Haki: Mwizi wa kuku afungwe

Idd Ninga

Verified Member
Nov 18, 2012
4,785
2,000
MWIZI WA KUKU.

1)Haki wala hina macho, na ndo mana haioni.
Haki imewa kificho, imeshia kitabuni.
Mwizi wa kuku afungwe, mchota hela aringe.

2)haki imewa zindiko, lifanyiwalo porini.
Haki kama sikitiko, kwa walio masikini.
Mwizi wa kuku afungwe, mchota hela aringe.

3)haki yatazama pesa, haipo mahakamani.
Haki wengi yawatesa, yaachwa hadi bungeni.
Mwizi wa kuku afungwe, mchota hela aringe.

4)haki ni kama mzimu, uliotupwa motoni.
Haki kuipata ngumu, kama uhai vitani.
Mwizi wa kuku afungwe, mchota hela aringe.

5)haki yatazama cheo, mahakimu hawaoni.
Haki nayo kichocheo, watu kwenda gerezani.
Mwizi wa kuku afungwe, mchota hela aringe.

Shairi=MWIZI WA KUKU AFUNGWE.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160.
iddyallyninga@gmail.com
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom