Hafla ya Invest in Africa Yafana Washington DC! Hivi kuna cha kufurahia kweli?

Mdondoaji

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
5,108
1,127
Leo nimeona kituko michuzi nikazijuliza maswali siwezi kuyajibu:-

Mojawapo ya swali ni hili hivi kweli hatuoni aibu mtu binafsi ananunua Boeing mbili wakati serikali yetu inashindwa kununua hata kajitwin otter au fokker friendship?

Sielewi aisee!!!
 
Gamba Jipya

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
401
80
Mkuu kama huwezi kuelewa vitu vidogo kama hivi ni bora ungekuwa unatuma PM ili ujuzwe kinaga ubaga. Kuliko kuanzisha thread zisizo na kichwa wala miguu.
 
Kang

JF-Expert Member
Jun 24, 2008
5,288
1,836
Sio mtu binafsi ni kwa niaba ya kampuni ya Arik Air.
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
73,771
74,419
Leo nimeona kituko michuzi nikazijuliza maswali siwezi kuyajibu:-

Mojawapo ya swali ni hili hivi kweli hatuoni aibu mtu binafsi ananunua Boeing mbili wakati serikali yetu inashindwa kununua hata kajitwin otter au fokker friendship?

Sielewi aisee!!!

Kumbuka, Serikali haishindwi kununuwa hata kumi hizo. Tatizo si kununuwa tatizo ni nani wa kuliendesha hilo shirika, watu wote wizi. Jiulize waliiuwaje ATC kwa nini haijaendelea? mashirika yote ya ummaa yamekufaje? viwanda vya umma vimekufaje? mabenki ya umma yamekufaje? mashamba ya umma yamekufaje.

Tanzania Mungu katupa kila kitu, katunyima akili.
 
Mdondoaji

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
5,108
1,127
Kumbuka, Serikali haishindwi kununuwa hata kumi hizo. Tatizo si kununuwa tatizo ni nani wa kuliendesha hilo shirika, watu wote wizi. Jiulize waliiuwaje ATC kwa nini haijaendelea? mashirika yote ya ummaa yamekufaje? viwanda vya umma vimekufaje? mabenki ya umma yamekufaje? mashamba ya umma yamekufaje.

Tanzania Mungu katupa kila kitu, katunyima akili.

FF,

Kweli hakuna watu wazuri wa kuendesha hilo shirika? Sisadiki. Wanipe mie niwasaidie ila kwa sharti nataka watu wanne tu wengine wote wasimamishwe kazi pamoja na bodi na iundwe bodi mpya na ndani ya bodi wasiwemo wanasiasa wala wabunge. Na shirika lianze mchakato wa kuwa listed company kwenye DSE kwani sitaki kukaa hapo muda mrefu. Ila aibu watu binafsi wanaenda kununua ndege viongozi wetu wapo pale hawasikitiki kwanini shirika la nchi halina ndege hata moja inayofanya kazi. Tuna roho ngumu watanzania.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom