Haki ya mwanaume kumchukua mtoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haki ya mwanaume kumchukua mtoto

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Nyakwaratony, Dec 29, 2011.

 1. N

  Nyakwaratony JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2011
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 575
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Hali zenu wana jamii forums?

  Naomba kueleweshwa kuhusu kisheria haki ya baba mtoto kumchukua mtoto afikapo umri wa miaka saba (7). Utakuwa mama mtoto kamlea mtoto wake kwa shida sana na kwa kujinyima thn baada ya miaka saba (7) baba wa mtoto ndo anajitokeza kutaka kumchukua mtoto eti ndo sheria inasema hivyo je ni kweli vipi kuhusu gharama alizotumia mama mtoto.......
   
 2. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,491
  Likes Received: 4,764
  Trophy Points: 280
  Ikiwa mmefanya tendo la ndoa nje ya ndoa...kisheria inatakiwa kipindi cha miezi tisa (au kipindi cha ujauzito) na mwaka mmoja baada ya mtoto kuzaliwa baba mhusika na ujauzito huo apeleke madai/utambulisho wa kuhusika kwake na ujauzito huo, ukiamua kutumia taratibu za mila na desturi utapewa masharti ya fidia kulingana na mila husika na hatimaye kuruhusiwa kulea mimba/mtoto huyo kwa maana rahisi utakuwa umehalalishwa baada ya kutimizwa masharti uliyopewa na mtoto huyo unatakiwa umutnze kwa maisha yake yote........kadhalika kwa mama mwenye ujauzito ikiwa baba muhusika atakataa ujauzito huo anaweza in the first place kutumia mila na desturi au kwenda mahakamani kwa kipindi tajwa hapo juu............ikiwa mazingira haya hayatafanyika kwa kipindi hicho (hasa baba) mtoto huyo atakuwa halali ya mama na baba muhusika hatatakiwa kuja tena ma madai ya mtoto (ingawa kimila inawezekana akatajiwa fidia yote na kukabdhiwa mtoto lakini isheria inakuwa time barred (limited by law)

  Baba aliyetimiza masharti ya awali anaweza kumchukua mtoto wakati wowote ikiwa atafauta hatua za kisheria na ikiwa mtoto ni chini ya miaka 7 basi anatakiwa atowe uthibitisho kwamba mama wa mtoto hawezi kumtunza mtoto huyo kutokana namazingira aliyomo (kutokuwa na kipato cha uhakika etc) aidha kwa kutumia uungawana anaweza kuendelea kumtunza mtoto huyo hadi afikie miaka saba ndipo anaweza kumchukua kwa taratibu za kisheria au kimila.

  Kwa fact ulizo-aduce hapa itategema huyo baba anamchukua katiaka mantiki ipi kama ilivyodadavuliwa hapo juu

  Karibu sana kwa msaada zaidi au waone kituo cha ustawi wa jamii/Baraza la Kata karibu yako
   
Loading...