hahaha Daktari na mtangazaji!

The Dude

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2011
Posts
1,029
Reaction score
464
Juzi kwenye hivi vipindi vya TV
ambavyo wadada wameshika hatamu
kutangaza, na huwa wanawauliza watu
mambo mengi tu nilisikia kali. Mdada
alikuwa kamkaribisha daktari wa
hospitali wa wagonjwa wa akili,
ambaye alielezea kuwa mtu anaweza
akaonekana mzima kabisa , lakini
ukimuuliza maswali fulani rahisi
ukaweza kujua kuwa mtu huyo ana
matatizo ya akili;
MDADA: Daktari unaweza
kutufahamisha ni maswali aina gani?
DAKTARI: Kwa mfano naweza
kumuuliza mgonjwa swali la kihistoria
kwa mfano nikasema,'Dr Livingstone
alifanya safari tatu kwenda Ujiji na
ndipo kifo kikamkuta, sasa je nika katika
safari ya ngapi alipofariki?'
MDADA: (kwanza alicheka kidogo)
Watazamaji hayo ndio aina ya maswali
ya dokta, mi kwakweli sikuwa mzuri
sana kwa historia wakati niko shule,
sina jibu ila nategemea watazamaji
kuna wengi mmekwishapata jibu....sasa
dokta huwa hamna maswali rahisi
yanayohusu jamii tuliyonayo leo?
(....nikahamisha chaneli)
 
hapo hakuna mtangazaji siku hizi mtu akiwa handsome/beautiful tu akiomba utangazaji anapewa taaluma si kigezo
 
Mkuu umenikumbusha mbali..anyway ndio aina ya watangazaji tulionao,wao shule kwao sio inshu..eti wanaangalia kipaji..matokeo yake ndio kama haya..swali rahisi mtangazaji kilaza..
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…