OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,073
- 114,571
Msemaji wa Simba SCC Taifa Kubwa Haji Manara-Scorpion ametamba kuwa Simba watachukua makombe hatua kwa hatua.Haji amesema kuwa walianza na Simba B ambao juzi kati wamechukua kombe,kinachofuata ni Kombe la Mapinduzi na VPL.
Manara ametamba kuwa kipigo cha Yanga juzi ulikuwa maandalizi ya kuichapa Yanga vizuri katika mechi yao ijayo katika ligi ya Vodacom. Manara amepongeza marefa wa Zanzibar na hakuna malalamiko tofauti na ligi kuu bara ambapo makocha wamekuwa wakinyooshewa vidole.
Manara ameshangazwa na kitendo cha Yanga kukata kupeana mikono na wadau baada ya mechi yao na Simba. Ikumbukwe kuwa mtangazaji wa Azam alilamika kukimbiwa na wachezaji wa Yanga wakati wa kufanya mahojiano baada ya mechi