Haki za wafanyakazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haki za wafanyakazi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chambila, Aug 4, 2012.

 1. C

  Chambila New Member

  #1
  Aug 4, 2012
  Joined: Aug 3, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanza kabisa naomba nimshukuru mwenyezi mungu kwa pumzi hii anayotupa,maanake akiamua aiondoe hakuna atakeyesalia hata hao mafisadi nao wataonja joto la jiwe.Narudi kwenye hoja yangu ya msingi kaka MUNYIKA simamia haki za vijana wenzako,nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu sana bunge linaloendelea na jinsi linavyoendeshwa kwa kutozingatia usawa na limekuwa likilinda sana chama tawala,hoja za msingi zenye manufaa kwa wananchi wa nchi hii zimekuwa zikipingwa tena mchana kweupe.Angalia hili sakata la hii mifuko ya jamii hivi kweli waliolipitisha akili zao ziko sawa,tazama mfanyakazi kutoka sekta binafsi ambako mikataba yake ni ya muda tu,mtu kafanya kazi miezi nane kazi imeisha naye asubili mpaka baada ya miaka 55 au 60? hii inaingia akilini kweli.Kuna vijana wengine wanajitahidi wafanye kazi ili baadae wakajiendeleze kielimu kwa kutumia hayo makusany
  o yake naye asubili miaka 50,55 au 60 ndo akasome tena.Hebu angalia ukiritimba uliopo kenye kutoa mikopo yenyewe ya wanafunzi watoto wengi wa wakulima ndo wanaonyanyasika.Kwa kulitambua hilo wakaamua kujishughulisha ili angalau waweze kutimiza malengo yao lakini serikali dhalimu inwafuata na huko na kuwabana ili wasiweze kabisa kutimiza malengo yao.Kweni na huruma na mwogopeni mungu aliyepa nyie leo na kesho nanyi atawanyima.Mh.Munyika kwa umakini wako saidia vijana wenzako,komaa na hiyo hoja bungeni kubatilisha hilo,tumia uwezo ulionao hata kuwashawishi na wabunge wenzako ambao hata hawaelewi wanachokifanya humo bungeni.Kwa leo naomba niishie hapo na wenzangu waweze kusema lolote
   
Loading...