Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 10,884
- 18,824
Mwandishi: H. Rider Haggard, 1892.
Install app ya Maktaba Sauti kutoka playstore uweze kusoma na kusikiliza vitabu mbalimbali.
UtanguliziMiaka mingi imepita—wakati wa baridi, kabla ya vita vya Wazulu, kulikuwa na mzungu aliyekuwa akisafiri kupitia Natal. Jina lake si muhimu kwa sababu hahusiki na hadithi hii. Alikuwa ameambatana na mikokoteni miwili iliyojaa bidhaa alizokuwa akizipeleka Pretoria. Hali ilikuwa ya baridi na hakukuwa na nyasi za kutosha kuwalisha ng’ombe waliovuta mikokoteni na hilo lilifanya safari kuwa ngumu sana. Alikuwa ameshawishika kufanya safari sababu ya nauli kubwa aliyotoza kwenye ule msimu, mapato ya nauli yalitosha kufidia hasara zozote ambazo angeweza kupata.
Alifanya safari yake na kila kitu kilimuendea vyema hadi alipopita mji mdogo wa Stanger, mahali ambapo zamani palikuwa na Duguza, yaani boma la Chaka. Mfalme wa kwanza wa Wazulu na mjomba wa Cetywayo. Usiku uliofuata baada ya kupita Stanger hali ilibadilika na kuwa ya baridi kali, wingu jeusi liliziba anga na kuzuia mwanga wa nyota.
‘Nisingekuwa Natal ningesema kuwa theluji nyingi itaanguka,’ alijiambia mzungu. ‘Huko Scotland mara nyingi anga kama hili hutokea kabla ya theluji.’ Akakumbuka kuwa hakujakuwa na anguko la theluji nyingi katika Natal kwa miaka mingi. Basi alikunywa mvinyo kidogo na kuvuta tumbaku, kisha akajilaza kwenye hema alilojenga chini ya mkokoteni mkubwa.
Usiku aliamshwa na baridi kali na kilio cha ng’ombe wake ambao alikuwa amewafunga. Alitoa kichwa kwenye hema na kuangalia nje. Nchi ilikuwa nyeupe kwa theluji, na hewa ilijaa theluji ikipeperushwa na upepo huku na kule.
Aliruka huku akiwa amejikunyata kwenye nguo zake, akawaita makafiri waliokuwa wamelala kwenye mikokoteni yake mingine. Waliamka wakitetemeka kwa baridi huku wamejitanda mablanketi toka kichwani hadi miguuni.
‘Harakisheni vijana,’ aliwaita kwa kizulu. ‘Harakisheni, mnataka ng’ombe wafe kwa theluji na upepo? Wafungueni ng’ombe na wapelekeni katikati ya mikokoteni; itawakinga kidogo. Aliwasha taa na kuingia kwenye theluji.
Kazi ilikuwa ngumu lakini mwishowe waliikamilisha. Haikuwa rahisi kwa mikono ya makafiri iliyokufa ganzi kufanya kazi ya kuwafungua ng’ombe. Mikokoteni ilipangwa na kuweka nafasi katikati, kwenye nafasi hii waliwekwa ng’ombe thelathini na sita na kufungwa. Mzungu akarudi kitandani na wale wenyeji wakajipasha kwa mvinyo na kuingia kulala kwenye mkokoteni wa pili na kujifunika turubai.
Kwa kitambo kidogo kulikuwa na utulivu, zilisikika tu kelele za ng’ombe wakigugumia.
‘Theluji ikiendelea hivi itabidi niwafungulie ng’ombe,’ alijisemea mzungu. ‘Hawawezi kuvumilia baridi hii.’
Haukupita muda mkokoteni wake ukatingishika sana; sauti za kamba kukatika na kwato zikasikika. Aliangalia nje tena. Aliona ng’ombe wakikimbilia gizani, wakitafuta mahali pa kujificha na baridi. Ndani ya dakika moja wakawa wametokomea kabisa. Hakukuwa na cha kufanya zaidi ya kusubiri hadi asubuhi.
Kukakucha, ardhi yote ilijaa theluji. Hakukuwa na dalili zozote za kuonyesha walikokwenda, alama zote za kwato zilikuwa zimefukiwa na theluji iliyoanguka. Mzungu akaita baraza la watumishi wake makafiri. ‘Tufanye nini?’ aliuliza.
Mmoja alisema hili na mwingine akasema kile, lakini wote walikubaliana kuwa wanatakiwa kusubiri mpaka theluji iyeyuke.
‘Au mpaka tugande tufe, nyie wapumbavu!’ alifoka mzungu, alikuwa na hasira maana alikuwa amepoteza ng’ombe wa thamani ya paundi mia nne.
Basi mzulu mmoja aliyekuwa amekaa kimya kwa muda mrefu akaongea. Alikuwa ni dereva wa moja ya mikokoteni. ‘Baabaangu,’ alimwambia mzungu. ‘Ni hivi, hakuna anayejua walikokwenda au kama wapo hai au wamekufa, lakini kwenye lile boma.’ Akaelekezea kwenye nyumba Fulani zilizokuwa juu ya kilima kama umbali wa maili mbili, ‘Anaishi mganga aitwaye Zweete. Ni mzee—mzee sana lakini ana maarifa, kama kuna mtu anayeweza kukuambia ng’ombe wako walipo basin i yeye.
‘Hekaya tu!’ alijibu mzungu. ‘Lakini kwa sababu bomani kutakuwa na joto kuliko hapa tutaenda kumuona Zweete. Bebeni chupa ya pombe naugoro kiasi kama zawadi. Baada ya saa moja akawa amefika ndani ya nyumba ya Zweete. Mbele yake alisimama mzee mmoja mzee sana, alibaki kama furushi la mifupa tu. Alikuwa haoni macho na mkono mmoja, mkono wake wa kushoto ulikuwa mweupe na uliojipinda.
‘Unahitaji nini kutoka kwa Zweete mzungu?’ aliuliza mzee kwa sauti nyembamba. ‘Hauniamini wala haiamini hekima yangu; sasa kwa nini nikusaidie? Lakini nitakusaidia japokuwa ni kinyume na sheria zenu na unatenda kosa kutaka msaada wangu. Nafanya hivyo ili kukuonyesha kuwa uganga wa kizulu ni wa kweli, nitakusaidia. Ninajua unachotafuta babaangu. Unataka kujua walipo ng’ombe wako baada ya kukimbia kwenda kutafuta mahali pa kujikinga na baridi, sivyo?’
‘Ndivyo mganga,’ alijibu Mzungu. ‘Una masikio marefu.
‘Ndiyo babaangu, nina masikio marefu japo wanasema kuwa nimekuwa kiziwi. Nina macho makali pia, japo siwezi kuona sura yako. Ngoja nisikilize, ngoja niangalie!’
Kwa kitambo kidogo alikuwa kimya, akiyumbisha mwili mbele na nyuma, kisha akasema: ‘Una shamba babaangu, huko karibu na mji wa Pine, sivyo? Na kama umbali wa saa moja hivi kutoka kwenye shamba lako anaishi kaburu mwenye vidole vine tu kwenye mkono wake wa kulia. Kwenye shamba la kaburu kuna korongo ambalo miti ya kifauongo imeota. Ng’ombe wako utawapata kwenye korongo hilo, ndiyo, safari ya siku tano kutoka hapa. Watume watu leo nao utawapata wote kasoro watatu waliokufa kwenye theluji. Sihitaji malipo yoyote! Sifanyi maajabu ili nilipwe. Kwa nini nifanye hivyo na mimi ni tajiri?’
Mzungu alibeza, lakini alituma watu. Siku ya kumi na moja aliowatuma walirudi wakiwa na ng’ombe wote kasoro watatu. Katika zile siku kumi na moja alizokaa kwenye boma la Zweete waliongea hadi usiku mwingi.
Katika siku ya tatu alimuuliza Zweete ilikuwaje mkono wake wa kushoto ni mweupe na umesinyaa, na Nada na Umslopogazi aliowataja mara kadhaa ni nani? Basi mzee yule akamsimulia kisa kinachosimuliwa kwenye kitabu hiki. Alimsimulia kila siku hadi kikaisha. Kisa chote hakijaandikwa hapa sababu mengine yanaweza kuwa yalisahaulika au yalionekana kuwa hayana umuhimu. Pia haijawezekana kwa mwandishi kupata maneno mazuri ya kuelezea kisa kama ambavyo msimuliaji angetaka. Maana kiukweli alikuwa kama anaigiza kuliko kusimulia hadithi. Aliposimulia kifo cha shujaa alionyesha ishara za kuchoma kwa fimbo yake. Hadithi ilipokuwa ya huzuni alionyesha majonzi na hata kulia. Na zaidi ni kuwa alikuwa na sauti nyingi, kila mhusika wa kwenye hadithi alikuwa na sauti yake. Mzee huyu alionekana kuishi tena katika nyakati za kale.
Mzungu yule alijitahidi kadri awezavyo kuiweka hadithi ya Zweete kama alivyosimuliwa. Na kwa sababu hadithi ya Nada—yungi yungi na wahusika wote ilimgusa sana ameamua kufanya hata zaidi, ameichapisha ili watu wengine waweze kuisoma.
Basi baada ya kusema hayo tumuache Zweete, ambaye alikuwa na jina jingine pia, aendelee na hadithi.
Install app ya Maktaba Sauti kutoka playstore uweze kusoma na kusikiliza vitabu mbalimbali.
Utangulizi