Hadithi ya mwanafunzi wa std 6

MANIAJE

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
244
461
Baaasi buana,

Jana ile nimekaa na wadogo zangu katika ku-stay home.

Mdogo wangu mmoja umri wake ni kama miaka sita hivi.

Akaanza kunipigia hadithi moja hivi.

Hadithi hadithi,

Hadithi njoo uongo utamu koleaaaa.

Hapo zamani za kale alikuwepo baba mmoja, mke wake na watoto wake watano.

Huyo baba aliajiri watu wanne ambao kazi yao ni kuihudumia familia, kupika, kufua na hata kuwapeleka watoto shule.

Maisha yao yaliendelea kusonga mbele kila ilipoitwa leo.

Siku moja kuna simba alivamia nyumba ya nne jirani na kwao, akawa anawaua watoto, anakula mbuzi pamoja na mifugo mingine, walinzi walipomuona huyo walitoa taarifa kwa baba na mama, hatimaye baba na mama wakaanza kupambana na huyo simba kuhakikisha haendelei kuleta uharibifu.

Baada ya simba huyo kudhibitiwa vikali sasa alisogea nyumba ya pili kutoka kwao, nako akaanza kufanya uharibifu huo huo.

Sasa walinzi wa ile familia ikabidi watoe taarifa kwa baba na mama kuwa kwa jirani kuna simba kwa jirani na anafanya uharibifu, baba yule alipuuzia na kusema huyo ni simba wa kawaida sana tena ni mdogo hawezi kuja kuleta madhara hapa

Wale walinzi wakazidi kumsisitiza tu, lakini hakuchukua tahadhari yoyote.

Siku moja wazazi wa yule baba waliugua. Hivyo akapanga kwenda kuwasabahi. Akiwa njiani kuelekea kwa wazazi wake, akapata ujumbe kuwa yule simba tayari amefika nyumbani kwake. Napo hakujali akaendelea na safari.

Yule simba akaanza kufanya uharibifu, akaua mbuzi, kondoo n.k. hali ikazidi kuwa mbaya pale nyumbani. Walinzi na wale waajiriwa wote wakaamua kupambana na huyu simba
Ikafikia hatua hadi mtoto mmoja akaliwa na yule simba..

Nikamuuliza baba alisemaje mtoto wake alipoliwa na simba.

Alisema wale watoto wengine waendelee na majukumu tuu, huyo simba ni wa uongo, tena anakulaga majani wala halagi nyama.

Baaaasi buana, nilivyosikitika tuu kwa uzembe wa huyu baba, ikabidi nimtume dukani akaniletee vocha ya jero nije kuunga mb ili niwasimulie hii hadithi, lakini cha kushangaza hadi sasa hajarudi. Sijui atakuwa amekutana na huyu simba,.

Akili za kuambiwa changanya na zako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watoto wangu eeh.....eeh
Mimi baba yenu......eh
Sina nguvu tena.....eh
Za kuua simba.....eh

Simba ni mkali aliua .....
Akaua.....
Sasa tukimbieni( tukimbilie wote chato😀)

Nacheka ila naogopa🙆🏼‍♀️
 
Magufuli
 
Back
Top Bottom