gemplatnumz
Senior Member
- Jan 24, 2017
- 133
- 371
tory za kusisimua.
Simulizi: 'MKUFU WA MALIKIA WA KIJINI'
Mtunzi: Meteck Derthod
SEHEMU YA--- 01
Shukurani kwa:-
1> Mungu aliyeniumba na kunifanya niendelee
kuishi mpaka muda huu.
2>Wote wanaotoa sapoti hata kama kunakikwazo
gani, wamekuwa waaminifu hata leo nimekuwa
na moyo wa kutunga simulizi hii.
Utangulizi:
>Duniani leo hii wanadamu tumekuwa
tunakumbana na changamoto mbali mbali katika
maisha ambazo ufumbuzi wake umekuwa ni
vigumu kuupata hivyo katika riwaya/simulizi hii
tutajua ni jinsi gani ya kufanya ili kuepukana na
changamoto hasi katika maisha yetu ya kila siku.
Kila mtu ni lazima atakutana na changamoto
katika maisha yake, na hata kama ulishawahi
basi zipo changamoto zaidi zitakazo kuja kwako.
Katika Simulizi hii tunamuona kijana mmoja
anayeitwa 'PAULO' aliyekuwa akipata shida mbali
mbali na kumfanya aingie kwenye mtego wa
majini/mapepo hivyo aliweza kuhangaika bila ya
ufumbuzi wowote ule hadi alikata tamaa lakini
baadaye alipata sululisho la changamoto zake
kwa msaada wa mtu aliyekuwa akimchukia na
Kumdarau, Je, ni kivipi aliweza kuitatua
changamoto yake? Na imekuwaje hadi asaidiwe
na aliyekuwa kama adui yake, Fuatilia mkasa huu
mwanzo mwisho ..!
(NI KISA CHA KUBUNI)
****MWANZO****
Giza lilitawala eneo lote, ilikuwa ni sehemu
iliyotisha sana, kwa binadamu wa kawaida
isingekuwa rahisi kuishi huko, kikao baina ya
majini watano kiliendelea kuhusu ndoa kati ya jini
la kiume na majini mawili ya kike yaliyokuwa
yakimtaka jini huyo wa kiume ili ndoa ifungwe
kati yao:-
"Ndoa haiwezi kufungwa kama mpo wawili, ni
lazima mmoja ajitolee kumuachia mwenzake ili
afunge ndoa na mwanangu!" Alizungumza malikia
wa majini huku anawaangalia mabinti wa kijini
waliokuwa mapacha maana wote walitaka
waolewe na jini mmoja.
"Hapana malkia, kwani kunatatizo kama mwanao
akituchukua sote wawili? Sioni shida Mimi, hebu
angalia jinsi ambavyo majini ya kiume yalivyo
machache, kwani unafikiri mmojawapo kati yetu
akiacha kuolewa na mwanao atapata wapi wa
kumuoa, muda wetu wa kuolewa tayari umefika
malikia!" Laylatush aliongea kwa msisitizo sana
na kumfanya huyo malkia afikiri kwa muda.
"Ingewezekana kama mwanangu
asingetegemewa kuwa mfalme, maana kama
akiwa mfalme ninyi wote hamuwezi kuwa
mamalikia, kwani wapi ulishawahi kusikia wapi
kuna mamalkia wawili?" Aliuliza malkia na kifanya
mabinti hao wanyong'onyee kwa muda.
"Au mwanangu Niju unasemaje kuhusihana na
hili? (huku anamuangalia)" malkia alisema
"Mama mimi sina usemi nakusikiliza wewe" Niju
aliishia hapo.
Malkia alifikiri tena kwa muda kisha
akawaangalia wale mabinti wa kijini akasema,
"Laylatush na laulati basi ngoja niwape zoezi
atakayeshinda ndiye atakaye olewa na
Mwanangu Niju, sawa?" Aliongea na kuwafanya
mabinti waangaliane kwa mshangao kwa muda
"Sawa, kwani ni zoezi lipi hilo?" Alijibu laulati
"Angalieni huu mkufu!" Muda huo huo akawa
anauvua kutoka shingoni mwake, akaendelea
kusema,
"Nitautupa duniani kwa wanadamu, atakaye
fanikiwa kuurudisha huyo ndiye malikia mtarajiwa,
ila kumbuka nguvu zenu za kijini hazitoweza
kuwaonesha huu mkufu atakapokuwa, sawa?"
"Sawa, tumekuelewa" walijibu kwa pamoja
Baada ya kufikia makibaliano hayo, malkia
alisimama na kuwafanya wote wasimame pia,
kama ilivyo desturi yao. Malikia akawapa
maelekezo kadhaa watakapo kuja duniani kisha
akaushika mkufu kwa staili ya kuuning'iniza,
akawa anatamka maneno yasiyo eleweka, mkufu
ukatoweka kimaajabu mkononi mwake na
kumfanya kila mmoja aelewe tayari ulishatupiwa
duniani..!
