Hakika sekretariat ya Ajira inajitahidi katika majukumu yake

Hakika sekretariat ya Ajira inajitahidi katika majukumu yake

Mwambawetu

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
25,383
Reaction score
34,367
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw.Juma Mkomi ameipongeza Sekretarieti ya Ajira kwa kuendesha mchakato wa ajira kwa ufanisi.

Bw.Mkomi ametoa pongezi hizo jijini Dodoma katika kikao kazi kilichowakutanisha Sekretarieti ya Ajira pamoja na wadau mbalimbali ili kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na uendeshaji wa mchakato wa ajira pamoja na kupeana mrejesho.

Aidha, Bw.Mkomi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kikao hicho ameitaka Sekretarieti ya Ajira kuendelea kuzingatia sheria,kanuni na taratibu katika shughuli zake ili kuhakikisha mchakato wa ajira unaendeshwa kwa haki na bila upendeleo.

"Sekretarieti ya Ajira niwapongeze sana kwa kazi kubwa mnayoifanya ya kuhakikisha tunaendelea kupata watumishi wa umma wenye ubora kwa kuzingatia sheria na taratibu ambazo kwa kiasi kikubwa zimepunguza malalamiko mengi kutoka kwa wananchi” alisema.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu huyo aliweka wazi kuhusu kukamilika kwa muongozo wa utoaji wa nafasi za kujitolea katika taasisi mbalimbali za umma ambao unatarajiwa kuanza kutumika hivi karibuni.

Kwa upande wake Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Bw. Mick Kiliba ameeleza kuwa lengo la kikao hicho ni kuhakikisha ofisi hiyo inawasiliana na waajiri pamoja na taasisi za elimu kwa lengo la kupata mrejesho ili kuendelea kuboresha mchakato wa ajira na hatimaye kupata watumishi wenye ubora na weledi.

Miongoni mwa wadau walioshiriki kikao hicho ni pamoja na Wizara mbalimbali, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa, Idara zinazojitegemea, Taasisi mbalimbali za umma, Mamlaka, Wakala, Vyuo Vikuu na Vyuo vya kati.
 
Katika report yako sijaona ni kwa namna gani inajitahidi katika hayo majukumu sanasana naona umetupa muhtasari na pongezi za kikao chao walichokaa ambacho ni kawaida katika ofisi na shughuli za kila siku za kiofisi.
 
Kijani - Apps on Google Play Gusa link uone fursa zilizopo ndani. Ajira za kutosha ni maombi yako tu hakuna haja ya connection. Wale tuliokosa TRA tuje hapa. Huu ni mshahara wangu wa kwanza. Niliweka nadhiri ntawasanua watu sitakula peke yangu. Kazi kwenu na sala zenu.
 
Back
Top Bottom