Hadithi za Esopo

Zero IQ

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
13,917
24,674
Uzi huu nitakuwa nakuwekea hadithi mbali mbali zinazopatikana katika kitabu cha Hadithi za Esopo hivyo kama ni mpenz wa hadithi itakuwa vyema kama ukiusubscribe mapema ili usipitwe na hadithi ata moja,

IMG_20181002_140915_623.jpeg


KISA CHA MCHEKESHAJI NA MWANAKIJIJI________1

Hapo zamani kulikuwepo mtu mmoja tajiri aliyeheshimika sana na watu wa jamii yake. Bwana huyo alifungua majumba ya maonyesho ya sanaa na watu wote waliruhusiwa kuingia bure. Wake kwa waume, watoto na wakubwa. Ikawa baada ya kazi nyingi za kutwa za kujitafutia riziki, Wananchi wakapata burudani na kufurahi pamoja.


Ila kwa kuwa maonyesho yalifanyika mara kwa mara, na wasanii walikuwa ni wale wale, na burudani ni zilezile zikijirudiarudia, siku zilipopita mambo yalianza kwenda doro kwa idadi ya wahudhuriaji kupungua na msisimko nao kushuka.


Yule tajiri alifikiri namna ya kufanya ili kuwarudisha watu katika uchangamfu kama awali.

Siku moja alitoa tangazo kwa umma akiahidi kutoa zawadi nono sana kwa mtu yeyote atakayeweza kufanya uvumbuzi wa aina mpya kabisa ya burudani jukwaani.

Watu kemkem wenye uzoefu katika tasnia ya kuburudisha umma kwa nyimbo, maigizo, vichekesho nk; walijitokeza kuishindania zawadi ile.


Miongoni mwao alikuwapo Mchekeshaji ambaye alikuwa maarufu sana kutokana na vichekesho vyake mahiri.

Alijitokeza na kusema kuwa yeye ana aina mpya kabisa ya burudani ambayo haijawahi kuonyeshwa jukwaani kabla. Na wala hakuna mtu yeyote atakayeweza kushindana naye. Alijigamba, na walio wengi walimwamini.

Habari ile ilisambaa kama upepo na kuleta hamasa kubwa, ikawa gumzo kila pahali. Na siku ya shindano ilipofika ukumbi ulijaa ukatapika. Waliochelewa kufika walilazimika kusikiliza wakiwa nje.


Kila kitu kiliandaliwa vizuri na muda ulipofika mambo yakajiri kama ilivyopangwa.

Baada ya wengine kutoa burudani zao, kila mtu akishangiliwa na kutuzwa kwa kadiri yake, ikafika zamu ya yule aliyekuwa akisubiriwa kwa hamu.


Mchekeshaji alitokea jukwaani peke yake, bila kifaa cha aina yoyote wala washirika. Shauku kubwa ya matarajio chanya vilipelekea ukumbi kugubikwa na kimya kikuu. Watu wakisubiri kwa hamu kushuhudia kichekesho kipya walichoahidiwa na msanii yule nguli. Akiwa amevalia joho lake refu la rangi ya hudhurungi, ghafla alijipinda na kuinamisha kichwa chake kuelekea tumboni, kisha akatoa sauti kali ya kuiga mlio wa kitoto cha Nguruwe. Mlio huo aliouiga kwa sauti yake ulikuwa wa kupendeza kiasi kwamba hadhira ile ikamshuku kuwa huenda alikuwa ameficha kitoto cha Nguruwe kwenye vazi lake pana. Wakadai akaguliwe ili kuhakikisha, kabla hawajampa sifa na kumtawaza kuwa ni mshindi halali wa zawadi inayoshindaniwa.


Baada ya kufanya hivyo na kukutwa hana kitu chochote alichoficha, ukumbi ulilipuka kwa mayowe ya furaha na kushangilia usanii ule mpya.

Mwanakijiji mmoja miongoni mwa hadhira alipoyashuhudia yale yote, alipata wazo na kusema, “Nisaidieni enyi wakuu, mimi pia naweza, najua hawezi kunishinda katika kuiga sauti kama hii.” Na hapo hapo alitangaza kuwa ataigiza sauti kama vile siku inayofuata, na itakuwa kwa ubora na uhalisia zaidi. Na akawaomba wananchi watulie kwani mshindi wa kweli wa zawadi ile atatambulika baada ya yeye pia kupewa nafasi ya kusikilizwa.


Kesho yake umati mkubwa zaidi ulifurika kwenye jumba la maonyesho, wakiwa na mapenzi na ushabiki kwa Mchekeshaji, na wengi walikuja kwa lengo la kutaka kumdhihaki na kumsuta Mwanakijiji, na sio kushuhudia uwezo wake wa kuiga sauti vizuri kuzidi ile ya msanii aliyepita.

Wasanii wote walitokea jukwaani. Mchekeshaji alikuwa wa kwanza, alijiinamia tumboni na kuiga sauti ya kitoto cha nguruwe, kama siku iliyopita, na hadhira ilimshangilia sana kwa mbinja na vifijo.

Ndipo Mwanakijiji akapewa nafasi, akainama na kujifanya kama ameficha kitoto cha nguruwe kwenye vazi lake (ambapo ni kweli alikificha, ila hakuna aliyemshuku) alishika na kuyanyonga masikio, na mlio mkali wa kitoto cha nguruwe ulisikika.


Watazamaji, hata hivyo, walipaza sauti kwa pamoja wakisema kuwa yule Mchekeshaji aliyepita ndiye mshindi kwani aliiga mlio wa kitoto cha nguruwe kwa ufasaha zaidi. Wakataka Mwanakijiji aburuzwe nje ya jumba lile. Ndipo yule mshamba akakitoa kitoto halisi cha nguruwe kwenye mavazi yake, na kuionyesha hadhira ushahidi chanya kuhusu upotofu wa hukumu waliyotoa.


“Tazameni,” alisema, “hii inadhihirisha wazi ninyi ni aina gani ya mahakimu!”
 
IMG_20181002_140915_623.jpeg


KISA CHA MUUAJI______2

Mtu mmoja alimjeruhi mwenzie na kumuua. Ndugu na jamaa wa marehemu walianza kumkimbiza wakiwa na silaha kwa minajili la kumuua kwa kisasi.


Yule muuaji alikimbia kwa bidii kuu ili aokoe roho yake na hatimaye akafika kwenye kingo ya mto Nile. Ng’ambo ya mto alimwona Simba na kwa woga wake wa kuhofia kuuawa akaamua kukwea juu ya mti.


Kule mtini pia aliona Joka kubwa kwenye matawi ya juu kwenye kilele, akaogopa sana kuuawa kwa sumu. Akaamua kujitupa mtoni ambako nako kulikuwa na Mamba.


Alishikwa akauawa na kuliwa papo hapo.


Hivyo ardhi, anga na maji vyote kwa pamoja vilikataa kumficha Mwuaji yule.
 
IMG_20181002_140915_623.jpeg


HADITHI YA TAI NA MBWEHA________3

Tai na Mbweha walikuwa marafiki wapenzi na hivyo walikubaliana kutoishi mbalimbali. Wakautafuta mti mmoja mzuri. Tai akajenga kiota chake kwenye matawi ya mti huo mkubwa, wakati Mbweha aliweka makazi yake kwenye shimo chini ya mti huo huo. Miezi michache baadaye Mbweha alizaa vitoto vinne.


Muda si mrefu baada ya makubaliano yao ya kuishi jirani kwa urafiki, Tai, kutokana na mahitaji yake ya chakula cha kuwalisha makinda wake, alishuka chini ya mti wakati rafiki yake Mbweha yupo matembezini, akakamata kitoto kimoja cha Mbweha, akakiua na kukila yeye na wanawe.


Mbweha aliporudi, aligundua kilichotokea, akahuzunika sana. Huzuni yake kuu haikuwa tu kwa kifo cha mtoto wake, bali pia ni jinsi ambavyo hakuwa na uwezo wa kulipiza kisasi kwa ukatili aliofanyiwa na rafiki yake, kwani asingeweza kupanda juu kwenye kiota cha Tai.


Hata hivyo muda si mrefu baadaye malipo ya udhalimu yalimfika Tai.

Akirukaruka kwenye mawindo sehemu fulani , ambako wanakijiji walikuwa wakitoa dhabihu ya mbuzi, ghafla akashuka na kudokoa pande la nyama, na kulichukua, pamoja na kizinga cha moto kilichoambatana nayo, bila kujua hadi kwenye kiota chake. Upepo mkali uliopovuma uliwasha moto kwenye kiota, hivyo wale makinda wake, kwa kuwa hawakuwa na mbawa bado, walishindwa kujiokoa wakaungua na kubanikwa kwenye kiota chao wakafa na kudondoka chini ya mti.


Hapo chini, huku mama yao Tai akishuhudia, Mbweha akawala wote kwa kisasi.

Naye Tai alihuzunika sana.
 
IMG_20181002_140915_623.jpeg



HADITHI YA SIMBA, MBWEHA NA WANYAMA WENGINE_________4

Siku moja Simba alitangaza kuwa yu mgonjwa mahtuti na kwamba alikaribia kufa. Hivyo alitoa tamko la kuwaalika Wanyama wote waende nyumbani kwake kumwona na kusikia wosia wake wa mwisho na ushuhuda wa mambo kadha wa kadha, na pia wapate busara za mfalme.


Hivyo Mbuzi alienda kwenye pango alililoishi Mfalme Simba ili kumjulia hali. Alisimama kwenye sehemu ya kuingilia pangoni na kusikiliza kwa muda mrefu. Kisha kondoo alikuja na akaingia pangoni moja kwa moja, na kabla hajatoka Mwanafarasi naye alikuja kupokea wosia wa mwisho wa Mfalme, akaingia pangoni.


Baada ya muda mfupi Simba alijitokeza nje akionekana kupata nafuu ya haraka, akaja kwenye lango lake la kuingilia pangoni ili apunge upepo wa nje. Alipopiga macho kushoto na kulia alimwona Mbweha, akiwa amejiinamia anasubiri nje ya pango kwa muda mrefu.


“Kwa nini ewe Mbweha hujaja ndani ya pango kutoa heshima zako za mwisho kwangu? Na badala yake unakaa tu hapa nje kwa kejeli?” Simba alimuuliza.


“Nisamehe Bwana mkubwa,” Mbweha alijitetea, “ila katika kuja kwangu hapa nimegundua alama za nyayo za wanyama wengi ambao wamekwisha kukutembelea pangoni mwako; na nikichunguza kwa makini zaidi naona alama nyingi za kwato zikiingia ndani, na sioni zitokazo nje. Hadi hapo nitakapowaona wanyama waliokwishaingia pangoni mwako wakitoka nje, sitoingia, naona ni heri nibaki hukuhuku nje kwenye uwazi na hewa safi.”
 
IMG_20181002_140915_623.jpeg



HADITHI YA MTOTO NA MBWA MWITU___________5

Mtoto mmoja, akiwa anarudi peke yake kutoka machungani wakati wa jioni, alipita katikati ya kichaka ambako alikutana na Mbwa mwitu. Kumbe yule Mbwa mwitu alikuwa na njaa na alijua kuwa mtoto kama yule angetosha kabisa kwa chakula cha jioni kwake na kwa familia yake ya watoto wanne kule pangoni. Alianza kumnyemelea akimmezea mate kwa uchu.


Yule mtoto aliogopa sana, mwili mzima ulitetema, ingawa alijitia ujasiri na hakutaka kufa kikondoo. Alifahamu ya kuwa hawezi kupambana naye kwa mabavu akamshinda, wala asingeliweza kushindana naye kwa mbio akamzidi.


Hivyo alipoona kwamba hakuwa na namna ya kujiepusha na hatari ile, alimgeukia Mbwa mwitu na kumwambia kwa unyenyekevu: “Najua, ee rafiki yangu Mbwa mwitu, ya kwamba u na njaa na mimi ni windo lako, na kwa kuwa sina uwezo wowote wa kujiokoa dhidi yako, basi kabla ya kuniua nakuomba unisaidie kitu kimoja tu. Nacho ni uniimbie wimbo mmoja niupendao ili nicheze kwa mara ya mwisho, kisha nikimaliza uniue na kunila.”


Mbwa mwitu aliangua kicheko kusikia ombi la mtoto ambaye kwake alikuwa tayari ni marehemu mtarajiwa. Baadaye alikubali, akachukua filimbi na kuanza kumpigia wimbo.

Wakati mtoto anacheza huku akiwa amejawa na hofu, Mbwa wa nyumbani kwake walisikia sauti ile, wakakimbilia pale kabla ya ule wimbo kwisha na kuanza kumtimua yule Mbwa mwitu.


Mbwa mwitu alimgeukia mtoto akasema, “Hii ni halali yangu; kwani mimi ambaye wasifu wangu ni muuaji na mla nyama, sikupaswa kugeuka mpiga filimbi ili kukidhi matakwa yako wewe.”
 
IMG_20181002_140915_623.jpeg



KISA CHA SIMBA NA PANYA___________6

Siku moja mfalme Simba akiwa amejipumzisha kivulini, alipitiwa na usingizi. Panya mtukutu alimsogelea na kuanza kuchezacheza juu yake; hali ambayo ilimfanya aamke mara moja. Alipoamka, Simba alimkamata Panya kwa kumkandamiza na guu lake kubwa, tayari kwa kumla.


“Naomba unisamehe, ee Mfalme,” Panya alilia na kuomba: “nisamehe kwa sasa na sitosahau kamwe: huwezi kujua pengine ipo siku mimi pia ninaweza kulipa wema wako kwa kukusaidia!.”


Simba aliguswa sana na maneno ya Panya kwamba eti huenda ipo siku akamsaidia yeye Simba, mnyama mkubwa ambaye ni mfalme wa wanyama wote. Aliinua mguu wake na kumwacha aende zake.


Siku moja Simba alinaswa kwenye mtego wa Binadamu, na wawindaji walipomkuta walipanga kumpeleka kwa Mfalme wao kama zawadi akiwa hai vilevile. Walimfunga kwenye mti kwa kamba kisha wakaondoka kwenda kutafuta usafiri wa kumbebea.


Punde ikatokea yule Panya alipita maeneo yale, na alipomwona Simba yupo katika hali ile ya taharuki, majonzi na hofu ya kuuawa, alienda pale mtini na kuzikatakata kwa meno yake makali kamba zile zilizomfunga Mfalme wa wanyama wote.

“Si nilikwambia,? unaona sasa…” alisema Panya.
 
IMG_20181002_140915_623.jpeg




KISA CHA SIMBA NA PANYA________ 7

Siku moja mfalme Simba akiwa amejipumzisha kivulini, alipitiwa na usingizi. Panya mtukutu alimsogelea na kuanza kuchezacheza juu yake; hali ambayo ilimfanya aamke mara moja. Alipoamka, Simba alimkamata Panya kwa kumkandamiza na guu lake kubwa, tayari kwa kumla.


“Naomba unisamehe, ee Mfalme,” Panya alilia na kuomba: “nisamehe kwa sasa na sitosahau kamwe: huwezi kujua pengine ipo siku mimi pia ninaweza kulipa wema wako kwa kukusaidia!.”


Simba aliguswa sana na maneno ya Panya kwamba eti huenda ipo siku akamsaidia yeye Simba, mnyama mkubwa ambaye ni mfalme wa wanyama wote. Aliinua mguu wake na kumwacha aende zake.


Siku moja Simba alinaswa kwenye mtego wa Binadamu, na wawindaji walipomkuta walipanga kumpeleka kwa Mfalme wao kama zawadi akiwa hai vilevile. Walimfunga kwenye mti kwa kamba kisha wakaondoka kwenda kutafuta usafiri wa kumbebea.


Punde ikatokea yule Panya alipita maeneo yale, na alipomwona Simba yupo katika hali ile ya taharuki, majonzi na hofu ya kuuawa, alienda pale mtini na kuzikatakata kwa meno yake makali kamba zile zilizomfunga Mfalme wa wanyama wote.

“Si nilikwambia,? unaona sasa…” alisema Panya.
 
IMG_20181002_140915_623.jpeg



HADITHI YA MBWEHA NA PAKA__________8

Mbweha alikuwa akijigamba mbele ya Paka kuwa yeye ana mbinu nyingi sana za kuwakwepa maadui zake.

“Nina fuko zima la mbinu na ujanja,” alisema, “ambalo lina mamia ya njia za kujiepusha na maadui zangu wakati wa hatari.”


“Mimi ninayo mbinu moja tu,” alisema Paka; “lakini ninaiamini, na inanifaa hiyo hiyo.”


Wakiongea maneno hayo, punde wakasikia sauti za Mbwa wawindaji zikielekea upande wao, na Paka alichupa akauparamia mti haraka na kujificha juu kwenye matawi. “Hii ndiyo mbinu yangu,” alisema Paka. “Je mwenzangu wafanyaje?”


Mbweha akafikiri kwanza kutumia njia hii, mara njia ile, na kabla hajafanya maamuzi, Mbwa walimkaribia na kumkaribia, na mwishowe Mbweha akiwa katika mkanganyiko huo, alikamatwa na kuuawa na Wawindaji.


Paka ambaye alikuwa akishuhudia kinachotokea, alisema;

“Heri njia moja salama kuliko njia mia ambazo huwezi kuzitumia.”
 
IMG_20181002_140915_623.jpeg



HADITHI YA SIMBA NA SUNGURA_________9

Simba mwenye njaa, katika pitapita zake za kuwinda, alimkuta Sungura akiwa amelala fofofo. Alishusha pumzi, akatabasamu na kumshukuru sana Mungu kwa ukarimu wake wa kutambua taabiko lake na kumtunuku chakula pasi na haja ya kukitolea jasho.


Taratibu alimsogelea Sungura ili asije akamwamsha, akalala yeye…

Alipoinua miguu yake kutaka kumkamata, mara akatokea Ayala mnono ambaye alipita akikimbia karibu naye, akielekea upande wa kaskazini kwenye uwanda wa nyasi fupi.


Simba alimwacha Sungura na akakurupuka kumkimbiza yule Ayala.

Vishindo kelele na purukushani za Simba na Ayala vilimgutusha na kumwamsha Sungura ambaye aliamka na kutimua mbio kuelekea upande wa kusini.


Baada ya kumkimbiza Ayala kwa muda mrefu Simba alishindwa na kuamua kurudi ili akamle yule Sungura.

Alipogundua kuwa Sungura naye alikuwa ameamka na kukimbia, Simba alisema kwa kujilaumu, “ama kweli nimepata nilichostahili; kwa kuwa nilikiacha chakula nilichokitia mkononi tayari kwa tamaa ya kutaka kupata zaidi.”
 
IMG_20181002_140915_623.jpeg



KISA CHA SIMBA, MBWA MWITU NA MBWEHA_____________10

Simba, kutokana na uzee wake, alilala akiwa hoi mgonjwa kwenye pango lake.

Wanyama wote wa mwituni walikwenda kumwona na kumsalimu mfalme wao, isipokuwa Mbweha. Kwahiyo Mbwa mwitu, ambaye walikuwa na uhasama wa jadi na Mbweha, aliwaza kuwa huo ulikuwa ni wasaa mzuri sana wa kumkomoa. Akabuni hila ya kutoa mashtaka kwa Mfalme Simba kwamba Mbweha hakuwa na adabu kwake yeye ambaye ni mfalme wao wote na kwamba hakuwa na sababu yoyote ya kutokuja kumjulia hali.


Wakati huohuo Mbweha naye akaingia mle ndani na kuyasikia maneno ya Mbwa mwitu kwa Simba. Simba alimwona na akanguruma kwa ghadhabu dhidi yake. Ndipo Mbweha naye akaona huo ulikuwa ni wasaa wake wa kujitetea na kumgeuzia kibao adui yake, akasema,

“ee bwana Mfalme mkuu, hivi ni nani kati ya wote waliokuja kukuona katika hali yako ya ugonjwa wamekuwa wa msaada mkubwa kwako kama mimi, ambaye nimesafiri nchi na nchi, nikaelekea kila upande, nikitafuta na kujifunza toka kwa matabibu dawa ya kukuponya ewe Mfalme wangu?”


Simba akamwamuru amtajie dawa hiyo aliyoigundua mara moja; kabla hajafikiria adhabu ya kumpa kutokana na kuchelewa kwake kuja kumjulia hali Mfalme.


Mbweha akajibu; “Dawa ya kukuponya ee Mfalme ninaijua, na ni ya uhakika kabisa. Itakulazimu ufanye ifuatavyo; Umchune Mbwa mwitu angali yu hai na kisha ujitande ngozi yake ingali ya vuguvugu. Utapona kabisa maradhi yako, na pia utaishi miaka mingi bila kupatwa kamwe na ugonjwa kama huu.”


Simba, kutokana na mateso aliyoyapata na hali mbaya aliyokuwa nayo wakati ule, alijikuta akipata tumaini ghafla kwa dawa ile ya Mbweha. Japo hakuwa na uhakika nayo, alitaka kuijaribu ili aokoe maisha yake.


Mbwa mwitu alikamatwa mara moja na akachunwa ngozi kikatili akiwa hai; ilhali Mbweha alimgeukia, akamwambia huku akitabasamu, “Ulipaswa kumfariji Mfalme wako kwa maneno mazuri ya faraja na kumtia moyo badala ya maneno ya fitina yenye kuchukiza na kukera.”
 
IMG_20181002_140915_623.jpeg


KISA CHA MWANAFALSAFA, MCHWA NA MEKYURI__________11

Hapo zamani za kale, Mwanafalsafa mmoja alikuwa na kawaida ya kwenda ufukweni mwa bahari kila siku nyakati za jioni, kujipumzisha na kutafakari. Ikatokea alasiri ya jumamosi moja, akiwa ufukweni kama ilivyo ada yake, alishuhudia kwa macho yake mashua ikipigwa na dhoruba kali na kuzama.

Mabaharia na abiria wote waliokuwamo chomboni walizama na kufa maji.


Yule bwana alihuzunika sana, hata alifikia kulaani kwamba majaaliwa ya Mungu hayakuwa ya haki kwani kutokana na mtu mmoja tu ambaye alipaswa kufikwa na mauti siku ile, umati mkubwa uliangamizwa pamoja naye. “Iweje roho za watu wote wale ziangamizwe kwa ajili ya mtu mmoja tu ambaye alipaswa kufa leo?” alijiuliza akiinua mikono yake juu kama ishara ya lawama kwa Mungu.


Wakati akiendelea kutafakari mawazo yake hayo, mara akajikuta amezungukwa na jeshi zima la Mchwa, ambao kumbe alikuwa amesimama kando ya nyumba yao.

Mmojawapo kati ya mchwa waliompanda miguuni alimng’ata na kumsababishia maumivu makali sana.

Yule bwana alighadhibika na kuanza kuwapondaponda kwa miguu na kuwaua mchwa wote waliokuwapo karibu naye.


Mara Mekyuri alitokea, akamcharaza fimbo za maonyo yule Mwanafalsafa huku akisema, “uu nani wewe hata ukatoa hukumu juu ya matendo ya Mungu juu ya wanadamu, ilhali wewe mwenyewe unatenda vivyo hivyo kwa Mchwa?”
 
IMG_20181002_140915_623.jpeg



KISA CHA MBWEHA, JOGOO NA MBWA__________12

Kulitokea usiku mmoja wa mbalamwezi Mbweha alikuwa akizungukazunguka kwa mawindo kwenye shamba la Mkulima mwenye mifugo, ambapo aliliona Jimbi moja limesimama juu kabisa asipoweza kufikia likiwika kwa sauti ya juu.

“Habari njema, habari njema!” Mbweha alipaza sauti kwa hila.