------------
*******
------------
Ilikuwa alfajiri ya saa 12, nilikuwa nimepumzika
kutokana na uchovu niliokuwa nao hivyo nilijikuta
nimelala sana siku hiyo! Mara, nikasikia mlango
wangu unagongwa kwa nguvu sana hadi nikaanza
kutetemeka,
"Nani wewe mbona unagonga mlango kwa nguvu
hivyo?" Niliuliza baada ya kuona mgongaji haachi
kugonga ukizingatia alikuwa akigonga kwa fujo!
"Hivi wewe Paulo, unaakili timamu kweli? Hebu
fungua kabla sijakufanyia kitu kibaya" ilisikika
sauti nje ya mlango uliokua ukigongwa kwa fujo
nikawa nimeshamjua mgongaji kutokana na
kuifahamu sauti yake vizuri.
"Lakini mama huwa hatuendi hivyo, uwe unakuwa
mstaarabu hata kama hiki chumba ni chako
mama angu!" Nilimjibu huku nausogelea mlango
niufungue hadi nilipofanikisha,
"Enhee Leo nimekukuta, kodi yangu iko wapi? La
sivyo natupa vitu vyako nje, umenielewa ee?"
Yule mama mwenye nyumba alizungimza kwa
jazba sana wala hakukumbuka hata salamu huku
moyoni mwangu nilikuwa na hofu sana nisije
kufukuzwa
"Samahani mama, ila nitajitahidi hizi siku mbili
tatu nikuletee pesa yako!" Niliongea namwangalia
machoni labda angeweza kujua uhitaji wangu
"Khee hivi we mtoto, nimekufanyia buku tatu kwa
mwezi kodi ya hiki chumba halafu bado
unashindwa? Kwani unafikiri utapata wapi
chumba kwa bei hiyo Dodoma hii? Hebu acha
porojo zako hapa, kama huna pesa acha
nikufukuze, maana nimekuvumilia miezi sita yote
hujanipa pesa yangu" aliongea na kunifanya
nijikune kichwa ambacho kilikuwa hakiniwashi ila
ni mbwembwe tu, nafikiria jinsi ya kuipata hela
nimlipe mama wa watu baada ya kupata jibu
nikamwambia,
"Basi, usijari Leo jioni nikirudi kutoka mihangaiko
nitakuletea pesa yako"
"Unajua mi nakusikiliza tu, usipo niletea utajuta
kunifahamu" alinijibu muda huo huo akawa
anaondoka na kufanya nimsindikize kwa macho
hadi alipoingia kwenye nyumba yake.
"Dah maisha haya yamekuwa magumu balaa, sijui
nitapata wapi hela yote hiyo, yaani kaupaisha
usingizi wangu wote yaani daah" nilijisemea kwa
malalamiko huku nachukua ndoo angalau
nikaoge, nilienda kuoga hadi nikamaliza nikawa
narudi chumbani kwangu ila nikawa nasikia simu
inaita kutoka chumbani kwangu hivyo nikajua
moja kwa moja ilikuwa ni simu yangu na
kunifanya niongeze spidi hadi nikafika
nikaichukua na kuipokea,
"Haloo, nani mwenzangu?" Niliuliza
"Hivi Paulo kila siku utakuwa ukiniuliza nani tu,
kwani hujasevu namba yangu?" Sauti upande wa
pili ilisikika na kufanya nimjue muongeaji
"Samahani bro Hamudu, lakini si unajua simu
yangu yenyewe ni kimeo, nilisha kuambia inawino
unaozuia majina yasionekane"
"Nunua simu nyingine hiyo hata demu huwezi
kumpata, sasa we boya hebu sikia kuna ishu
hapa vipi utakuwa na muda" aliongea na kuniita
boya, kwa kweli hii tabia sikuipenda ila kwakuwa
nilikuwa ninashida na pesa nikawa mpole tu,
"Muda upo, ishu gani hiyo jamani?"
"Usiongee kwa jazba bhana, sasa njoo hapa
taveta Kikuyu magengeni utanikuta" aliishia hapo
na kukata simu, sikuwa na chaguo tena nikawa
navaa haraka haraka nilipomaliza nikachukua
mkokoteni wangu maana nilijua ni lazima itakuwa
ishu ya kubeba mzigo nikawa natoka nianze
safari,
"Hahaha! Sasa mbona suruali yako imechanika
hivyo Paulo" nilisikia sauti nyuma yangu lakini
sikutaka niijali maana nilijua watakua wambea tu,
kila mtu na maisha yake, hivyo baada ya
mwendo wa dakika kadhaa nilifika sehemu
husika na kumkuta Hamudu ananisubiria, baada
ya kuniona mara moja tukaanza safari kuelekea
chinyoya maana alidai kuna mtu anataka kuhama
kwa hiyo anatafuta mtu ambebee mizigo hivyo
tulienda moja kwa moja hadi sehemu husika
ambapo tulikuta tayari vyombo vyote
vilishatolewa nje tuliokuwa tukisubiriwa ni sisi tu!
"Sasa wewe bhana, ongea na huyu Dada mambo
ya bei Mimi ngoja niwaache" Hamudu aliongea
anamshika mdada aliyekuwa pembeni yangu na
Mara moja akapewa elfu Kumi na yule dada
kama malipo ya udalali akawa anaondoka,
nikajikuta nikishikwa na tamaa ya pesa maana ile
elfu Kumi ilinikata stimu kabisa.
