ULIMWENGU WA SIRI: Sehemu ya Pili
0652 212391
MR ROBIN Thomas alikuwa ni mwalimu wa sosholojia katika chuo kikuu cha Birmingham. Kila siku asubuhi ilimpasa kusafiri kutoka Milton Keynes hadi Birmingham, na jioni kurejea.
Umbali kutoka jiji la Birmingham hadi Milton Keynes ni maili 71. Kwa gari inakadiriwa kuchukua saa moja na dakika kumi na moja kutoka jiji la Birmingham hadi mji wa Milton Keynes.
Mr Robin Thomas alikuwa anaishi na mke wake na watoto wao wawili mapacha. Mke wa mwalimu Robin alikuwa anaitwa Glory Deen. Wazazi wa Glory walikuwa wamelowea kwa muda mrefu katika mji wa Milton Keynes, wakitokea katika nchi jirani ya Scotland.
Ilikuwa ni kawaida kwa Mr Robin kuamka saa kumi alfajiri. Na kuanza kujiandaa ili aelekee kazini kwake, Birmingham.
Alam aliyoitega Mr Robin ili imuamshe ilikuwa inaita kwa mara ya tatu sasa. Mara mbili za mwanzo bi Glory hakutaka kumuasha mumewe. Alijua atasikia na kuamka mwenyewe kama ilivyo ada yake. Lakini mwito huu wa tatu ulimfanya bi Glory kuamka na kufanya jitihada za kumuamsha muwewe. Lakini jitihada zake hazikuzaa matunda. Mr Robin Thomas hakuwa katika ulimwengu huu!
Bi Glory alimuamsha mumewe kwa takriban dakika tatu. Huku sasa sauti yake ikiingiwa na hofu juu ya kilichompata mumewe. Ilipotimu dakika ya nne ndipo alipogundua kwamba mwili wa mumewe ulikuwa wa baridi sana, tofauti kabisa na mwili wa kawaida. Fikra za kwamba mumewe amefariki zilianza kumea katika ubungo wake. Na hofu kuu ilishamiri moyoni mwake. Mumewe amefariki? Katu haikumuingia akilini mwake. Lakini kila alipomgusa mumewe, basi hisia kwamba mumewe amefariki zilipata nguvu kichwani mwake. Alijiona dhahiri alikuwa anaiamsha maiti!
Hapo ndipo yowe lilimtoka, huku akilia kwa nguvu na kuomboleza juu ya kifo cha mumewe.
Wanawe mapacha, Lilian na Irene, ambao walikuwa na umri wa miaka kumi na tisa walitoka mbio chumbani kwao na kukimbilia katika chumba cha wazazi wao. Walianza kugonga mlango ili waweze kufunguliwa mlango na kujua kulikoni?
Wakati huo Irene alipiga hatua moja mbele. Hisia zake zilimwambia kwamba kuna hatari, nao kama watoto wa kike alihisi pengine haitokuwa rahisi kukabiliana na kitu watakachoenda kukutana nao. Alimpigia simu binamu yake, Raul.
Bi Glory alilia sana kule chumbani. Kilio chake kilificha sauti za kina Lilian waliokuwa wanalia kule nje. Ndani ya nusu saa nyumba ilitawaliwa na vilio. Mama akilia ndani, watoto wakilia nje.
"Irene kuna nini? Mbona nyumba mzima mnalia?" Raul aliuliza akiwa nyundo mkononi.
"Mbona na nyundo Raul? Ya nini hiyo?" Irene aliuliza.
"Nimevunja milango yote kufika hapa. Nimegonga sana nikiwa nje, lakini hakukuwa na majibu. Imenipasa nitumie njia hii ili kufika hapa" Raul alisema.
Irene na Lilian walibaki na mshangao. Hakuna aliyesikia sauti ya Raul akivyowaita, wala sauti ya nyundo. Walijisukia wao wakilia, na ndani walimsikia mama yao akilia.
"Tusamehe kaka Raul, hatukukusikia gata kidogo waka.." Lilian alikuwa anaelezea jinsi alivyoingia ndani, lakini Raul alimkatisha.
"Kuna tatizo gani?" Raul aliuliza.
"Mama!" Lilian na Irene walijikuta wakisema kwa pamoja huku wakiuonesha ule mlango wa chumba cha wazazi wao.
Ndipo hapo Raul alipotuliza akili, na kumsikia bi Glory akilia kwa kwikwi mle ndani.
"Amekuwa akilia kwa muda gani?" Raul aliuliza..
"Ni zaidi ya saa sasa" Irene alijibu..
"Tuuvunje mlango!" Raul alisema. Na alisema kweli maana hakutaka ushauri. Alitumia nyundo yake kuuvunja ule mlango.
Raul alifanya kama alivyofanya katika milango mingine ndani ya nyumba ile.
Sent using
Jamii Forums mobile app