Haiwezekani kushusha thamani ya dola ya Marekani

Haiwezekani kushusha thamani ya dola ya Marekani

Linganisha na kauli hizi:
1. Titanic haiwezi kuzama kamwe; hata Mungu hawezi kuizamisha.

2. Dola ya Babeli (baadaye wakasema Rumi) haitoweza kuangushwa kamwe.

3. Michael Jackson hawezi kufa.

4. Korona haiwezi kuisha.

5. Makao makuu ya Bongo hayawezi kuhamia Dodoma.
Una akili sana mkuu
 
Lakini hawana nguvu za kutetea na kulinda fedha zao.

Marekani kwa nguvu alizokuwa nazo, aliweza kuiaminisha dunia kwamba makaratasi yake yana thamani zaidi kuliko dhahabu yetu ya Geita, Almasi ya Mwadui, Tanzanite Mererani, Gesi ya Mtwara, mbuga za wanyama, mito, maziwa na bahari, na hivi karibuni kabisa, viwanda vyetu vya sukari.
Hapana mkuu, $ nguvu yake ipo kwenye ucelebrity. Yaani kila unapogeuka ipo. Ilianza kutokushikika baada ya mataifa kukopeshana kwa $. Hii ilisababisha demand ya $ ikapaa mno, maana nchi zina madeni interm of $ na zinahitaji $ kuyalipa. Hapa ndipo mtego ulipo, Sarafu mpya yoyote ikiweza kutegua huu mtego $ inakufa kifo cha mende, ndembe ndembe.
 
Dunia inasogelea matumizi ya sarafu moja japo muda bado. Upo sawa kuwa $ ina nguvu na ndio giant wa sarafu dunia ya leo, ila kusema kuwa sarafu mpya zitafeli kabla hata hazijaanza matumizi ukaona udhaifu na uimara wake hayo ni mahaba mkuu.
Hakuna mahali nimesema sarafu mpya itafeli, but nimeelezea how US wamepita kuifnaya sarafu yao iwe juu
 
Sasa kwa namna China anavyoshika masoko ya dunia nani atanunua bidhaa za kibeberu kwa bei mara 2 ya china?🤣
Watu hawajui kama US na EU wenyewe bado wananunua Crude Oil Urusi wanafikiri wakienda kununua wanatumia Dollar au EU currency? Wananunua kwa Rubble maana US alishawekea vikwazo reserve yote aliyonayo Mrusi ya Dollar hatoweza kuitumia popote.
 
yuma ya tawala mbalimbali za dunia, kuna nguvu inayotenda kazi kisirisiri. Direction ya dunia inatokana na hii nguvu.

Hapa duniani tupata matokeo tu. Hii nguvu ndiyo yenye mamlaka ya nani aongoza dunia. Au taifa gani lipewe nguvu ya kuongoza dunia. Mambo yote Yanapangwa na hii nguvu.

Mipango yote ya viongozi wa dunia hii kujaribu kupanga mikakati Yao kinyume na hii nguvu inafeli. Mfano ni baadhi ya mataifa kufanya mikakati yao ya kuongoza dunia kinyume na hii nguvu inafeli vibaya. Majuzi tu hapa kwenye mkutano wa BRICS, viongozi wamejaribu kutambulisha SARAFU mpya ya BRICS ili iondowe utawala wa Dollar. Hiyo itafeli. USD Itaendelea kuwa na nguvu.

Tusijisumbuwe, Dollar bado IPO, USA bado IPO sana.

Ufalme wa MAREKANI una mizizi milefu sana kung'olewa ni ngumu sana.
Dunia inapitia mizunguko na ukiishi kipindi cha zama fulani unaweza kuhisi zitadumu milele. Kama mtu aliyeishi enzi za Roman empire ungemwambia kuwa siku moja Roma itaanguka bila shaka asingekuelewa inawezekanaje dola ambayo imetapakaa mabara yote ianguke.
Mtu aliyeishi zama za Ottoman empire naye bila shaka asingeweza kukuelewa ukimwambia Ottoman itaanguka maana ni kitu ambacho kilikuwa haki make sense at all.
Kabla ya dollar kuwa reserve currency ilikuwepo British pound sterling na bila shaka hakuna mtu ambaye angefikiri kuwa itafika siku itaanguka.
Mambo huwa yanaenda taratibu yani anguko la madola huwa si la siku moja.
Hebu fikiria, US na Europe kwa sasa wameacha kuimba wimbo wa free market sasa wanaimba kuweka tarriff kwa bidhaa za china hasa EVs. Hii inamaanisha kuwa badala ya kufanya ushindani wa innovation, wameshindwa sasa wanahamia kuweka vikwazo ili wananchi wao wasinunue hizo bidhaa maana zitaua bidhaa za soko lao. Miaka kadhaa nyuma wao ndio walikuwa wanahubiri free trade.
Inawezekana kuanguka kwa dollar lisiwe tukio la miaka michache, lakini tunakoelekea litatokea.
 
Linganisha na kauli hizi:
1. Titanic haiwezi kuzama kamwe; hata Mungu hawezi kuizamisha.

2. Dola ya Babeli (baadaye wakasema Rumi) haitoweza kuangushwa kamwe.

3. Michael Jackson hawezi kufa.

4. Korona haiwezi kuisha.

5. Makao makuu ya Bongo hayawezi kuhamia Dodoma.
Hata mimi niliwaza yule mama alivyomkali na kunifokea sitakuja kumpiga PARA,,, wapiiii....
Kama vile namsukuma mlevi shaaaa
Upwiru nehii 🙂 🙂 🙂 :NyanLove:🙂:NyanLove::ClapHD:
 
Mbona kuna fedha nyingi zenye thamani zaidi ya Dollar hamzizungumzi?

Kama ukikosana na US anaweka anakuwekea vikwazo kupitia hela yake ata hiyo reserve uliyonayo anahakikisha huwezi kuitumia kuna haja gani yakuendelea kuitumia kama bank reserves kwa wale ambao wataona haiwafai?

Leo hii sisi nchi nyingi za Africa tunaenda kununua bidhaa China na Duba(UAE) hawa wawili ni wanachama wa Brics tuambie kwanini tusiweke Brics currency katika hazina yetu? Brics pia ina bank yake ambayo itakuwa inatoa mikopo ya fedha utaniambia ukienda kukopa huko utapewa USD? Mnaenda kununua vifaa vya jeshi huko Urusi utaenda na USD? basi kama sivyo hivyo vitakuwa vichocheo vya kushuka kwa mahitaji ya Dollar.
Tanzania ina deni LA zaidi ya billion 40 za Dola ya Marekani...

Marekani na China wanafanya biashara ya thamani kubwa kuliko China na vitaifa vyote vya BRICS..

Tanzania ukiwa na hazina ya sarafu ya BRICS unalipaje deni lako la Dola?
 
Ok mkuu, $ Sarafu ipo juu ila ipo juu sababu ya nchi nyingine ikiwemo China kuitumia. Kuanguka kwake kutatokana na hilo hilo hivyo usiunderestimate nchi kama China zinapojaribu kuanzisha sarafu.
Once again, hakuna mahali nime underestimate, na si kweli kwamba china tu ndio inatumia US$
Unajua ni nchi ngapi zinafanya transaction in USD?
China pekee haitoweza kushusha, kunahitajika multiple countries, and thats when diplamacy na relations ina play part kubwa.
Haitokuwa rahisi kama unavyodhani
 
Atakayeshinda ni yule atakayezalisha zaidi, hapa sio suala la kuwa na pesa yenye nguvu tu kuliko US hiki sio kigezo maana ziko pesa zina nguvu kuliko US katika exchange tu sio kiuchumi. Brics wakiwa wazalishaji wakubwa kwa maana mahitaji na wakajitosheleza hapo nguvu ya dola au mahitaji yatapungua. Nadhani vita ya kiuchumi ni kubwa ila Brics wakijikita uzalishaji wakauziana mahitaji wao kwa wao hii itaumiza US kwa kiasi. Chukulia mfano leo sisi TZ tuwe tunahitaji bidhaa na zote zinapatikana katika Brics na Yuan onakubalika kibiashara utakuwa maduka ya fedha yana change zaidi Yuan au Brics currency. Kwa ufupi uzalishaji wa bidhaa muhimu zenye kuhitajika ila USD haitakufa itapungua mahitaji yake kwa kiasi kikubwa sana.
 
Hapana mkuu, $ nguvu yake ipo kwenye ucelebrity. Yaani kila unapogeuka ipo. Ilianza kutokushikika baada ya mataifa kukopeshana kwa $. Hii ilisababisha demand ya $ ikapaa mno, maana nchi zina madeni interm of $ na zinahitaji $ kuyalipa. Hapa ndipo mtego ulipo, Sarafu mpya yoyote ikiweza kutegua huu mtego $ inakufa kifo cha mende, ndembe ndembe.
Uchumi haufanyi kazi hivi...

BRICS ni muungano wa nchi Maskini ambazo zinapolitical instability kila baada ya Miaka 5.

Only Euro kwa sasa Ndio inaweza kuitoa Dola kama wakiwa Neutral but that is USA the advantage.

Sharti la kujiunga na BRICS ni zile nchi 5 zikupende tu, sharti la Kujiunga EU mfano
1. Ubadili Sheria zako zinahusiana na Rushwa kwa kuhakikisha Rushwa kweli ni Adui wa haki.
2. Mihimili ya Nchi iwe na nguvu na Uhuru sawa bila kuingiliana
3. Nchi iwe na utawala wa Sheria
4. Uhuru wa soko.

Jana Uganda 😂😂😂 iliingia BRICS kama partner state... Nchi ambaye Kuna zaidi ya 60% Rais atafia madarakani alafu power struggle ianze, no succession plan
Aina nyingine ya Wanachama wa BRICS Ni Venezuela, Beralus.

Hakuna economic opportunities ndani ya BRICS kwa wananchi, i.e there is justifiable reason ya Wahindi kwenda China kama skilled workers and vice versa, Wala kwa Wanachama wengine
 
yuma ya tawala mbalimbali za dunia, kuna nguvu inayotenda kazi kisirisiri. Direction ya dunia inatokana na hii nguvu.

Hapa duniani tupata matokeo tu. Hii nguvu ndiyo yenye mamlaka ya nani aongoza dunia. Au taifa gani lipewe nguvu ya kuongoza dunia. Mambo yote Yanapangwa na hii nguvu.

Mipango yote ya viongozi wa dunia hii kujaribu kupanga mikakati Yao kinyume na hii nguvu inafeli. Mfano ni baadhi ya mataifa kufanya mikakati yao ya kuongoza dunia kinyume na hii nguvu inafeli vibaya. Majuzi tu hapa kwenye mkutano wa BRICS, viongozi wamejaribu kutambulisha SARAFU mpya ya BRICS ili iondowe utawala wa Dollar. Hiyo itafeli. USD Itaendelea kuwa na nguvu.

Tusijisumbuwe, Dollar bado IPO, USA bado IPO sana.

Ufalme wa MAREKANI una mizizi milefu sana kung'olewa ni ngumu sana.
Wewe kaa tulia watu wafanye mambo mazuri, watu hawataki tena Dollar iwe silaha
 
Tanzania ina deni LA zaidi ya billion 40 za Dola ya Marekani...

Marekani na China wanafanya biashara ya thamani kubwa kuliko China na vitaifa vyote vya BRICS..

Tanzania ukiwa na hazina ya sarafu ya BRICS unalipaje deni lako la Dola?
Nashindwa kukuelewa kwakweli! Kwani China anatudai bei gani? Tutalazimika kumlipa China kwa Dola ata mara baada ya currency ya brics kuwa active? Waulize wafanya biashara wanaoenda kununua vitu China watakuambia mwisho wa kuingia na Dollar ni kiasi na mara baada ya hapo utapaswa kufanya nini?

Unafikiri kwanini ao Marekani wanaishutumu China kwa kushusha thaman hela yake?
 
Once again, hakuna mahali nime underestimate, na si kweli kwamba china tu ndio inatumia US$
Unajua ni nchi ngapi zinafanya transaction in USD?
China pekee haitoweza kushusha, kunahitajika multiple countries, and thats when diplamacy na relations ina play part kubwa.
Haitokuwa rahisi kama unavyodhani
Hujanielewa boss.
 
Linganisha na kauli hizi:
1. Titanic haiwezi kuzama kamwe; hata Mungu hawezi kuizamisha.

2. Dola ya Babeli (baadaye wakasema Rumi) haitoweza kuangushwa kamwe.

3. Michael Jackson hawezi kufa.

4. Korona haiwezi kuisha.

5. Makao makuu ya Bongo hayawezi kuhamia Dodoma.
Makao makuu ya Tanzania hayajahamia Dodoma ila yapo Kati ya Dsm na Dodoma ndio maana mawaziri hata Rais muda wote kiguu na njia
.
 
Makao makuu ya Tanzania hayajahamia Dodoma ila yapo Kati ya Dsm na Dodoma ndio maana mawaziri hata Rais muda wote kiguu na njia
.
Itoshe tu kusema ungalimo kwenye hatua mkataa (denial stage). Halafu, umegundua kwamba sikusema chochote kuhusu utekelezaji huo kama umefanyika ama la.

Inawezekana tayari yameshahamia Dodoma au bado. Na kama bado, unadhani haitowezekana kabisa huko mbeleni?
 
Umekula chochote asubuhi hii au umefunga ?
 
Back
Top Bottom