Hakimu hoooooiiiii

Mbimbinho

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2009
Posts
8,326
Reaction score
7,807
Mshikaji alijikuta yuko mahakamani kwa kosa la kuiba gari.

HAKIMU: Mshtakiwa unamaelezo yoyote?

MSHKAJI: Mzee, hawa jamaa wamenibambikia kesi,
ishu nzima ilianza nilipokuwa pale masikani kwetu
naosha magari kama kawa. Yule maza pale akaja na
ndinga lake la nguvu, akaniambia nilioshe, mi
nikalipiga maji kisawasawa, huyu maza akanambia
niiingie kwenye gari yake kuna ishu muhimu,
akanichukua mpaka pale Mwenge, akaniambia
nichague viwalo, nikachagua nguo za nguvu akalipa,
akanambia nimsindikize home kwake, tukasepa,
nikafika kwake, mjengo wa nguvu, akanambia nioge
nikaoga fresh, ile natoka bafuni akanipa msosi wa
nguvu nikashushia na mzinga wa Nyagi, kisha
akaniita chumbani kwake, akasaula akajitosa
kitandani, kisha akanambia,

MAZA: Mpenzi
nimekupenda sana, nimekuridhia kila kitu, chukua
unachotaka. Basi kusikia hivyo mzee wangu
nikacheki kushoto , nikacheki kulia nikaziona funguo
za ndinga lake, nikaona poa ngoja nichukue mkoko.
Nikachukua nikasepa, sasa hawa polisi wanasema
nimeiba gari how kam mzee wangu?

HAKIMU: Mmmmh!!!
 
tunataka huyo maza athibitishe kama alitoa kauli kama hiyo kisha kesi inafutwa na jamaa aendelee na ndinga lake.
 
Safi sana hizo ndo akili za maendeleo.
 
mmmh huyo jamaa kwa maana nyingine alikuwa sahihi ili kwa maana yakimazingira ( contextually) mama aliposema kujisevia chochote pale hakumaanisha hayo magari nk. ndio maana alipochukua gari mama akaenda kumshtaki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…