Hakikisha wewe na mwenzako huitizami tena tbc one kwani ndio inailinda ccm.

richone

Senior Member
Apr 3, 2012
146
35
Ndugu watanzania wapenda mabadiliko. Ninawaombeni wote kwa umoja wetu hasa sisi tunaoamini katika nguvu ya umma tusiitizame tena TBC one tuikatae kwa vitendo. hiii ni kwasababu zifuatazo.
1.imekuwa ikitumika kama chombo cha kuiimarisha ccm kwani inaeneza na kusambaza propaganda za CCm
2. TBC one wamekuwa wakitumika kuichafua CHADEMA ikitumiwa na Nape na baadhi ya mawaziri.
3. Kuitizama TBC tunawafanya wapate biashara ambapo kipato hicho wanakitumia kuwalipa wafanyakazi ambao wanatuvunja moyo.
4. Hatuwezi kugaramia kujeruhiwa(pesa yetu wenyewe isitudhuru)
5. Haina vipindi vyenye mvuto kwa jamii.
kutokana na haoy yote na mengine mengi ambayo sijayasema ni vizuri tukasusa kuiangalia ili nayo iumie kama sisi.
 
Bunge likianza huwa ndio natazama tbccm.ila tufanyeje ili cdm ipatikane walau radio ?
 
TBCCCCC............................hapo huwa naangalia tuuuuu......mmmmhhh, sina kipindi hapo.
 
Yaani Hukumu ikitoka Chama chako kikianguka tu wote tukuunge mkono basi hata Dini za wenzako huzitaki
Maana Mlokole hamtaki M-KKKT nae KKKt hamtaki Muislam
Siasa za ..com zinaturudisha CUF walimcgguunja Polisi pale Mwembechai na kule Pemba kweli 2015 tutapika tukiizima TBC?
 
Kutoangalia tbc ni choice yako.waache waangaliao nao wapate ile kitu roho yao inapenda. Sii wote wana Jf ni cdm lakini mbona wapo? Mbali na hayo,ukitaka kumjua adui yako vizuri mkabili na sio umkwepe. Siasa za chuki hazifai. Leo itakua tv, kesho utasema tusinunue duka flani ni la mwana ccm, itafuata usafiri, nyumba ya kupanga, msiba wa mwana ccm nk. Hii sio demokrasia tulioikusudia.Demokrasia ya kweli sii kubaguana bali ni kushimdana kwa hoja na mfano wake hai angalia wagombea ubunge wana cdm jinsi walivyojenga hoja vyema na kushinda ubunge kwa kishindo. Chuki haina nafasi hapa
 
Hoja haina msingi kwa mantiki hiyo ifike hatua tuache kusaidiana kwa sbabu ya sihasa la hasha huo ni uchuro na ushabiki usiokuwa na mantiki tunapingana kwenye majukwaa tunapingana hukohuko kwenye majukwaa tukirudi nyumbn au mtaani sisi ni ndugu na ni jmaa pia
 
Kutoangalia tbc ni choice
yako.waache waangaliao nao wapate ile kitu roho yao inapenda. Sii wote
wana Jf ni cdm lakini mbona wapo? Mbali na hayo,ukitaka kumjua adui
yako vizuri mkabili na sio umkwepe. Siasa za chuki hazifai. Leo itakua
tv, kesho utasema tusinunue duka flani ni la mwana ccm, itafuata
usafiri, nyumba ya kupanga, msiba wa mwana ccm nk. Hii sio demokrasia
tulioikusudia.Demokrasia ya kweli sii kubaguana bali ni kushimdana kwa
hoja na mfano wake hai angalia wagombea ubunge wana cdm jinsi
walivyojenga hoja vyema na kushinda ubunge kwa kishindo. Chuki haina
nafasi hapa

Uko right! tatizo wanakariri! tushindane kwa hoja! sote tunapenda mabadiliko! lakini linapokuja suala la kumpangia mtu afuatilie chombo gani cha habari,huko ni kusigina misingi ya demokrasia!
 
Kwa tathimini yangu,TBC1 hawafurahii harakati za mabadliko zinazotokea nchiniNi kama wanajiona wana mkataba na serikali& CCM nawakati mwingine nao wanajiona ni sehemu ya watawala!!!kumbe ni watumishi wetu!!
Siku inakuja TBC watalazimika, huku machozi wakiwatoka,nyuso zikiwajaa aibu ,mioyo ikiwasuta,kutangaza ushindi wa Rais kutoka CHADEMA.Siku hiyo haipo mbali,i karibu yaja.
KBC ya Kenya ilikuwa na mizengwe hii wanayopenda kufanya,lakini sasa ni kama wamesahau kama kuliwahi kuwapo KANU na MOI!!!
Ni dhahiri kuwa weledi na kutenda haki ni masomo magumu sana kwa TBC1 kuyaelewa kwa nadharia.Watajifunza vizuri zaidi kwa vitendo wakati ukifika.
 
Kwenye habari ndo kabsaaa, nimeacha kuangalia cku nyingi uwa nachek star tv, ila bunge likiwepo ndo naangalia. Vpndi vingne ni vya sera.
 
Hii station iko bias sana yanapokuja maswala ya cdm.
Ninacho jiuliza hivi hawa wahusika
huwa hawapiti humu jf hata wasijirekebishe?
Hebu 2015 ifike Tido Mhando arudi pale.
 
Back
Top Bottom