Hakuna anayestaili kuvaa jezi namba 11 ya Ryan Giggs

Hakuna anayestaili kuvaa jezi namba 11 ya Ryan Giggs

DMaty

Member
Joined
Jun 7, 2012
Posts
15
Reaction score
4
Siku chache zilizopita, Ryan Giggs alitangaza
kustaafu soka. Atajiunga na Luis Van Gaal
kwenye benchi la ufundi la Manchester United
kama kocha msaidizi.
Ni huzuni kubwa kutomuona tena dimbani akiwa
na jezi yake namba 11, badala yake tutaendelea
kumuona akiwa katika benchi na LVG.
Sidhani kama ni sahihi kumpa mtu mwingine
namba (11) ya Giggs aitumie, Sio kwa heshima
tu, Bali ni kwa mambo makubwa aliyoyafanya
huyu jamaa akiwa Man U.
Giggs ana historia ya kipekee katika ulimwengu
wa soka, Ni mchezaji pekee aliyefunga goli
kwenye kila msimu wa ligi kuu tangu anze
kucheza kwenye msimu wa 1990-91 mpaka
2013-14, alifunga goli lake la kwanza kwenye
Manchester Derby (nikimaanisha dhidi ya Man
City), Manchester United ikishinda 1-0.
Ikumbukwe kuwa alipitia Man City kabla ya
kujiunga na Mashetani wekundu mwaka 1987.
Giggs ni mchezaji wa kwanza kushinda mfululizo
tuzo ya Young player of the year mwaka 1992 na
1993, Wayne Rooney ni moja kati ya wachezaji
waliowahi kushinda mara mbili mfululizo tuzo
iyo.
Giggs katika historia yake aliweza kufunga
magoli kadhaa ya kusisimua sana yakawa ni kati
ya magoli bora ya msimu, lakini goli ambalo
halitosahaulika milele ni lile alilowafunga Arsenal
kwenye nusu fainali ya FA, akichukua mpira
uliopotezwa na kiungo Patrick Viera kutoka
katikati ya uwanja aki-drible kwa spidi na kwa
kujiamini akikatiza katika ngome imara
iliyoundwa na beki kama Tony Adams, Martin
Keown na Lee Dixon na kuweka mpira nyavuni
akimuacha David Seaman akiwa langoni.
Akiwa Manchester United ameweza kushinda
mataji makubwa mbalimbali kama UEFA
champions league, EPL, FA....
Msimu wake wa mwisho 2013-14 alikabidhiwa
kuiongoza ManU katika mechi 4 zilizobakia
baada ya kutimuliwa David Moyes. Kitendo cha
Giggs kuaminika na kupewa nafasi iyo,
Kinaonyesha yeye ni mtu wa aina gani.Ni ngumu
kupata mtu kama Giggs tena kwenye ulimwengu
wa soka.
Kuna tetesi kwamba kijana Adnan Januzaj
anaweza kupewa jezi namba 11 ya gwiji Ryan
Giggs. Sidhani kama uyo kinda anaweza kuvaa
viatu vilivyoachwa na Giggs, Ni vikubwa mno.
Watu wengine wanaweza kusema "kumpa mtu
namba aliyokuwa anatumia mchezaji fulani
haimaanishi unataka kumfananisha na mtu
aliekuwa anaitumia", Iyo kauli sio sahihi. Ukweli
ni kwamba ukimpa mchezaji namba iliyokua
inatumika na mchezaji mwingine itajenga picha
akilini mwako ya yule mchezaji wa zamani kila
ukiona ile namba mgongoni mwa yule mchezaji
mpya anaetumia ile namba.Januzaj anaweza
kuwa ni mchezaji mzuri, lakini kila nikimuona
uwanjani na namba 11, nitakua namkumbuka
Ryan Giggs, Ningependa Januzaj asihusishwe na
hii namba, inaeza kumuharibia mpira wake huyu
bwana mdogo. Acha Januzaj awe Januzaj,
aendelee kuvaa namba yake 44 au wampe
namba nyingine lakini sio 11.
Ikiwa WestHam na Ac Milan waliweza kufuta jezi
namba 6 kwa kuwaenzi Bobby Moore na Franco
Baresi, Kwanini ManU wasifanye ivo?
Ata Bongo, usitegemee kuona jezi namba 30
ikitumika tena Msimbazi, Hii ni kutokana
waliamua kuifuta ili kumuenzi marehemu
Mafisango.
Mimi huwa namuita Sir Ryan Giggs mwenye
namba 11 mgongoni ya maajabu.
Imeandikwa na David Ngemela
 
Hata mimi nakubaliana na mwandishi,Gigs kaifanyia mambo mengi club ya manchester united ni vyema namba alokuwa anatumia ibaki kama kumbukumbu ya u_legend wake.
 
Wameshasema hyo jezi haiwezi kustaafishwa hata iweje, kuna mchezaji atapewa tu
 
Ukiangalia historia ya no. 7 pale Man U utagundua kila aliyeitumia alikuwa fundi kupita maelzo,na kama Ferguson angesema aipumzishe hiyo jersey cdhan kama Beckham au Ronaldo wangeivaa,ila alichofanya baada ya Cantona kustaaf akampa Bekham kisha Ronaldo,ushawahi kujiuliza kwann Ferguson alikuwa anafanya vile?Lengo lake ilikuwa ni kumpa motisha ya kujituma yule anayegewa hiyo no. Na kama utakumbuka pindi Ronaldo alivyogewa ile jezi kwa mara ya kwanza alikataa kwa kuhofia kutoitendea haki ile jezi lakini Ferguson alimsisitiza kuivaa na mwishowe akaja kuwa mchezaji bora tena zaidi ya waliokuwa wanaitumia hawali.

Kwa mtazamo wangu mtu kama Januzaj akigewa namba 11 ni vizuri tu kwani kutokana na uwezo wake atajituma zaidi ili kulinda heshima ya jezi
 
Ilikua nimuunge mkono mtoa uzi ila itabidi niwe upande wako kwa jinsi ulivyochambua hili...
Kumpa motisha dogo wampe tuu naye ajitahidi kuitendea kazi...

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ilikua nimuunge mkono mtoa uzi ila itabidi niwe upande wako kwa jinsi ulivyochambua hili...
Kumpa motisha dogo wampe tuu naye ajitahidi kuitendea kazi...

Sent from my iPhone using JamiiForums

Asante mkuu,nnaimani dogo Januzaj kwa uwezo alionao akijituma atakuwa bonge la mchezaji miaka ijayo....wampe tu hiyo jezi
 
Asante mkuu,nnaimani dogo Januzaj kwa uwezo alionao akijituma atakuwa bonge la mchezaji miaka ijayo....wampe tu hiyo jezi

Amesha onesha analiweza hilo, ni kumuamini tuu

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hata Michael Owen?

Ferguson alimpa Owen ile namba ili kum4c jamaa arudi kwenye kiwango kama alivyokuwa Liverpool kabla ya kwenda Madrid.....Ferguson ni kocha aliyekuwa anajua kucheza na saikolojia ya wachezaji.

Mm ni shabiki wa Man U ila nakubali kuwa toka waondoke kina Kean,Butt,Neville na Beckham hatukuwa na competitive players tena katika timu yetu hasa midfield,ila timu ilikuwa inafanya vzr bcz Ferguson alikuwa anacheza na saikolojia ya wachezaji tu,kitu ambacho Moyes alishindwa ndio maana kikosi kile kile lakin kashindwa kwenda nacho popote.Wachezaji walipoteza uoga kwa kocha ( Ferguson alikuwa anaogopwa na wachezaji wote )
 
Back
Top Bottom