Haki na Amani

Haki na Amani

mtwana

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
428
Reaction score
141
Tupo ukingoni mwa zoezi letu la kupiga kura kwa kuchagua viongozi wataoweza kutuvusha katika miaka mitano mengine
Dhima ya kuingia kwenye uchaguzi ni wananchi kuchagua kiongozi wanaomfaa na kumchagua yupi ataeweza kuleta maendeleo.

Suala la kuchagua kiongozi sio jambo la mtu kulazimishwa amchague huyu au amuwache huyu, ni hiari ya mtu kuchagua na kutochagua. Ama katika kuchagua huko kuna chombo ambacho kiko huru katika kutoa majibu ya uchaguzi huo nayo ni Tume ya Uchaguzi kwa hakika tume hii ipo kwa mujibu wa sheria za nchi na haipo kwa ajili ya kumfurahisha fulani na kumliza fulani.

Ninaamini Tume hii itasimamia uchaguzi huu kwa huru na haki bila ya kuingiliwa na upande wowote katika maamuzi hayo
Bila haki hakuna amani nami naamini Haki itandeka ili amani tuliyokua nayo isiondoke

Namuomba Mwenyezi Mungu atuletee viongozi wazuri wenye kutuletea maendeleo na asijaalie hata siku moja amani tuliyokua nayo ikapotea na ajaalie haki itendeke kwa kila mmoja wetu
amin
 
Back
Top Bottom