajimwambafy kwenye comment kuwaambia wengine ni maskini au awatafute.. wakati wote tuko nyuma ya keyboard hakuna anaejua maisha ya mwenzake
 
Ujue kila jamii inatafsiri ya peke yake ya mafanikio.

Wengine huona kumiliki nyumba ndio alama kuu ya kufanikiwa kuna wenzako wanaona kununua ndinga ndio alama kuu ya mafanikio.
 
chief, humu kuna watu naona wanajimwambafy kwenye comment kuwaambia wengine ni maskini au awatafute.. wakati wote tuko nyuma ya keyboard hakuna anaejua maisha ya mwenzake
Mkuu,usikute hao wanaotukana hata bando tu lenyewe kapewa,hayo ndio maisha ya mtandaoni😀😀,kila mtu ana gari nzuri,nyumba,biashara na mke mzuri.Asante
 
Njia rahisi ya kufanikiwa kuliko zote ni kuiga, ukiboresha unaongeza chance ya kufanikiwa zaidi
 
Umenikumbusha shule kuna kijamaa prepo ya usiku haingii kazi yake ni kulala tu yaan ukitaka kumpata iwe usiku au mchana we zungukia vitandani utamkuta kalala cha kushangaza kila mitihani ukija katusua kuzidi hata wanaokesha kusoma, Sasa wewe jifanye kumgeza uone. ila nilikuja kugundua jamaa ni mtu wa mipango sana na sio kwamba hasomi kabisa
Noma sana.........
 
Aisee vijana wenzangu

Unajua watu tunashindwa kuelewa uvivu ni nini in such au tunajitia kutokuelewa?

Kuna uvivu wa kutenda (kufanya kazi kwa vitendo na ule uvivu wa kufikiri sasa ndugu yangu wewe endelea kusema mwenzio mvivu kutwa kushinda hapa JamiiForums, wakati yawezekana mwenzio ni mvivu wa kutenda haonyeshi kujishughulisha tu

Lakini kumbe mwenzio genius wa kufikiria na kupanga karata zake kichwani anashinda analala ,yuko mtandaoni 24/7hrs, anakula bata na ana mingle kila kijiwe na life linatembea kwa reli kama mtoto wa chifu huwezi jua hatufanani.

Ukiwa nyuma ya keyboard epuka kuona wenzako maskini, kisa unawaona hapa kwa kila comment..ohoooo

Narudia,usiige mtu hatufanani fuata njia yako. Utakufa unalaumu kama mfuasi wa kibwetele

Shauri yako.
Jinsi ya kutafuta hela
 
Ila usicheze mbali na ulimwengu wa roho
Good. Umenena vema mkuu, siyo wote wakaokuelewa maana wapo waliofanikiwa ila mpaka sasa hawajatambua mchango wa ulimwengu wa kiroho mpaka kufika hapo walipo.

Wengi wasioelewa huwa wanaamini mafanikio ni bahati!

Mafanikio unayatengeneza mwenyewe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom