Hakuna jambo linalotokea kwa bahati mbaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hakuna jambo linalotokea kwa bahati mbaya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpangamji, Jun 1, 2012.

 1. Mpangamji

  Mpangamji JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2012
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 536
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Yaliyotokea Zanzibar kuhusiana na Uamsho yamepangwa, wale jamaa wanaotuzidi akili wameyapanga; kwa nini

  1) Wanauamsho lengo lao ni kuukataa muungano na tayari walikuwa wamepata wafuasi wengi na watu wengi walikuwa wanakubaliana nao wakiwemo wabara, nini cha kufanya? kwa kuwa ni kundi linalohusiana na Uislamu, kuwagombanisha na wakristu italeta maana zaidi kwa jamii na likifanikiwa hilo piga ban kama ya JF, tunafanyaje? choma makanisa kwa kivuli chao (wanauamsho), baadae tunafanyaje? tutalipa gharama zote za uharibu utakaojitokeza.

  2) Ili kuonyesha kuwa wa Zenj hawawezi kuishi peke yao nje ya muungano andaa waraka ambao utaonyesha kuna uhasama kati ya wapemba na waunguja. hii itasaidia nini? hii italeta utengano kati ya waunguja na wapemba na hivyo kushindwa kusimama pamoja katika kutetea masilahi yao.

  3) Ninafikiri kuwa wanauamsho wakitaka kutimiza malengo ya kuboresha au kuvunja muungano wabadili njia ya kutumia, waachane na maadamano kwani wasiohusika wale wenye akili nyingi watapitia hapo kufanya waonekane watu wa ajabu katika jamii.

  Ni mawazo yangu tu

  Mods mwanzoni nilipost hii post kwa namna ya uwazi zaidi mkaificha, futeni na hii.
   
 2. leroy

  leroy JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2012
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 839
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 60
  Hapo pekundu nina mashaka.
   
Loading...