Haja ya kuwa na Machapisho ya Jamii Forum | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haja ya kuwa na Machapisho ya Jamii Forum

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Chizi Fureshi, Jan 5, 2011.

 1. Chizi Fureshi

  Chizi Fureshi JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,710
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Wana jamvi, nimekuwa nikisoma sana mabandiko humu ndani na wakati mwingine nami hubandika. Elimu iliyomo humu imetufaidia sana tunaoweza kuingia mtandaoni na wachache tukutanao katika vijiwe vya kahawa, mama muuza,kwenye mambo yetu yale, n.k. Kwa upande wangu naona kama eneo kubwa la watanzania halifikiwi na ujumbe/mchango mzito wa wana jamii forum. Ushauri wangu sasa, naomba tuwe na utaratibu wa kuandaa vijarida, machapisho au vitabu vitakavyo jumuisha michango yote ya mawazo juu ya mambo ya msingi katika uhai wa Taifa letu. Kwa mfano, tukitoa kitabu juu ya mchakato wa kupatikana kwa KATIBA MPYA kuonyesha ni jinsi gani wana jamvi wanavyoshiriki kwa dhati.
  Naomba kuwasilisha.
   
Loading...