Haki ya mtu husimamiwa na Mungu mwenyewe

ndege joni

JF-Expert Member
May 23, 2017
673
1,082
Habarini za leo watu wa Mungu
Kuna kisa nahitaji kuelezea ili mjue kuwa hata kama una nguvu au mamlaka kiasi gani huwezi kuzuia haki ya Binadamu.

Nilikuwa nafanya kazi kampuni moja, mimi na meneja tukawa kama Mbwa na paka. Ilikuwa kila ifikapo mwisho wa mwezi, nakatwa mshahara kisa nimetia hasara kampuni(siweki wazi vitu gani). Bahati nzuri hata wafanyakazi wenzangu waligundua hilo... mmiliki wa kampuni hakuwa anaishi karibu, so alikuwa anakuja mara moja moja sana kwa sababu ana matawi mengi duniani. Anaweza chukua hata miezi sita au zaidi kuja au atume watoto wake. Kuna siku alikuja mtoto wake na mmiliki wa kampuni, bahati nzuri alikaa kikao na wafanyakazi wote akiwemo meneja. Kutokana na alivyokuwa friendly watu waliongea yasiyoongelewa. Na mimi ilibidi nitoe ya moyoni kuwa miezi mingi nakatwa mshahara kwa mambo madogo. Bahati nzuri nilikuwa namzidi elimu meneja. Mtoto wa bosi alishangaa akauliza wengine.... wakanisapoti. Aliambiwa ahakikishe amenilipa mpaka senti ya mwisho na kumbe alikuwa anakula yeye kwa sababu taarifa zinaonesha nimelipwa. I was paid everything na hicho alichonilipa kumbe alitia hasara kampuni, saivi tunamkata salary kufidia. Nifupishe tu, Saivi mimi ni meneja, yeye ni mfanyakazi wa kawaida. I can do anything for him. Kawa mpole kama nini.

Nachohitaji kusema hata kama una mamlaka kiasi gani, haki ya mtu anasimamia Mungu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom