Decree Holder
JF-Expert Member
- Jul 19, 2015
- 2,556
- 3,741
Wataalamu wa sheria za haki za binadamu wamejaribu kuzigawa haki za binadamu katika makundi mawili makubwa nayo ni positive human rights na negative human rights.
Positive human rights ni haki za binadamu ambazo zinahitaji state interference ili mwananchi azipate. Haki hizi za binadamu zinahitaji juhudi kubwa upande wa serikali na ni wajibu wa serikali kuhakikisha haki hizi zinatekelezwa. Upatikanaji wa haki hizi huilazimu serikali kuingia gharama kubwa ya muda na fedha ili kufanikisha haki hizi. Mfano wa positive human rights ni right to life yaani haki ya kuishi, right to good health yaani haki ya afya, right to education yaani haki ya elimu
Kwa mfano ili wananchi wapate haki ya elimu ni lazima serikali igharamike kuanzisha mashule, kusomesha walimu, kuanzisha vyuo vikuu na hata kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu ili wasome. Ukiangalia gharama hizi ni kubwa sana ambapo serikali huincur, mfano mwingine upo kwenye afya ambapo serikali hugharamia kujenga mahospitali, kusomesha watumishi wa afya nk. Kiufupi ukisoma bajeti za wizara zinazohusu positive human rights utaona ni kubwa mno kifedha kutoka serikalini na wakati mwingine hata taasisi za private zinazoisaidia serikali kufanikisha haki hizi hupewa ruzuku na misamaha ya kodi. Yote hii inaonesha ni jinsi gani tunavyohitaji state interference kwenye positive human rights.
Kundi la pili la haki za binadamu ni negative human rights. Haki hizi za binadamu hazihitaji state interference ili mwananchi aenjoy, kwa negative human rights state interference may lead to conflicts. Serikali haitakiwi kuincur gharama kubwa sana kwenye upatikanaji wake. Serikali inachotakiwa ni kuregulate kuhakikisha kuwa wananchi wanaenjoy negative human rights bila kuvunja sheria za nchi. Mfano wa negative human rights ni haki ya kuabudu, haki ya kukusanyika, haki ya kupata habari nk. Serikali haihitaji kujenga misikiti au makanisa ili watu wapate haki yao ya kuabudu. Serikali haihitaji kuwajengea watu majukwaa ili wakakusanyike, hata katika haki ya habari serikali haihitaji kuingia gharama kubwa wala kuinterfere uhuru wa vyombo vya habari. Hata ukiangalia bajeti ya wizara ya habari iliyowasilishwa na Mh Nape jana haizidi bilioni 25 na fedha nyingi hapo ni kwa ajili ya chai na semina hii ni tofauti na fedha zilizotengwa kwenye wizara za afya na elimu.
Mara nyingi serikali ikiingilia angle za negative human rights lazima kutokee mgogoro na mkanganyiko kwenye jamii hii ni kutokana na nature ya haki zenyewe, rejea jaribio la serikali la kuingilia kati haki ya kuabudu kutaka kuanzisha mahakama ya kadhi mkanganyiko mkubwa ulijitokeza. Hata pale serikali ilipojaribu kuingilia uhuru wa watu kukusanyika kupitia jeshi polisi mwisho wake ulikuwa vurugu tu, rejea kilichotokea Arusha. Mkanganyiko unaoendelea sasa wa matangazo ya bunge kwamba yawe live au recorded ni jaribio la serikali kuinterfere enjoyment of negative human rights. Serikali kama kweli haina fedha za kugharamia live broadcasting ya bunge kupitia TBC1 ni sahihi kutokuonesha kutumia TBC1, lakini haikuwa sahihi hata kidogo kuvizuia vyombo vya habari vya private kurusha live matangazo ya bunge kwani havitumii gharama za serikali!
Ni ajabu kuona serikali inaacha kujishughulisha na positive human rights, ambapo hali ya huduma za afya na elimu si ya kuridhisha yenyewe inapoteza muda na gharama kuzuia vyombo binafsi kuonesha bunge live yaani inainterfere negative human rights!!!
Siku njema!!