Haji Manara anatafuta nini zaidi? Nani yuko nyuma yake?

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,049
4,904
Wakuu wapenzi wa soka na haki za binadamu hili linawahusu!

Psychologically, Manara inaonekana ana jaziba juu ya adhabu aliyopewa, yawezekana ameonewa lakin professionally hatumii hekima, Ni kama kuna mtu (ambaye anamaslahi binafsi na TFF) Yuko nyuma yake anampampu, maana pengine anajiona anawaexpose Karia na TFF lakini kwa msomi anaonekana anaropoka!

Kwa nini anataka attention ya watu kwa social media na si kufuata utaratibu wa kukata rufaa kupinga maamuzi?

Kwanini pamoja na maamuzi yaliyotolewa bado anatoa kauli za kuwa against nayo kana kwamba TFF na Manara mkubwa Ni Manara?

Kwanini Manara badala ya kutoa misimamo itakayoenda kuzima Moto lakini anatokwa na maneno ya kuukoleza Moto? Ni nani aliye nyuma ya pressure aliyonayo Manara?

Screenshot_20220725-160811.jpg
Screenshot_20220725-160811~2.jpg
 
Tatizo hauja sikiliza umekuja tu kanzisha uzi ukiwa bias huwezi elewa mimi nlikua namuona Haji ana matatizo ila kwa hio press nmepata picha hapo TFF pana shida
Ni kweli , yawezekana TFF pana shida kubwa, lakini lazima tubalance story, hatuwezi kuhukumu mgogoro huu kwa kusikiliza A to Z ya upande mmoja!

Pili, ingekuwa ni wewe, professionally ungelitatuajw hili? Ungefanya ubabe kama Manara anavyofanya au ungelifuatilia kisheria zaidi?
 
Kitabia Haji ni mtu asiyekubali kushindwa.

Najaribu kuwaza hivi Rais Magufuli kipindi kile alikuwa akitukana na kudhalilisha viongozi wa chini yake kila walipovurunda kwenye utendaji, Sasa nao wangeweka kibesi na kumdindia Rais - ni nini kingetokea?.

Ukiwa mtoto utaendelea kuwa myonge tu hata kama Baba yako anachokifanya ni cha kukuonea. Usipomheshimu Baba yako anaweza kukuchapa viboko na matusi juu. Watoto watukutu ndio wenye ujasiri wa kumrudishia matusi Baba.

Nashauri kamati ya TFF Imuongezee adhabu huyu mtu, maana bado anajiona ni mkubwa na yupo juu ya zaidi ya TFF iliyomuadhibu.
 
Kitabia Haji ni mtu asiyekubali kushindwa.

Najaribu kuwaza hivi Rais Magufuli kipindi kile alikuwa akitukana na kudhalilisha viongozi wa chini yake kila walipovurunda kwenye utendaji, Sasa nao wangeweka kibesi na kumdindia Rais - ni nini kingetokea?.

Ukiwa mtoto utaendelea kuwa myonge tu hata kama Baba yako anachokifanya ni cha kukuonea. Usipomheshimu Baba yako anaweza kukuchapa viboko na matusi juu. Watoto watukutu ndio wenye ujasiri wa kumrudishia matusi Baba.

Nashauri kamati ya TFF Imuongezee adhabu ya kifungo cha maisha huyu mtu, maana bado anajiona ni mkubwa na yupo juu ya zaidi ya TFF iliyomuadhibu.
Na amevuka mipaka anamtuhumu waziri Mchengerwa kuwa ndiye ameshinikiza yeye kupewa adhabu hii. Huyu akapimwe akili yaelekea jani limeshaharibu ubongo wake
 
Back
Top Bottom