Haipiti wiki bila kukwaruzana, nikikaa kimya malalamiko

Haipiti wiki bila kukwaruzana, nikikaa kimya malalamiko

Sigara Kali

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2017
Posts
3,712
Reaction score
8,769
Wakuu salaam
Jamanii mi nna mama mtoto wangu ambaye tunaishi mbalimbali japo sio sana na tupo kwenye uhusiano almost 5 years now

Labda nielezee tabia zetu nikianza kwa upande wangu nna tabia zifuatazo
[emoji117]Sipendi kusikia/kuona mwanamke ananikoromea.
[emoji117]Ni mwepesi kukasirika Lakini ni mwepesi kurudi katika hali ya kawaida
[emoji117]Nina huruma na Nina jishusha pale ninapokumbuka wapi tumetoka na huyo mzazi mwenzangu/Mke wangu( hatujafunga ndoa)

Huyu mwenzangu ana tabia hizi:-
[emoji117]Mbishi sana sometimes hashauriki kwa yale ninayomshauri
[emoji117]Mkimya,ila sometimes ana majibu ya ovyo kwangu
[emoji117]Mgumu kupiga simu kutuma msg,hadi nimuanze Mimi

Sasa katika mawasiliano na kulingana na tabia zetu nlizozieleza hapo juu huwa tunakwaruzana kwaruzana Mara kwa Mara

Sometimes nikikaa kimya bila kumtafuta atapiga simu atatoa lawama nami najikuta nampandishia kwa hiyo tumekuwa watu wa migogoro ya Mara kwa Mara hadi najiuliza je huyu mwanamke hii kazi yake na mshahara wake unampa kiburi hadi awe na jeuri ya kunipandishia/kunijibu ovyo!?anajua nampenda ndo mana ananifanya mtumwa wa kuanza kumpigia simu kila siku!? , nashindwa kuelewa

N.B Nyie wanawake hata kama mna Mali na kuwapa waume zenu vitu mbalimbali ,kama umeshindwa kumpa heshima yake ni sawa sawa na bure,Mwanaume anahitaji KUHESHIMIWA
 
Haa mimi nina miaka 8 na mpenzi wangu. Hata nlkuwa nmeshamtambulisha nyumbaani. Tumekuja shindana kwenye kubishana na kufarakana kila cku. Ukiangalia sababu kubwa ni huyu bint anataka kujfanya kidume na mjuaji sana. Nlchofanya nimechukua kimchepko den yeye naweza kaa hta wiki bila mpigia.
 
wala husibabaike ndojinsi walivyo hata kwetu wapo......hata mgine utakae pata utaona mapya tena vumilia tu nahuyu huyu
 
Uchumba sugu unasababisha matatizo ya kisaikolojia. Ndio maana anakuwa hakuamini amini.
5years??? Duh.....
Kuna mkaka namjua ana mpenzi wake na wameshazaa mtoto mmoja. Huyo mpenzi wake sasa haishi drama,yani ni ugomvi kila siku visa. Na wamekaa mda mrefu sana kwenye mahusiano. Nahisi yule dada ameshachoka anataka ndoa ndomana anafanya visa,sa sijui anaogopa kusema direct.
 
Hapa kila mwanaume mtakatifu lol.Mapenzi kuelewana jamani na kukosea katika mapenzi pia kupo ni kiasi cha kurekebishana tu sababu siku zote hakuna mkamilifu.

Na hiyo heshima ni kwa kila mmoja na sio kwa mwanamke peke yake cha muhimu kujitambua tu na kila mmoja kujua thamani ya mwenzake.
 
Una uhakika huyo mtoto ni wako???
Yaap wa kwangu 100% ,huyu mwanamke nlimeet tu kitaa na vyeti vyake anatafuta kazi nkavuta ghetto nkaanza kuishi nae hadi kapata ujauzito kapiga interview n mwisho kapata kazi nzuri tu na salary akaenda kituoni hapo ndo ubishi ubishi ukaanza
 
Back
Top Bottom