sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,687
- 1,111
Iko wapi haki ya kikatiba ya kuishi ikiwa kila aliyeuwa naye atauwawa,kuna haja gani kuwa na mamlaka ya kisheria ikiwa tunaweza kuhukumu kwa kujichukulia sheria mkononi?
Tumeweka mhimili mahakama kuwa ndicho chombo chenye haki ya kutafsiri sheria na kutoa hukumu,tukiacha matukio yanayo tamalaki huko Kibiti kwa kukaa kimya tutatengeneza chuki ya kundi moja dhidi ya jingine,hali hiyo ikiendelea tunaelekea kutengeneza vita vya wenyewe kwa wenyewe,mbaya zaidi tuna tengeneza udini katika mazingira ya kuwasaka majambazi.
Serikali inajuwa kinachoendelea huko Kibiti,askari walio uwawa ni miongoni mwa familia zetu,tuliwapenda,tuliumia sana kupotezwa kwao kwa kunyimwa haki yao ya kikatiba ya kuishi,lakini yanayotokea huko Kibiti ni zaidi ya uhalifu. Ikiwa serikali itanyamazia mauaji yanayotokea huko ya raia wasio na hatia dhidi ya askari nchi haitakalika.
Wananchi wanalalamika ndugu zao kuwawa na askari,kilio chao hakuna anaye kisikiliza kwa kuwa tu askari wako kwenye msako wa kumsaka muuaji,huenda muaji si Mkibiti au Mrufiji,iweje wauwawe familia za wasio na hatia wa Kibiti,ikiwa muaji amepatikana au laa,ni sahihi kujichukulia sheria mkononi kwa msako wa kuuwa wasio hatia!
Tume ya haki za binadamu iko wapi kuishauri serikali juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu,bunge kupitia mbunge wa Kibiti hamuoni kinachowapata ndugu zetu! Harufu ya damu inayonuka huko Kibiti nani ataisafisha na kuifanya Kibiti kuwa sehemu salama ya kuishi.
Viongozi wa dini mko wapi,maadili yamepoteza mwelekeo,watu wanauwana kama si watoto wa mama mmoja Tanzania. Kimya chenu kinaashiria nini, je ni uoga umewakumba au nchi yetu imeingia maagano ya kutoa damu,na kama ndivyo kwa nini hamsimami kwenye majukumu yenu ya kuamrisha mema na kukatazana mabaya.
Tubadilike kuinusuru nchi yetu, kila mmoja asimamie majukumu yake, kuua mtu kwa kuwa miongoni mwetu kuna waliouwawa ni kinyume na maadili ya haki za binadamu,na kwa kuwa nchi yetu ni miongoni mwa nchi zilizo saini mkataba wa amani Geneva wenye kulinda na kuheshimu haki za binadamu ni muhimu serikali kusimama imara kulinda haki za raia wake na kuwajibika kisheria kulinda utii wa sheria bila kuathiri haki za binadamu.