Hakuna kama baba yangu

loyda

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2014
Posts
436
Reaction score
128
Nimejisikia kusema hivi
Wakati namaliza form 4 baba yangu alisema elimu niliyonayo inatosha hawezi kusomeshea mwanaume Mke.

Nililia sana kidogo nijiue.

Mwishowe mama yangu akanitoa nyumbani akanipeleka kwa wadogo zake mjini nikakaa huko nikasoma chuo bila ya baba yangu kujua nafanya nini, naishije, kwa miaka 3.

Hapo mama yangu anaomba omba na kukopa kwa nduguze ananilipia ada nasoma, baba hakuangaika na mimi

Nikaja kupata Kazi daah baba anavyopiga simu na maombi naombewa vibaya( kusema ukweli nampenda baba yangu kufa japo hajachangia senti Mimi kuwa hapa nilipo mama nae nampenda lakini nampenda baba zaidi.
 
Hongera kwa kumpenda baba yako...

Wazazi wako ni Mungu wako wa pili..
 
we ule uzi umeanzisha kule wa wanaume kujiamini umemwachia nani au leo kazi yako kuanzisha tu sredi unapojisikia..
 
Nina mjomba wangu hakusomesha watoto wake..alikuwa mlevi mbwa...watoto wakajitafutia maisha...siku hizi kutwa anasema 'wale Watoto nimewasomesha hawanijali' standard seven ya serikali ndo anaita kuwasomesha..
 
Uko dillema. Mzazi ni mzazi tu. Nenda nao sawa.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…