"Nataka nihamie nkuhungu chama, utanifanyia
shilingi ngapi?" Aliongea yule mdada
"Mmmmh...mbona mbali hivyo, hivi unapajua
nkuhungu chama wewe"
"Napajua, nifanyie tu kaka angu maana sina
jinsi" aliongea nikawa nafikiria jinsi palivyo mbali
ila sababu nilikuwa ninashida na pesa niliamua
nilikubari tu,
"Basi sawa, lete elfu ishirini na tano"
"Jamani we kaka, nifanyie ishirini basi maana
hela siku hizi ngumu sana"
Nilikubari na haraka haraka tukawa tunapakia
mizigo hadi tulipo maliza nikaanza safari huku
yeye akidai kuwa anikute katika kituo cha
daladala cha chama ili tuende kwenye hiyo
nyumba anapohamia hivyo ilinichukua masaa
matatu hadi nikafika sehemu husika ila badala
yake Mimi ndo nilimkuta yeye tofauti na mpango
wetu, alionekana kakasirika sana kiasi kwamba
nilipomfikia alinifokea akawa anasema,
"Hivi wewe unaakili kweli? Mbona mirembe
hospitali ya vichaa ipo karibu tu hapa hapa dom?
si nakuuliza wewe?" Aliongea, kwakweli
alinishangaza sana maana sikujua hata kosa
langu
"Kwani tatizo nini, mbona umekasirika hivyo"
nilimuuliza
"Heeee....haloooohooo! Ina maana hujui eee?
Makubaliano yetu ni kwamba Mimi ndio nikikute
wewe na wala sio wewe unikute Mimi"
Nilijikuta namshangaa tu maana hata
sikumuelewa vizuri,
"Kwani wewe hujui kwa mkokoteni kutoka kule
kufika huku ni mbali sana ukizingatia mkokoteni
ni mzito mpaka utumie nguvu?"
"Mmmh...haya, hebu njoo hapa, weka hii mizigo
chini maana nyumba yenyewe ndio hii" aliongea
na kunionesha nyumba yenyewe na haraka
haraka nilishusha mizigo yote ila akaomba tena
nimsaidie kuiingiza ndani, nilikubari nikamsaidia
hadi nikawa nimenaliza kabisa,
"Haya asante bhana, nashukuru sana, vipi
unanidai shilingi ngapi?" Aliongea yule mdada
"Tulikubaliana shilingi elfu ishirini!"
"Mmmh...unajua sasa hivi pesa ngumu sana kaka
angu, hebu chukua hii jero nenda kanywe hata
chai, maana mi ninayo hii tu"
Mwanzoni nilihisi anatania lakini nilimshagaa
sana jinsi yule Dada ambavyo hana huruma,
"Hivi Mara ya mwisho kwenda kuipima akili yako
ilikuwa lini? Yaani nitoke na mzigo toka chinyoya
hadi huku halafu nikuingizie mizigo ndani, unipe
jero kweli, hivi una huruma wewe?"
"Heeeee bhanaa, acha porojo zako hapa, kama
hutaki hii jero, uchukue mzigo kaurudishe
chinyoya ulipoukuta nitauleta Mimi mwenyewe
sio lazima kubishana kitu chenye suluhu"
"Duuh, yaani niurudishe nianze tena moja mbili,
kwani nimekuwa roboti Mimi hadi uniendeshe
hivyo, au huwa unaninunulia chakula wewe?"
"Nasemaje, ingia ndani chukua mzigo, kairudishe
ulipoukuta tumalizane"
"Sasa wewe naona unaanza kunipanda kichwani,
ngoja nikuoneshe kuwa mimi ni nani!" Niliongea
nimekasirika balaa nikawa namfata yule Dada
kwa hasira ila cha ajabu akaanza kupiga kelele
akadai nimuache kitu kilichofanya watu waanze
kusogea karibu tulipokuwa wakawa wanauliza juu
ya ugomvi uliokuwepo kuwa ulisababishwa na
nini,
"Yaani huyu kaka ni katili sana yaani kanibebea
mizigo na mkokoteni wake halafu nikimpa hela
anakataa eti anasema anataka kunitumia halafu
nikimuambia kuwa nnamume wangu anaanza
kunilazimisha, Mimi simtaki hebu nisaidieni
jamani" aliweza kuongea uwongo ulioniweka
katika wakati mgumu maana nilitaka kujitetea
wale wananchi wenye hasira Kali walianza
kuniandama na kunipiga kama mwizi ila cha
ajabu yule Dada nilipomuangalia alikuwa
akinicheka halafu akaanza kuniitia mwizi ambapo
watu wengi walifika hadi wengine walifika
wameshikilia viberiti na matairi na mafuta ya taa
wanichome moto, hakika siku hiyo nilijuta sana
wala sijikuhisahau jinsi watu walivyo wakatili,
wakawa wananipiga mawe huku wengine wao
wakisema,
"Piga huyoooo.....mwizi mkubwa na achomwe
moto kabisa!!!" ITAENDELEA