VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Ingawa sisomisomi biblia kila mara,nina mistari naijua. Najua kuna mistari inayosimulia jinsi wayaudi walivyokuwa hawamkubali Yesu na kumuona wa kawaida,tapeli na mbabaishaji. Wapo ambao hawakumkubali kuanzia mwanzo hadi mwisho.
Hata siku Yesu,saa saba mchana,alipokufa msalabani,askari waliokuwa lindo kwenye misalaba walikosulubiwa Yesu na majambazi wawili walikiri kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu. Walisema: hakika huyu alikuwa ni Mwana wa Mungu!
Hapo ni baada ya giza kuifunika nchi na hata pazia la hekalu kuraruka katikati wakati Yesu akikata roho msalabani. Ndicho kinachotokea kwa mwanasiasa Edward Lowassa. Lowassa anaivuruga CCM. Anaichachafya. Haili na kulala kwa raha.
Kwa matendo na maneno yake pamoja na fukuto linaloendelea ndani ya CCM,Lowassa alikuwa nguzo chamani. Alikuwa ni mwenye ushawishi na kukubalika. Ameshajihakikishia kura kwa maelfu toka kwa makada wa CCM ambao wanamkubali. Wale walio CCM kimwili tu. Wengi tu.
Lakini,CCM itapambana naye hadi mwisho wa uchaguzi huu. Mpira ni dakika 90!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam