Haki za Binadamu nao watoa tamko

Haki za Binadamu nao watoa tamko

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,116
Reaction score
34,960
kibanda.jpg


KWA UFUPI
"Takribani ndani ya miezi 10 sasa, zaidi ya watetezi wa haki za binadamu 10 wakiwamo waandishi wa habari wameshajeruhiwa, wamepata vitisho au kuuawa."

Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu ambao ni mkusanyiko wa asasi zaidi ya 70 za kiraia zinazotetea haki za binadamu (THRD-Coalition) , kwa kushirikiana na Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC),vimeelezea kulaani vikali shambulio la kinyama alilofanyiwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda.

Uchunguzi tulioufanya bado haujatujapatia habari za undani zaidi na uhakika wa tukio hilo, lakini kwa taarifa za awali kwa asilimia kubwa linahusiana na kazi yake ya utetezi wa haki za binadamu kupitia taaluma yake ya uandishi wa habari.

"Tunasema hivyo kwa sababu vitisho dhidi ya wanahabari na watetezi wengine wa haki za binadamu,vinataka kuzoeleka sasa hapa nchini jambo ambalo halikuwapo katika miaka ya nyuma.

"Takribani ndani ya miezi 10 sasa, zaidi ya watetezi wa haki za binadamu 10 wakiwamo waandishi wa habari wameshajeruhiwa, wamepata vitisho au kuuawa."

Ilisema taarifa hiyo iliyosainiwa na Onesmo Olengurumwa, Mratibu wa Mtandao huo kuwa matukio hayo yanaashiria lengo la kutaka kuzima sauti za watetezi wa wanyonge kwa visingizio mbalimbali na wakati mwingine matukio haya yakipewa sura tofauti ikiwamo uhalifu wa kawaida, visa vya kudhulumiana na visasi vya kimapenzi.

"Hatupendi kuingilia wala kukwamisha utendaji kazi wa jeshi hilo, lakini pia hatupendi wanahabari na watetezi wengine wafanye kazi yao katika mazingira ya woga. Tunaamini kwamba zipo njia muafaka zaidi za kushughulikia masuala yanayohusu taaluma ya habari," ilisema taarifa hiyo.

Mtandao huo umewataka watu wote wanaotumika au wanaoendeleza wimbi la mashambulizi kwa wanahabari na watetezi wote wa haki za binadamu kwa ujumla, waache kufanya hivyo kwani wataliingiza nchi katika machafuko makubwa pamoja na kuisihi Polisi na Serikali kubeba jukumu lao la kuhakikisha usalama wa watetezi wa haki za binadamu, na raia wote. chanzo. Haki za Binadamu nao watoa tamko - Kitaifa - mwananchi.co.tz


 
tutalishwa matamko mpaka tukome kwa uzalendo unaogarimu maisha naona Tanzania ya Matamko.

Wanajamvi kazi kwetu tujadili matamko nasi tuwe Wanachama wa Matamko Tuendeshe nchi kwa matamko bila kuadhiri uchunguzi unaondelea wa kulimbokiwa, kumwangosiwa na kubanduliwa
 
Jamani haya matamko watanzania yanatusaidia nini haswa!? Ningefurahi sana kama matamko yangeambatana na mikakati ya kukabiliana na serikali hii goigoi isiyojishughulisha kabisa na usalama wa raia wake. Ningefurahi kusikia wanaharakati wanakwenda Dodoma kuwahamasisha wabunge wapige kura ya kutokuwa na imani na serikali hii goigoi ambayo ndani ya uongozi wake tumeshuhudia mauaji ya kila aina. Ningefurahi wanaharakati wakiandamana kuelekea ofisi za UN kuomba nao waingilie kati au kuitaka serikali itoe maelezo kwa nini imeacha wananchi wake wauawe kama kuku! Bila kufanya hivyo, matamko hayana maana.
 
Matamko juu ya matamko. This is very common nowdays. Hawa wanaharakati wa Tanzania wanaanzisha hizo NGOs kwa ajili ya njaa zao msidhani wana msukumo wa dhati kwa kusaidia jamii. Wanaharakati gani wanashindwa kuitisha maandamano ya kuiondoa serikali dhalimu iliyopo madarakani badala yake wanaitisha maandamano ya kuitetea serikali eti twende ubalozi wa uingereza tukawalalamikie kwa nini wanadhalilisha serikali ya kikwete. Wanaume wenzangu wa kitanzania wamekuwa waoga hadi mnazidiwa ujasiri na mama Hellen Bisimba na Ananilea Nkya? Hebu twendeni Dodoma tukakeshe nje ya viwanja vya bunge huku tukishinikiza ipigwe kura ya kutokuwa na imani hadi kieleweke watz tuache woga.
 
Sie watanzania ni wapole sana na tumejawa na ujinga pamoja na sifa zisizo na sababu, hatupendi kugombana wala kukamata watu, pale watu wa kawaida wanapoumizwa na wahuni waliotumwa na viongozi. Kiongozi akiumizwa tu ndipo serikali inakuja juu na kuanza kuwatafuta wahuni. Tuzidi kuichagua CCM tutapata tu maendeleo na haki zetu zitatetewa.
 
Sasa matamko bila action ni uhuni kabisa, watu wanapigwa na wanakufa tamko linasaidia nini? Ulimboka alipigwa mkatoa matamko, Mwangosi aliuawa mkatoa matamko na leo Kibanda amepigwa mmeungana kutoa matamko. Haya nyie wanamatamko mtuambie yanatija gani hayo matamko yenu?
 
hivi hao wanaotekeleza hayo mateso na mauaji,wanadhani wanauwezo wakusimamisha hizi harakati zinazo endelea nchini,haiwezekan maana huu ndio muda wake km watetezi wa watu wanawasumbua basi wabadilike kwan kwa dunia ya leo wapenda haki lazima watakuepo tu.je wetawaua na kuwatesa mpaka lini?nchi ya kidemokrasia ni yakusikiliza na kuheshimu fikra tofauti.
 
Back
Top Bottom