Haiwezekani kufanya ziara za kimkakati? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haiwezekani kufanya ziara za kimkakati?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by siyabonga, Oct 2, 2012.

 1. s

  siyabonga Senior Member

  #1
  Oct 2, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu,wiki iliyopita nilipost thread hapa ya baadhi ya mambo yanayotufanye tuwe dhalili na kuonekana duni mbele ya wageni wanaoishi ndani na nje ya Nchi.

  Kwa bahati mbaya sana thread hiyo haikukaa hata dk 5 hapa JF.

  Nilikuwa na nia njema tu, tuangalie, tujitafakari na kujipanga upya ili tusonge mbele.

  Leo, langu ni dogo tu. Ingekuwa vema iwapo wanaotunza diary za wakubwa na wana nafasi za kushauri waangalie uwezekano wa kufanya ziara za kimkakati Nje ya Nchi na sio ziara za kuhudhuria hafla, parties, birthdays na nyinginezo eti kwa sababu tu umepata mualiko!

  Huku ni kujidhalilisha na kupunguza nguvu uzito wa ofisi tulizopewa dhamana ya kuziongoza.

  Ziara za kimkakati zinakuwa na malengo mahsusi ya kitu unachoenda kufanya na zinalenga kuvuta uwekezaji wa kudumu wa kimaendeleo katika nyanja mbalimbali kama vile elimu, afya, barabara, maji, n.k.

  Ziara za namna hii, zinakwenda kwa mpangilio maalum na mapitio kila baada ya muda fulani. Tuentendee haki Nchi yetu!
   
 2. T

  Triple DDD Senior Member

  #2
  Oct 2, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 151
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  HO NDIO ccm AU MAGAMBA
   
 3. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  Wazo lako ni zuri sana . Hata hivyo, sera zetu za kimkakati ni kutembeza bakuli badala ya kujitegemea kwa raslimali zetu wenyewe!
   
Loading...