“Nijuze, ni ipi habari hiyo njema?” Jimbi lilijibu.


“Mfalme Simba ametoa tamko la makubaliano ya amani kwa wanyama wa ulimwengu mzima. Kuanzia sasa ni marufuku kwa mnyama yeyote kumdhuru mwingine, bali sote hatuna budi kuishi pamoja kwa amani na urafiki kama ndugu.”

“Shime, hakika hiyo ni habari njema,” lilisema Jimbi; kisha likaendelea “na kule kwa mbali namwona kuna rafiki anakuja, ambaye tunaweza kufurahi naye pamoja, tukianza ukurasa huu mpya wa amani.” Akisema hayo Jimbi aliinyoosha shingo yake akitazama mbali upande ule alio yule mbweha.


“Unamwona nani anakuja?” Mbweha aliuliza kwa hamaki.

“Ni Mbwa wa bwana wangu ndiye anayekuja kuelekea upande wetu… Vipi, mbona unaondoka mapema?” aliuliza, kwani Mbweha alishageuka na kuanza kuondoka mara baada ya kusikia habari ya ujio wa Mbwa.


“Huwezi kusubiri kidogo umpongeze Mbwa kwa kupata utawala wa sheria hii mpya ya amani ya ulimwengu?” alimuuliza huku akitabasamu.

“Ningeliweza kufanya hivyo,” alijibu Mbweha, “ila nahofia huenda Mbwa akawa hajasikia bado tangazo la mfalme Simba.”
 
IMG_20181002_140915_623.jpeg



KISA CHA MWANAMFALME NA PICHA YA SIMBA___________ 13

Hapo zamani kulikuwako Mfalme, ambaye alikuwa na mtoto mmoja tu wa kiume, kijana aliyependa sana mazoezi ya sanaa za mapigano. Kila siku alijichanganya na vijana wa rika lake katika mazoezi na michezo. Na awapo nyumbani alipendwa sana na wazazi wake, hasa baba yake.


Siku moja Mfalme akiwa usingizini aliota ndoto. Na katika ndoto hiyo alipewa onyo la kuwa mwanaye huyo wa pekee atakufa kwa kuuawa na kuliwa na Simba.

Aliposhtuka alipatwa na hofu, kwani katika himaya yake wanyama wakali kama Simba kushambulia binadamu au mifugo ilikuwa kawaida.

Kwa kuhofia huenda ndoto yake ikawa ni ujumbe wa kweli, aliamua kumjengea yule mwanaye, Mwanamfalme, kasri kubwa maridadi.


Jengo lilinakshiwa maridadi na kuta zote zilipambwa kwa picha nzuri za wanyama mbalimbali, zikiwa na ukubwa unaolingana na wa wanyama halisi. Mojawapo kati ya zile picha za ukutani ilikuwa ni picha ya Simba dume.

Hivyo Mwanamfalme aliwekwa ndani ya kasri, akapewa mahitaji yote humo, akafungiwa asitoke nje hata mara moja kwa hofu ya kuuawa na Simba.


Siku moja yule kijana mwana wa mfalme aliiona ile picha ya Simba, ndipo huzuni yake ya kukosa uhuru na kufungiwa ikafufuka upya, na akiwa amesimama kando ya ile picha ya Simba, aliitazama kwa jazba na kusema: “ee mnyama ninayekuchukia kuliko wanyama wote! Kutokana na ndoto ya uwongo aliyoota baba yangu, na kuona maono ya usingizini, nimefungiwa ndani ya kasri hili kama mtoto wa kike, nisitoke kwa kukuhofia wewe: nikutende nini sasa baradhuli mkubwa wee?” Akisema hivyo aliunyoosha mkono wake wa kuume kuelekea mti wa miiba, kwa nia ya kukata tawi atengeneze fimbo ili amsulubu yule Simba kwa kisasi.


Bahati mbaya miba moja ilimchoma kidoleni, akatokwa damu nyingi na kupata maumivu makali sana, kiasi kwamba Mwanamfalme alianguka chini na kuzirai. Ghafla alishikwa na homa kali, ambayo ilimuua siku chache baadaye.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom