Hadithi: KIVULI NA JUA!

Hadithi: KIVULI NA JUA!

Dogoli kinyamkela

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2024
Posts
2,144
Reaction score
3,459
Hadithi: KIVULI NA JUA!

Kulikuwa na kijana mmoja aliyeitwa AMANI, aliyekuwa na ndoto ya kuwa mtu maarufu sana kijijini.
Kila alipofanya jambo dogo, alitaka watu wamsifie.

Siku moja, akiwa anatembea barabarani, akaona KIVULI CHAKE chini ya JUA.
Kivuli kilikuwa KIREFU SANA, kikionekana kama MTU MKUBWA SANA.

Amani akasema kwa fahari:
“Tazama, hata kivuli changu ni kikubwa kama mfalme! MIMI ni mtu wa maana sana.”

Lakini jioni ilipofika, Jua lilipozama, kivuli kikapotea kabisa,
Amani akabaki peke yake gizani, akijiuliza:
“Liko wapi lile likivuli langu kubwa?”

Mzee mmoja aliyekuwa karibu akamwambia kwa upole, “Mwanangu, kivuli chako kilionekana kikubwa kwa sababu ya mwanga wa jua — si kwa sababu wewe ni mkubwa"

Hiyo ndiyo EGO ambayo watu wengi tunayo na inatusumbua sisi wenyewe na watu wengine waliotuzunguka.
Tusipoishinda inatuumiza na kuumiza kila mtu aliye karibu nasi.

EGO ni kama kivuli, hukufanya uonekane zaidi, lakini unakuwa siyo wewe halisi.

Amani alijifunza kitu baada ya kumsikiliza mzee mwenye busara na kuanzia siku hiyo, alianza kujifunza kuwa ukubwa wa kweli haupatikani kwa sifa au majivuno, bali kwa unyenyekevu, hekima, na moyo wa kujifunza.

Hadithi hii inatufundisha kwamba;

EGO kwenye maisha ni Kivuli tu, huonesha picha kubwa ya “mimi” lakini si halisi.
IMG-20251107-WA0374.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom