HAI, KILIMANJARO: Mwenyekiti wa Kata ya Muungano pamoja na Mwenezi wajiondoa CHADEMA na kujiunga CCM

Emc2

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
16,808
16,836
20 Julai 2018

upload_2018-7-20_21-15-38.png

CCM YAIBOMOA NGOME YA MBOWE HAI

Viongozi wote wa Chadema Kata ya Muungano, wakiongozwa na Godliving Emmanuel Kimaro ( Baba Diana) Mwenyekiti wa Kata ya Muungano na Ibrahimu Hamis Mkindi (Mparee) Mwenezi wa Chadema Kata Muungano kutoka Wilaya ya Hai wamejivua uanachama wa Chadema na kujiunga na CCM.

Viongozi hao wamepokelewa na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa Kamaradi Humphrey Polepole kwenye Mkutano wa hadhara Moshi Mjini Kata ya Mawenzi wakati akimnadi Mgombea wa Udiwani wa CCM Kata ya Mawenzi Ndg. Apaikunda Ayo Naburi.

Imetolewa na,
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
 
Hahahaha! Pesa za korosho zimeanza kazi kwa speed ya 4G. Kuna siku hao mnaowanunua wataongea ukweli. Endeleni kuwatishia maisha pamoja na kubana biashara zao ili mtuletee kiini macho...Ikifika kwenye sanduku la kura hamjianini mnaiba kura kwa kutumia NEC na policcm +wakurugenzi na mawakala... Hahahah! raha sana magogoni movies ...mnapata tabu sasa.
 
Huo mchezo wa siasa za kutumia dola na kusema mnashinda ndio sasa umesababisha uasi huko Rwanda kwa Kagame. Ngoja muone machafuko yatakayotokea huko na hata Kagame atolewe madarakani kama utaona hilo kundi analosema huwa linamfanya ashinde kwa 90%
Tunawachapa tu hatuangalii nyuso zenu ninyi adui wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom