Mlendamboga
JF-Expert Member
- Sep 14, 2011
- 670
- 347
TCRA imeanza kampeni za kuelimisha wananchi kuhakiki usajili wa simu card zao ili kujiweka salama kutokana na utekelezaji wa sheria ya Epoca ya 2010 inayotaka kila simu ya mkononi iwe imesajiliwa na kuwa na utambulisho wa mmiliki.Ili popote pale ulipo uweze kuhakiki kama umesajiliwa bonyeza kwenye simu yako ya mkononi *106# ok italeta taarifa za usajili wako, kama utabaini kasoro ni muhimu uende kwa wakala aliyekaribu akurekebishie taarifa zako ikiwa ni pamoja na kasoro za Majina.
Vitambulisho vinavyoruhusiwa kwa sasa kutumika kusajili simu ni
1. Kitambulisho cha uraia(NIDA)
2.Kitambulisho cha mpiga kura
3.Leseni ya kuendeshea gari
4.Hati ya kusafiria
5.Kitambulisho cha mkazi Mzanzibar
Kulingana na sheria ya Epoca kosa kubwa ni kusajili simu kwa taarifa za uongo (zisizo za kwako) ambapo adhabu yake ni kifungo cha miezi 12 na faini ya Tshs 3milioni