Haipiti wiki naota napiga pepa la form 4

Mkuu ni kweli hata mimi hunijia ndoto za namna hiyo hasa paper ya form 6, japo sio kila wiki lakini wiki 2 hazipiti lazima niote
 
Back to koromije!!!!
 
Mkuu kuna nafasi ya uongozi unayo au cheo chochote iwe kazini au kwenye jamii au popote pale? Ndoto yaweza kukujurisha kuwa kuna mambo unapaswa kurudi kujifunza ili kuleta ufanisi ktk nafasi uliyopo.

Kuna pito litakujia mbeleni kama bado haupo ktk jaribu kwa sasa, jinsi unavyofanya huo mtihani ndivyo utakavyopita ktk hilo pito au ndoto inaweza ikawa inaonesha status ya maisha yako kwa sasa, jinsi mtihani unavyouona ndio maisha yako unayoishi.
 
Ila mm naota kwamba nipo chuo na siku ya mtihani imekalibia harafu cjasoma, au hata leo nimeota kwamba nilivyovisoma nimevisahau, yaaan hasa ndoto inakuwa mtu unaota husomi
 
Hii imewahi kunitokea kitambo ila yenyewe nilikuwa naota paper moja ya advanced physics mara nimepiga paper mda umeisha, wakati mwingine naota paper kesho hafu kichwani naona empty. Ila baada ya mda hiyo hali ilipotea kabisa.
Hali hiii kama mm, yaaan mm utakuta naona harafu sijasoma na labda paper siku mbili mbele, kuota kwangu ni elimu ya chuo, mwaka juzi nikaenda kusoma chuo kwakweli nilisumbua darasani, ila leo nimeota tena kwamab nimesoma lakini kichwan sina kitu nikastuka fasta
 
Mkuu hii mambo ni hatari sana maana unashtuka unasindikizwa kwa kusweat.
Ila ukishajua ni ndoto ndio moyo unatulia.
 
Kwa ufupi ni kuwa nyota yako ya maendeleo waswahili wameisha ichukua. na ww utabakia hivyo hivyo. yalinikuta na ndivyo nilivyobakia. mbaya sana aliyenichukulia ni mwana ndoa mwenzangu. nimeshituka mda umekwenda sana. ushauri: watu wako wa karibu kuna mmoja anakuchukia sana na kukusema kwa watu vibaya. anakuchonganisha na watu na kukuzulia sifa mbaya, ila anajifanya kukupenda mnapokuwa pamoja, mtafute ndiye huyo. pili yy ameanza kupaa kifedha si kimaisha.
 
akitokea mtu akakuambia kuna mtu anaitembelea nyota yako mwamini. Namna ya kujinasua ni hii. Nenda bila kujali imani yako kwa wataalamu wa mizimu. ambao ni wakristo kwa dini. waambie watakusaidia. waislamu huwa ni waongo. hutumia majini badala ya mizimu.
 
Mkuu hebu tuambie ulijuaje ni yy yan ulitumia njia gan utakua umetusaidia sana na ss wahanga
 
Kuna uwezekano wakat ulipokua unaanza elim yako uliomba na ulikua na ndoto sana ufike hatua flan au usomee kitu flan, lakin baadae ukaamua kuishia hapo ulipo, Hilo yaweza kuan n deni kwa mungu, km ulimuomba na yy akaahid kukufikisha lkn ww hukufika bas anakukumbusha agano lenu. Km n kweli bas hilo n Agano lako lzm ulitimze na yy amekuahdi lazma ufanikiwe ndo mana unatewa kweny ndoto.
 
Naishia hapa kusoma comments ....sitak kusoma zilizobski
 
Hakika Mungu ni mwema, ndoto hii imenitesa sana, mara kibao nimeota niko o,level, siku nyingine naota naenda kwenye pepar naingia kumbe wengine wanamalizia , wakati mwingine naota nikiwa na rafiki zangu tukiwa katika mazingira ya shule ya o,level, imekuwa ikijirudia sana nawaza bila majibu, la kushangaza katika safari yangu ki masomo sikuwahi kukwama popote wala kupata matatizo makubwa leo nakaribia kumaliza miaka miwili niko kazini . Namshukuru Mungu hata kazini naendelea vizuri kwa mtazamo wangu tu sasa nawaza ndoto hii kwanini inajirudia? Mungu tusaidie wote tunaopata mafumbo kupitia ndoto pasipo tafsiri
 
Ni PM nitakusaidia
 
ndoto hii nimeota sana, na kuna mtu siku aliniita na kuniambia kapata ufunuo ndotoni kwamba kuna watu wameshikilia nyota yangu ya mafanikio.
 
Ndugu umenikumbusha mbali sana ndoto za hivi kuna wakati ziliniandama sana exactly kama ulivyoandika mara nyingi inanikuta nikiwa sijajiandaa haswaa mitihani ya f6.. niliambiwa ni roho mbaya hataki upige hatua ama ni dalili ya kurudi nyuma kimaendeleo ama kunahofu na jambo fulani mbele.. Muhimu jiangalie na utafakari je tayri una kazi yako? una majukumu magumu ya kifamilia? Pia kumbuka kusali sana ndoto za kujirudia mara nyingi huja kama onyo
 
Reactions: SDG
Hayupo duniani kivipi wakati ndiyo anakulipa pesa kushinda hapa jf kumtetea?

Tena mpe Bashite hongera zake lile bao la mkono limezaa matunda tayari shemeji kitumbo kimevimba baada ya wazungu kusokomezea bao lake kwa mkono mpaka mimba ikanasa.
Mimba ishatokaa
 
Wakuu hii issue na mimi nimo lakini mimi nilipasi vizuri sana O-Level lakini nilivyoingia A-Level hamu ya kusoma iliondoka kabisa na nilifanya vibaya mno kwenye A-Level.

Sasa hii ndoto ya kuwa narudia O- Level tu imenitokea sana lakini sikuwahi kuichukulia seriously kabisa , SASA HIVI ndo nimeanza kuona kuna haja ya kufikiri baada ya kukutana na hii thread, na mimi huwa sio mtu ninayeamini mambo ya ndoto kabisa! Lakini nimeota mara nyingi hii ndoto karibu kila mwezi mara moja kwa miaka sasa!

Wenye elimu kweli na haya mambo tusaidiane!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…