Haiwezekani tukawa hivi!

Edson

JF-Expert Member
Mar 7, 2009
9,846
5,076
Haiwezekani tukawa hivi, wote tukawa hiv, yaan nchi nzima tukawa hivi! kwa nini tuko hivi lakini?

nchi nzima tumekuwa tukilalamika,tunaona maovu yanafanywa na viongozi wa juu, kila kitu kimekwisha, tuona, tusema lakini tatizo moja hatuko siriaz. ndo maana tuko hivi. wengi wetu tunasuburi mtu fulani ndo aanze kuleta mabadiliko, wengine tuko pembeni tunaangalia tu, wakati huo huo wote tunaumia lakini hatutaki kuchuka hatua madhubuti wote kama kundi.

ndio maana tuko hivi. mabaya mangapi nchi yetu inafanyiwa tunaona, tuanaanza kuguna guna, tunalalamika lakini hatua madhubuti hakuna.wengi wetu mmeona ripot ya merermeta kwa wale ambao hawakupata kwa njia ya kununua mzee mzima mwanakijiji ameitoa bure, si ajabu kuna watu wanayo lakini wamesoma sura ya kwanza wakaachia hapo,

kwa wale amabao wameisoma na kuielewa sasa mda wa mabadiliko umefika na hapa hakuna kutupiana lawama na kusubiri wengine waanze kuleta mabadiliko,maana ndio tatizo letu.kuna watu wanamlaumu mwalimu Nyerere, eti ndo amesababisha umasikini nchi hii.sasa hebu ona miaka mingapi baba wa wa Taifa ametutoka? nchi hii imepiga hatua yoyote? tuache lawama zisizo na msingi.yuel mzee amefanya kazi sana na tena tumuache apumzike.

juzi hapa nilikuwa nasoma thread moja ya Rev. kishoka nadhani bado ipo humu kwa wale ambao hamjaisoma isomeni.yule bwana kaanadika mambo ya msingi sana.ngoja ninukuu , anasema hivi''Kwa hiari yetu wenyewe, kwa kutumia nguvu zetu wenyewe, kwa akili zetu na utashi wetu ulioambatana na upofu uliojaa tamaa, uvivu, usengenyaji na uroho, Tumeuza Uhuru wetu na hazina yetu tumeifuja.'' kisha akaendelea kusema '' Siwalaumu viongozi pekee, bali lawama za kwanza ni kwangu mimi (na wewe), niliye mjinga ambaye kwa upumbavu nimekimbia majukumu yangu na wajibu wangu niliopewa na Mola na kulindwa na Katiba ya Nchi yangu, kwa kuuza haki yangu ya kupiga kura kwa kukubali kuburuzwa kwa kulishwa andazi na chai.

Laiti ningekuwa mjasiri na kuitafuta kweli na haki na hata kuamua dira ya Taifa langu kwa kutumia umakini na busara, leo hii nisingekuwa hapa nikiangua kilio na kujitwisha mavumbi nikiwa nimevaa kaniki, nikihangaika kwa tabu na mateso, njaa na magonjwa yakiniwinda kwa urahisi nami nikawa mkimbizi wa ardhi niliyopewa na muumba.''

hapa Rev kishoka amesema kweli, wengi wetu tunatupa lawama kwa viongozi tena amabao tumewachagua wenyewe.mimi huwa najiuliza sana, inawezekanaje mtu amejiuzuru wadhifa tena uwaziri mkuu, anarudi kwao anapokelewa kama mfalme!!! kuna akili hapo?

jukumu nil kila mmoja wetu kusema hapana, kwa nini lakini tuchague watu wasio makini? natoa wito kwa watanzania wenzagu kusema hapana uchaguzi ujao kwa wote wanaosababisha matatizo haya. uwezo tunao wa kufanya hivyo

lakini pia lazma niseme ukweli nchi yangu watu wake si wakweli, waoga waongo na wanafiki wengi, maana haiwezekani kwa kiongozi mzima kama spika kusita kuwataja mfisadi na kuanza kusema wapo watatu tena ni wahalifu sugu. huu ni unafiki hapo hapo analiklia kuongzewa ulinzi. huyu angekuwa muwazi awatajer ili tujue kweli hata kama tunamuongezea ulinzi inakuwa sahihi.

wapo na wengine wengi wenye tabi kama hizi za sita, huu ni Ujinga. tukiamua tunaweza hata ikitupasa kutoa ''sadaka kubwa'' lakini lazima mabadiliko yaje mwakani, awe raisi, mbunge. na nimesikia kuna uchaguz wa madiwani mwaka huu huko, mzee wangu aliniambia alipokuja huku kunitembelea, tuanze na hawa maana wapo wengine wasumbufu sana.

Mi mpaka hapa nilipo sijawahi kuona mwenye HAKI anaachwa na Mungu na wala watoto wake kuwa omba omba barabarani, Mungu ni mwaminifu kwa watu wake, ametupa utashi lazima tuvitumie kufanya mambo ya maana, juu ya hatma ya nchi. sio kukaa tunalia lia tuuuuuuu wakati akili tunazo.

tufanye kazi kwa bidii kila mmoja kwa nafasi yake, lakini lazima busara iwepo, maana unaweza kufanya kazi kwa bidii kumbe ile bidii ni adhabu kwa maisha yako yote, fanya kazi huku ukifakari hatma ya nchi mwakani wakati wa uchaguzi sema hapana kwa mafisadi wote.

Naomba pia nimuombe Raisi kama ana wazo la kugombea mwakani nimuombe alipitie upya maana yeye ndo chanzo cha yote.haiwezekani hosea na mwanyika wakapona juu ya sakata la richmond, amemfanya hata pinda apinde, hafanyi kazi zake vizuri maana nae ni mtoto wa kufikia(kama shibuda alivyosema).Raisi amekuwa na fadhila sana,kipindi flani alisema kwa kimombo hivi ''i have a smilling face but firm on issue'' . simwamini sana maana naona smilling face tu hili linginge silioni.

Mwisho Niwatakie kazi njema wote huko nyumbani, tufanye kazi kwa bidii sana na tupige vita ufisadi wa aina yoyote ile.mwisho niwaachie swali ambalo baba aliniuliza. eti ni kwa nini watanzania wengi wana stoo za mkaa na si stoo za chakula??!
 
Back
Top Bottom