Hadithi ya Kujiongeza

Hadithi ya Kujiongeza

poppah

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2014
Posts
630
Reaction score
548
Mwita na Chuwa walipata kazi katika kiwanda cha kukamua juisi ya miwa pamoja, baada tu ya kuhitimu masomo yao. Wote walifanya kazi kwa bidii sana.

Baada ya miaka mingi kupita, Bosi alimpandisha cheo Mwita na kuwa mkuu wa mauzo lakini Chuwa alibakia pale alipokuwa. Siku moja Chuwa alishindwa kuvumilia na kumpelekea boss malalamiko na kuomba kuacha kazi kwakua boss hathamini mfanyakazi anayefanya kazi kwa bidii bali anathamini mfanyakazi amabaye ana maneno,

Boss alijua kwamba chuwa alifanya kazi kwa bidii siku zote kwa miaka mingi, lakini ili kumsaidia chuwa aone tofauti kati yake yeye na mwita, boss alimwambia chuwa afanye yafuatayo. “nenda ukatafute yeyoteanayeuza miwa sokoni, ujue kilo moja sh ngapi, Chuwa akaenda na akarudi na majibu kwamba, nimewaonam na kilo moja ni sh elfu mbili.

Boss akamwambia, nitamuuliza Mwita swali hilo hilo.
Mwita pia alikwenda na kurudi na majibu: Nimeona mtu mmoja tu anauza miwa, kilo moja shilingi elfu mbili, kilo kumi kwa shilingi 19,000. Kwenye stoo ana akiba ya kilo 300 za miwa. Mezani alikua na miwa 200, kila muwa mmoja una kilo 20, yote ameisafirisha kutoka Morogoro siku mbili zilizopita. Bado ina afya na ina rangi nzuri na ubora unaotakiwa.

Chuwa alivutiwa sana na aligundua tofauti kati yake na Mwita. Aliamua kutokuacha kazi badala yake kujifunza kutoka kwa Mwita.
 
Back
Top Bottom