Hakuna Jipya chini ya Jua

Hakuna Jipya chini ya Jua

Ukweli1

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2013
Posts
550
Reaction score
333
Inafahamika kuwa serikali ya sasa ya Zimbabwe waliiga mfano wa Serikali ya Kenya wa mtindo wa kugawana madaraka. Na kinachotabiriwa kuendelea sasa ni kuwa First Lady Grace Mugabe anaandaliwa kuuchukua Urais. Hii inakaribiana na hatua alizofuata Hilary Clinton. Tofauti iko ni kuwa hawa wawili wana historia, uwezo, vipaumbele na tabia zisizofanana.

Hatua hii "Hillary's Step" siyo ngeni Afrika, former First Lady wa Ghana Nana Konadu Agyeman Rawlings mke wa Rais Jerry John Rawlings aligombea urais mwaka 2012 hakufanikiwa kupita na chama chake wameshatangaza kuwa First Lady Nana ni pendekezo lao na atagombea tena urais mwaka 2016. Former first Lady Nana ni mwanasiasa mwenye PhD ya heshima toka Lincoln University (Pennsylvania).

Historia fupi ya First Lady Grace Mugabe ana miaka 49, ameolewa na Rais Mugabe mwaka 1996. Rais ana miaka 90 kamzidi Grace na miaka 41 wana watoto watatu pamoja. Mbio za kisiasa za First Lady zilionekana rasmi August 2014 Grace alipopendekezwa kuwa mgombea wa pekee wa kiti cha Katibu mkuu wa Umoja wa Wanawake (the national secretary of the Zanu-PF women's league).

Hivyi karibuni First Lady Grace amegraduate PhD in sociology aliyotunikiwa na Chancellor (Rais Mugabe) September 11 2014 kutoka University of Zimbabwe ambako aliregister July 2014. Alikuwa mwanafunzi wa PhD kwa miezi miwili tu. Hii siyo PhD ya heshima kama aliyopata Rais JK hii ni ya kusomea kaandika Thesis (Disstertation) na topic ni "The changing social structure, the functions of the family: The case of children's homes in Zimbabwe". Degree yake ya kwanza ni by correspondence na ni Bachelor of Arts (BA) in Chinese language aliipata 2011, hana masters. Kwa sasa kama watabiri wanavyyosema anaelekea kuwa mgombania wa kiti cha urais.

Mpinzani wake wa karibu anasemekana kuwa ni Makamu wa Rais Joice Mujuru ambaye wiki mbili zilizopita amelalamika maisha yake kuwa hatarini baada ajali ya moto kuteketeza nyumba yake ya vyumba tisa, ikukumbuke kuwa mume wa Joice alifariki 2011 kwa ajali ya moto.

Je Dr. Grace Mugabe anauwezo wa kufuata hatua za Hillary?

​
Mwakani tuna uchaguzi ni nani akiwa Rais Tanzania mkewe anaonyesha mwelekeo wa kufuata hatua za Hillary?

MziziMkavu, Invisible, Mchambuzi, The Boss, BAK, The Boss, Janjaweed, sr bachelor, Dingswayo, MCHUNGUZI HURU, Ambiente Guru
Hilary.jpg Hillary na Grace Grace-Mugabe.jpg
Grace and Joice talking.jpgDr Grace na Dr Joice siku ya graduation (PhD)Grace and Joice.jpg
Grace.png​
 
Sio Rahisi kwa wanawake wa Kiafrika kushinda U-Rais kwa njia ya uhalali itakuwa kama ni miujiza Kuwa Rais wa Zimbambwe kwa sababu aatagombea U-Rais nyumaya mume wake Mzee Mugabe lakini kama hatokuwepo Mzee Mugabe hawezi kugombea hicho kiti cha U-Rais.
 
Hiyo Thesis Grace Mugabe nasikia imetoweka au kuchmolewa kwenye Tovuti ya Chuo Kikuu ila imebaki ya Mhitimumwenzaka aliyekuwa naye katika katika hiyo PHD.

Ningekuwa Juice Mujuru ningejiuzulu haraka sana kunusuru mali na maisha ya familia.
 
wake wa waheshimiwa wengi wa tz wahana elimu kubwa ndiyo sababu ya kupelekea uoga wa madaraka
 
Sio Rahisi kwa wanawake wa Kiafrika kushinda U-Rais kwa njia ya uhalali itakuwa kama ni miujiza Kuwa Rais wa Zimbambwe kwa sababu aatagombea U-Rais nyumaya mume wake Mzee Mugabe lakini kama hatokuwepo Mzee Mugabe hawezi kugombea hicho kiti cha U-Rais.
Sio swala la kuwa mwanamke tu MziziMkavu maana hata hao wanaume wengi marais Afrika sio njia za uhalali.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
ni kweli mkuu, ukiangalia Hillary Clinton, japo alikuwa first lady lakini alijenga profile ya maisha yake ya kisiasa mwenyewe hasa elimu na siasa yenyewe, lakini hapa Africa wanawake wengi hasa first lady wanaanza kujenga political profile kupitia migongo ya wanaume zao....utaona hapa kwetu tunasikia first lady kagombea hichi lindi, mara kafanya ziara hii, unajiuliza alikuawa wapi miaka yote..?
 
Back
Top Bottom