radika
JF-Expert Member
- Jul 15, 2014
- 20,450
- 32,293
Amani iwe kwenu Waheshimiwa.
Alhamisi ya tarehe 25/1/2018 nikiwa Dodoma ktk vikao vya Kamati ya Bunge, nilipigiwa simu na wananchi wa Limalyao kuwa Polisi wamevamia usiku wa manane ktk majumba yao na kuwakamata wananchi wanne, nakuwafikisha kituo cha Polisi Kilwa Masoko.
Nilimpigia simu Afisa Upelelezi OC CID wa Wilaya ya Kilwa na kunithibitishia ni kweli na wapo kituoni Kilwa Masoko. Nilipo muuliza tuhuma zipi walizokamatiwa, alinijibu "ni kweli na tuhuma ya ugahidi lakini ni msako maalumu unaongozwa RCO wa Lindi, lkn yeye hana Madaraka nao, ukihitaji zaidi mapigie simu",
Nikampigia simu RCO wa Lindi naye akanithibitishia ni kweli na akanambia, "wengine wamekimbia na akaniuliza "kwa nini wakimbie" mimi nikamwambia Kukimbia ni muhimu kwa hali halisi ya nchi yetu ya Utekwaji wa watu na watu wasiojulikana na kupelekwa kusiko julikana, lkn nikamfamisha kwamba, nitawafahamisha na kuwaomba hao waliokimbia waje Polisi Kilwa Masoko kwa RCO Lindi, akaniambia itakuwa vizuri zaidi.
Kweli niliwafahamisha na kuwaomba wafike Polisi Masoko, wakanikubalia na wananchi takribani wanane, siku ya Ijumaa wakafika Polisi Kilwa Masoko; nikafahamishwa na wao pia wamewekwa mahabusu.
Nikamfamisha RCO kuwa mimi nakuja Kilwa na Mwanasheria naomba wahojiwe watuhumiwa mbele ya Wakili? RCO akanikubalia kwa kuniambia hiyo ni Haki yao ya msingi hatuwezi Kuizuia.
Tulifika Polisi Kilwa Masoko mimi na Mwanasheria, Wakili, Hashimu Mzirai na kufahamishwa kuwa watuhumiwa tisa wamepelekwa Lindi na watuhumiwa watatu wamebaki hapa, tuliomba tuwaone hao watuhumiwa watatu na tukawaona na kuongea nao, wawili walikuwa wanawake na mmoja mwanamume na walitufahamisha kuwa walikamatwa Usiku wa manane na Polisi wasiopungua 15 waliovalia sale za Polisi na waliovaa kiraia bila kuwaambia kosa lipi wanalotuhumiwa.
Baada ya kuongea nao tukaamua tuwafuatilie watuhumiwa waliopo Lindi na nikamfaamisha RCO wa Lindi kuwa ninakuja Lindi pamoja na Mwanasheria hili wahojiwe mbele yake akaniambia sawa.
Jumapili tarehe 28/1/20218 saa 3:40 tulifika Lindi, nikampigia simu RCO wa Lindi lkn simu yake haikupatikana, tukaamua kwenda kituo cha Polisi Lindi na tukajitambulisha na kuomba kuwaona watuhumiwa. Jibu tulilopewa ni kwamba, hatuwezi kuwaona isipo kuwa kwa idhini ya RCO, tena, tukampigia RCO kwa mara kadhaa lkn simu yake ikawa haipatikani.
Tukamfaamisha RPC, nae akatujibu tumsubiri RCO hapohapo anakuja, lakini mpaka muda wa saa Saba mchana, hakuwa amefika.
Mwanasheria akampigia msaidizi wa IGP na mi mi nikampigia Naibu Waziri wa mambo ya ndani, Mhe Masauni, kumfahamisha kuwa tupo hapa kituo cha Polisi Lindi kuomba kuonana na watuhumiwa tangu saa 3:40 na sasa ni zaidi ya masaa 4 sasa hatujafanikiwa kuwaona, tunaomba msaada wenu.
Baada ya muda mchache RCO akanipigia simu na kunifahamisha kuwa watuhumiwa wanahojiwa nje ya hapo kituoni, tunategemea kuwarudisha hapo saa 12 jioni na ndipo mtapata nafasi ya kuwaona. Tukamwambia sawa, tutafika hiyo saa 12 jioni.
Saa 11:45 tulimpigia simu RCO simu ili tujuwe kinachoendelea, lkn simu iliita kwa muda mwingi lakini haikupokelewa tukaamua kwenda kituo cha Polisi Saa 12:00, tukafika na kumkuta OCD, tukamfaamisha tatizo letu ni kuwaona watuhumiwa walioletwa kutoka Kilwa Kijiji cha Lihimalyao; Mzee Mbwana Mohamedi na wazake wanane, ambapo tuliambiwa na RCO watuhumiwa watakuwepo hapa saa 12 ili tuwaona.
OCD akatufahamisha tumpigie simu RCO tumfaamishe, tukampigia simu, lkn simu ikawa inaita lakini haipokelewi na nikapiga tena mbele yake pia iliita lakini haikupokelewa, baadae akafika OC CID, yeye akatufahamisha kuwa nimeandikiwa msg na RCO kuwa watuhumiwa wamehojiwa baadhi na wengine hawaja hojiwa kwa hiyo hamuwezi kuwaona na kuongea nao, isipo kuwa munaweza kuwaletea Chakula ili wajuwe uwepo wenu.
Baada ya kauli hiyo tukampigia msaidizi wa IGP Sirro akatuambia tumpe simu OCD ili aongee naye tukampa simu OCD, akasema mimi sina mamlaka ya kuongea nae, Nikamfamisha akasema basi nitampigia RCO wakati tunasubiri majibu ya Msaidizi wa IGP kutoka kwa RCO, tuliwapa Chakula watuhumiwa wote kwa hiyo tukahakikisha watuhumiwa wapo kwa kutumia njia ya kuwapatia Chakula lakini mpaka leo tarehe 29/1/2018 saa 05:25 hatujafanikiwa kuongea na watuhumiwa hao.
Nafikiri hatukutendewa Haki kama tunaambiwa ni Haki ya mtuhumiwa kutoa maelezo mbele ya Mwanasheria na RCO wa Lindi tulimwambia na akatukubalia kufika Lindi na tulipo fika Lindi RCO hataki kuonana nasi pia kuwaruhusu OCD na OC CID kuwaona watuhumiwa, na watuhumiwa kujieleza mbele ya Mwanasheria.
Hilo ndilo Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania walinzi wa Amani wa raia na mali zao.
Seleman Bungara Bwege (MB)
Mambo ya kutekana ktk Taifa hili bado yanaendelea hao wamefahamika je wasiofahamika wanapotelea wapi? Inatia mashaka sana amani ya Taifa hili tunaoishi kwa kubahatisha tuendelee kumshukuru Mungu sana.
Kesho huenda ikawa zamu yako
Mbunge tu kazungushwa hivyo.