detective mfaume
Member
- Dec 23, 2016
- 31
- 69
*HAKI YA USHOGA TANZANIA*
Je nikwel kwamba sheria za Tanzania zinatambua haki ya ushoga?
Vipi kuhusu haki ya mtu kutumia mwili wake atakavyo?
Na
Mfaume Hassani Hamadi
Mwanafunzi wa shahada ya usimamizi wa sheria UDSM.
Kumekua na watu kadhaa wakiwemo baadhi ya mawakili wanaotaka kujaribu kutetea ushoga Tanzania.
Umoja wa mataifa kupitia balozi wake anayesimamia haki za binadamu Michelle Bachelet, na Shirika la kutetea haki za binadamu (Amnesty International) kupitia Mkurugenzi wake katika kanda Afrika Mashariki, Pembe ya Afrika na nchi za Maziwa Makuu Joan Nyanyuki, wamelaani juhudi zinazofanyika Tanzania katika kuhakikisha maadili ya nchi yanalindwa.
Makundi yote yanadai kwamba kudhibiti ushoga ni kuhamasisha chuki kati ya wananchi. Kuendeleza harakati za ubaguzi na uvunjifu wa Amani. Eti mashoga wanabaguliwa, na kubughudhiwa jambo ambalo si ni kinyume na haki za binadamu.
Lahashaa tusidanganywe tukakubali kuingiza jinamizi la aina hii Tanzania.
Jamvi la itikadi ya amani, usawa na haki za binadamu ndilo linalotumika kutuingizia tamaduni ambazo si asili yetu.
Jitihada hizi ndizo zinazotupa picha halisi kua mataifa ya magharibi yanataka kutuongoza katika nyanja zote ikiwemo kifikra na kitamaduni baada yakufanikiwa katika siasa na uchumi. Hili linafanyika kwa kutumia myamvuli ya umoja na mashirika tunayowekewa vibaraka na kutamkishwa maneno na misimamo ambayo ni kinyume na Imani na mila zakiafrika. Japo hatuwezi kukataa ukweli kwamba yapo mambo ambayo tayari tumekubali kuyafanya kua ni damaduni zetu lakini hili halitupi sababu yakukubali ushoga.
Tujiulize maswali kadhaa ili tuweze kujibu hoja za watetezi.
Je mashoga ni watu walio baguliwa kinyume na sheria?
Jibu ni hapana. Kwanza kabisa ushoga ni kosa la jinai Tanzania kama ilivyo katika jinai na makosa mengine. Sheria zetu haziruhusu ushoga na hii imeainishwa katika sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16.
Kama ilivyo falsafa yakuzuia uhalifu katika jamii. Moja ya adhabu inayotolewa na sheria ni kutenga wahalifu na kuwaweka mbali na jamii, ili kuepusha adhima na janga lao kwa watu wengine. Itambulike kwamba endapo tutaweka wahalifu na jamii nyingine wanaweza kuwafundisha watoto, dada, kaka, baba na mama zetu juu ya uchafu na uhalifu wao. Tutakapo endelea kulea kizazi cha mashoga katika jamii yetu, tujue yakwamba tutajenga jamii ya namna hiyo na ni watoto wetu watakao kuja kudhurika.
Je katiba ya jamhuri inatambua haki ya ushoga?
Jibu ni hapana. Licha ya katiba yetu kubeba haki za binadamu lakini haitambui haki yakutokubaguliwa kwa maana ya kuruhusu ushoga. Haki zote zakikatiba ziko chini ya masharti kadhaa ikiwemo sharti la kulinda maadili ya taifa. Hakuna dini, kabila ama tamaduni ya watu kokote Tanzania, inayoruhusu ushoga. Hii inatosha kuyaambia mataifa ya nje kua sheria mama ya Tanzania hairuhusu ushoga.
Vipi kuhusu mikataba ya kimataifa
Ni kweli kwamba Tanzania tume saini mikataba yakimataifa yakulinda haki za binadamu. Mikataba hii ni kama Mkataba wakimataifa wa haki za kiraia na kisiasa wa mwaka 1966, mkataba wakimataifa wa haki zakiuchumi, kijamii na kiutamaduni wa mwaka 1966, na mkataba wakutokomeza ubahuzi dhidi ya wanawake. Mikataba imebainisha haki kadha wa kadha.
Licha ya Tanzania kua wanachama wa mikataba hii, bado hailazimiki kukubaki ushoga. Mikataba imetoa mianya kwa nchi ambazo zinataka kua wanachama kuweka akiba ya baadhi ya vifungu ambayo haviendani na maadili ya nchi husika. Tanzania wakati wakusaini mikataba hii tulifanya vivohivyo kwa shabaha yakulinda maadili ya taifa.
Mikataba hii pia imeweka matakwa ambayo yanaweza kuzuia haki yamtu. Matakwa haya ni kwa maslahi mapana kama ilivyo katika katika ya jamhuri ibara ya 30. Maslahi kama, maadili ya nchi, usalama wa nchi, haki za wengine, na maslahi ya umma ni muhimu kuwekwa katika mizani na haki za binadamu.
```Siracusa principles``` na ```Limburg principles``` zinaelezea matakwa haya kwa mapana katika kutekeleza haki za binadamu.
Je mfumo unaotumiwa kwasasa kudhibiti ushoga ni sahihi.
Mfumo unaotumiwa kwa sasa kuwatangaza watu wanaodhaniwa kua ni mashoga mitandaoni ni kinyume cha sheria. Na hapa ndipo unapokuja ule mjadala wa niipi nafasi ya matumizi ya mtandao katika jamii, na ni upi umuhimu wa sheria za kudhibiti matumizi mabaya ya mitandao.
Kuwataja watu mitandaoni kama mashoga ni kuchafua utu, sifa na heshima yao katika jamii. Na waadhirika wanaweza kutumia mwanya huu kufungua kesi ya madai dhidi ya watajaji, endapo itathibitika kua taarifa zao ni za uongo.
Katika sheria kila mtu anadhaniwa kua hana kosa mpaka pale mahakama itakapothibitisha vinginevyo. Na kama mtu anatuhumiwa au kudhaniwa kutenda kosa, na ushahidi ukawepo, anatakiwa kupelekwa mahakamani sio mitandaoni.
Vipi kuhusu adhabu ya ushoga kua kubwa?
Adhabu ya wanaojihusisha na ushoga nikubwa na inapaswa kua hivyo ili kuzuia watu wengine kuiga tabia za ushoga. Hii ni moja pia ya kanuni katika falsafa ya kuzuia na kuonya jamii juu ya hatari ya kujihusisha na jambo au uhalifu fulani.
```Tunaunga mkono serikali katika jitihada za operesheni tokomeza ushoga Tanzania. Na pia tunaishauri serikali kutumia sheria na taratibu zilizopo katika kufanikisha jambo hili.```