HADITHI

HADITHI

Giday

New Member
Joined
Jan 26, 2017
Posts
3
Reaction score
2
Dilemma
Hodi iliyokuwa inagongwa kwenye mlango wa nyumba yangu ilikuwa ikiniboa.

Nikawa nikishangaa nani anaepiga hodi jumanne hii asubuhi wakati muda kama huu huwa nakua kazini. Nani anaejua kwamba nimepewa likizo nipumzike kidogo?

Nilikuwa nimeshamaliza kuongea na mama. Na alikuwa ameshaondoka kurudi Morogoro hivyo nikawa na uhakika sio yeye anaepiga hodi. Ni nani sasa?

Nikaenda katika dirisha na kuchungulia, nikakuta mwanaume mmoja amesimama huku akiwa amebeba bahasha kubwa mkononi.

Nilijua kabisa kwamba sikutegemea mzigo kutoka kwa mtu yoyote lakini ikabidi niende kufungua mlango.

"Habari za asubuhi mama, wewe ndio Mrs Theresia?"

"Yah ndio mimi".

"Kuna barua yako hapa".

"Sikuwa natarajia ujumbe wowote lakini sawa nipe tu".

"Tafadhali weka saini yako hapa kuonesha umepokea mzigo wako". Akawa akiniambia huku akinikabidhi fomu ya kuweka signature.

Nikatia sign haraka haraka na kumuaga huku nikianza kuifungua ile bahasha palepale huku nikiingia ndani na kufunga mlango.

Ilinichukua muda kidogo kuelewa ambacho nilikiona. Sikuweza kuamini. DM alikuwa ameenda mahakamani ku-file talaka kwa msingi wa "irreconcilable differences" na nilipewa notice ya kuonekana mahakamani. Kwanini alifika hatua hii lakini?

Nilifikiri mambo yatakuwa sawa baada ya kuongea na mama. Mama alichukua hatua za kuonana na DM ingawa hawakuweza kuonana, alikuwa ameshamtaarifu kwa njia ya simu kuhusu miscarriage ya ujauzito...

Sijamsikia tokea aongee na mama na nikashangaa kama hata alikuwa akijali kuhusiana ma miscarriage niliyoipata.

Nilikuwa bado nikisubiri aje au anipigie kwa wiki mbili sasa tokea nitoke hospitali lakini hakuja wala kunipigia simu. Ndio nashangaa kupokea notice ya mahakamani.

Nilipatwa na mshtuko na kwa kweli nilichanganyikiwa. Sababu ipi iliyompelekea kutaka tutalakiane?

Mimi ndio muhanga wa hii ndoa sasa kwanini aoneshe kukata tamaa badala ya mimi ndio nikate tamaa? Nilichanganyikiwa..nikaamua kumpigia simu palepale...nilitaka nisikie mawazo yake...nikashangaa akapokea mara ilipoanza kuita tu...

"Ehee Teddy naona umepata notice" nilijisikia vibaya sana baada ya kuniambia hiyo sentensi ila nikajikaza na kutulia ili nipate ninachokitaka...

"DM, kwanini? Kwanini unataka talaka?"

Sikuwa nimejiandaa na kicheko alichocheka baada ya mimi kumuuliza hivyo, actually ikanibidi nitoe hata simu sikioni kwa muda nimuache amalize kucheka...baada ya muda kidogo nikairudisha tena....

"Teddy uko serious unaniuliza sababu za kutaka tutalakiane? Unatania Teddy si ndio?"

"DM, mimi sitanii, nataka nielewe kwanini unataka tutalakiane ghafla hivi?"

"Ahaa hata mimi naona, okey nitakueleza kwanini Teddy..ni kwamba mimi siwezi kuishi na muuaji.."

Nilishindwa kuyazuia machozi kunitoka ila bado nilikuwa na ujasiri wa kuongea...

"Sijawaua mimi, DM. Najilaumu mimi...ni sababu ya miscarriage.."

"Shut up Teddy, just shut it...unafikiri nitashawashika na upumbavu ulimwambia mama yako? Huna hata aibu? Kweli unamdanganya mama yako kwamba umepatwa na miscarriage wakati umeua watoto wangu..? Nimesikia walikuwa mapacha...umewaua wote..wewe ni muuaji!"

"Sijawaua DM, ni kweli ilikua ni miscarriage, siku ile uliponijibu ile sms yako niliahirisha kutoa mimba...sikuitoa...asubuhi yake ndio nikapata hayo matatizo ya miscarriage.."

Ingawa nilikua nikimueleza hivyo, nilijua fika hataweza kuniamini na moyo wangu uliniuma sana kwa hilo.

"Kwa kuwa unayo sababu, unaweza kukata simu sasa me niandelee na mishe zangu.?"

"Please DM subiri. Nakuomba nipe favour ya kitu kimoja. Nakuhitaji nyumbani mara moja..nakuomba uje..."

"Kwanini nifanye hivyo Teddy, uko high?"

"Please DM, wewe njoo. Nipe hii favour ya mwisho hata kama it's over with you. Nataka tuonane..."

"Okey, nitakuona kesho jioni na nitaondoka jumapili. Nitatumia huo muda kupaki vitu vyangu na jumapili nitaondoka...na nikiondoka hiyo jumapili kuonana ni mahakamani baada ya hiyo miezi mitatu..."

Akakata simu..! Nikaka kwenye sofa huku nikiwa sijielewi...nikataka nimpigie mama lakini nikaona hatanisaidia...

Ilikuwa ni kazi yangu peke yangu kuiokoa ndoa yangu. Haijalishi ni kwa kiasi gani nilikuwa n

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom