Hadithi: Jini Kuruthumu

the numb 1

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2020
Posts
1,573
Reaction score
2,940
STORY: JINI KURUTHUMU

EPISODE 1

Ni jumapili angavu ndani ya mji wa Moshi, mji uliosheni kila aina ya pilikapilika na purukushani. Jua lilikuwa likielekea magharibi na kulipisha giza lichukue nafasi yake. Jioni hiyo, Sudy Chinga kama wengi walivyopenda kuniita kutokana na kazi umachinga nilikuwa narudi masikani kwangu MLANDEGE.

Nikiwa natembea kutokea barabara ya Manyema kuelekea Mlandege, mbele yangu alitangulia msichana mrembo kupindukia. Alikuwa mrembo na mwenye mvuto wa aina yake. Binti huyu licha ya kujaaliwa kchwa kizuri chenye nywele ndefu na laini, alikuwa na uso mpana wa mviringo ulionashkiwa na macho makubwa yenye kurembua muda wote. Midomo yake mizuri, laini ambayo akikupiga busu, katu hutatamani abanduke mdomoni.

Kimwana huyu mwenye uzuri wa kuvunja mizani, alijaliwa kifua kipana kilichobeba maziwa madogo yaliyosimama wima kiasi cha kuwatoa udenda wanaume wakware pindi wamtizamapo. Alikuwa na umbo nzuri, umbo ambalo ni wasichana wachache sana waliopewa upendeleo na maanani kwa kuwa nalo.

Sudy Chinga sikuwa mtu wa wanawake kama walivyo vijana wengine ambao pindi wamuonapo tausi mzuri hawawezi kumuacha apite bure. Hata hivyo nilikuwa nimeoa na Mungu ameijalia ndoa yangu nikapata watoto wawili na mke wangu kwa jina Agness. Tuliheshimiana sana na mke wangu, na hivyo sikupenda kumsaliti mtu anayenipenda na ambaye amejitoa kuishi na mimi katika hali yoyote ile. Nitaanzaje kumsaliti mwanamke anayejiheshimu, mama bora wa familia anayejitambua, mcha-Mungu na asiyeendeshwa na mihemko ya kidunia?. Kwakweli isingewezekana hata kidogo.

Wakati nataka kumpita yule binti, gafla akanisemesha "Jamani kaka mbona wanipita bila hata salamu?" Aliniuliza kwa lafudhi tamu ya kimwambao.
"Aah nisamehe bure dada nilikuwa mbali mno kimawazo" Nilimjibu ningali napunguza mwendo. Kadri alivyonikaribia nikaanza kuhisi harufu ya manukato mazuri ambayo sikuwahi kuyahisi hapo kabla.

"Pole na kazi" Alinieleza baada ya kunifikia.
"Ahsante dada nishapoa!" Nilimjibu.
"Si vibaya kama tukifahamiana. Mimi naitwa Kuruthumu, sijui mwenzangu waitwa Nani?" Alinitupia swali tukiwa tunaendelea kutembea.
"Mimi naitwa Masudi ila ukiniita Sudy chinga kama wengi wanavyopenda kulikatisha jina langu ni vizuri pia"
"oooh Wow! jina lako zuri sana, je pengine una mchumba, mke au hata rafiki wa kike?" Alinihoji.
"Ndio, nina mke na watoto wawili"Nilijieleza bila kuficha chochote.
"Hongera sana kwani kwa umri wako si rahisi mtu kugundua kama umeoa. Ila nilikuwa na ombi? " alinieleza.
"Nieleze tu usijali" Nilimjibu.
"Ningefurahi sana kama tutakuwa marafiki, je hilo nalo unalichukuliaje?"
"Sawa, kuhusu hilo ondoa shaka dada yangu" Nilimjibu.
"Wow! Ahsate sana, si vibaya tukabadilishana namba za simu." alinieleza kisha tukabadilishana namba za simu na kuagana.

Kabla sijafika nyumbani kwangu, uliingia ujumbe wa maandishi aliotuma Kuruthumu kwenye simu yangu.

"Nakupenda sana Masudi ijapokuwa mwenzangu tayari umeoa ila chonde, naomba niwe hata mkeo wa pili. Nakuahidi hutojutia upendo wangu endapo ukinikubalia. nitakufanya uwe mtu katika watu, hutokuwa na sababu ya kuungua juani. Please Masudi Open your Heart"

Sikuijibu ile SMS mpaka ulipoingia ujumbe mwingine tena ulionishangaza sana.

"Endapo utajaribu kunikataa, nitamuua mkeo na wanao kwa mkono wako. by kuruthumu malikia wa bahari ya Hindi" Niliusoma ujumbe huo huku nikiwa nimeyatumbua macho yangu juu ya kiyoo cha simu yangu. Nikamjibu nimekubali kusudi familia yangu isije kupatwa na baya lolote. Kwa mara ya kwanza nikatia password kwenye simu yangu ili Kuruthumu akituma Jumbe zake mke wangu asizione.

Nilifika nyumbani saa tatu usiku tofauti na ilivyo kawaida yangu. Nilikuwa sina raha kabisa, nikakosa hata hamu ya kula kitendo ambacho kilizua hisia mbaya kichwani kwa mke wangu.

Mke wangu alipogundua hali hiyo, alisubiri mpaka watoto walipolala. Kisha tukabaki mimi na yeye sebuleni.

“Unawaza nini mpenzi wangu?” Mke wangu aliuliza
“Nothing. Siwazi chochote zaidi yako na wanangu”.
“Sasa mbona huna raha, unaonekana una mawazo hata chakula ni mpaka ubembelezwe?usinifiche mkeo, maana leo upo tofauti na nilivyokuzoea.”

Kufuatia swali hilo nikabaki kimia kidogo bila kujibu chochote.
“Ni kitu gani kinakusumbua Sudy mume wangu hebu niambie. Au kama kuna kitu nimekukosea niambie nijirekebishe maana tangu tumeanza mapenzi yetu sijawahi kukuona ukiwa katika hali hii. ” Alinieleza mke wangu.

Mke wangu akashindwa kujizuia na kuanza kulia kwa kwiwi. Nikamvutia kifuani kwangu kisha nikambusu na kumwambia.
“Usihofu kitu baby, hakuna kitu chochote kile kinachonisumbua, ila uchovu wa kazi ndio umenipelekea kuwa hivi. Yaani sijisikii hata kula lakini usijali nitakuwa sawa mamaa” Nikamueleza huku nikizichezea nywele zake laini. Nafsini niliumia sana kumficha mke wangu ila ilinilazimu kufanya hivyo kwani sikujua kwamba endapo ningemueleza ukweli nini kingetokea kati yangu na Kuruthumu.

“Pamoja na hayo dear, najua lazima kuna kitu kinachokusumbua akili na hutaki kuniambia ” Agness mke wangu alizidi kunidodosa.
“My dear Agi, wewe ndio maisha yangu, wewe ndiye mfariji wangu, wewe ndio kila kitu maishani mwangu sasa kwanini nikufiche kitu?au kama sitakuambia wewe nimwambie nani mwingine tena?”

Nilijitahidi kumtoa mke wangu wasiwasi, taratibu akaanza kurudi katika hali yake ya kawaida na ucheshi mkubwa mno. akanipeleka maji ya kuoga bafuni. Nikiwa humo bafuni, Kwenye simu yangu niliyoiacha sebuleni kuliingia ujumbe.

Mke wangu akachukua simu ili ajibu jumbe ile kwamba naoga。Kwa mara nyingine akajikuta akiwa na wasiwasi juu yangu baada ya kukuta password kwenye simu yangu, jambo ambalo sikuwahi kulifanya tokea tumeanza uhusiano wetu.
ITAENDELEA....
 
STORY : JINI KURUTHUMU

EPISODE 2


Baada ya kumaliza kuoga nikarejea sebuleni alipo mke wangu.
"Hee! Agness my dear what's wrong with you mke wangu, mbona walia umepatwa na nini tena?"
Nilimuuliza mke wangu ambaye alinitizama tu huku machozi yakimtiririka.

"Sudy hakuna kitu nimewahi kukuficha wewe mpenzi wangu na haitakuja tokea nikawa na tatizo nikashindwa kukuambia. Lakini wewe mpenzi wangu umeanza kuwa msiri mpaka umefikia hatua ya kuweka password kwenye simu yako, je huniamini mkeo? " Akaniuliza Agness.

"Hicho tu ndicho kinachokuliza mke wangu? Usihofu kuhusu hilo my wife. I know what i'm doing ok?. Kama nilishindwa kukusaliti kipindi tukiwa wachumba iweje leo hii nikusaliti tukiwa tayari kwenye ndoa?"..

"Sudy mume wangu, siku hizi si kama zamani. Nilikuwa kama yai kwako kabla sijakuzalia, lakini baada ya kumzaa Naomi na Vick mahaba yote yamekwenda na maji. Sawa bwana endelea kuwa msiri na mambo yako. Hata huku kudamka kwako alifajiri kwenda kazini ninaanza kupata shaka sasa, si ajabu unaenda kumalizia usingizi huko kwa bi mdogo" Mke wangu alizidi kulalama.

"He mke wangu hayo yote yameletwa na nini? ni hii password tu kwenye simu yangu au kuna lingine? . Hembu naomba usitake kuamsha yaliyolala. Tena naomba yaishe kwa wema tu"

"Sawa nakubali yaishe, lakini unapaswa ujirekebishe mume wangu, siku hizi kuna magonjwa na ndio maana ninakuwa mkali sana na wewe. Sipo tayari kufa niwaache wanangu kwasababu ya starehe zako, Maana mienendo yako inaonyesha kabisa kwamba mwenzangu utakuwa umeshapata bibi mwingine zaidi yangu naona ndio anakuzuzua. Mlete basi tuhangaike naye hapa?" Alinieleza mama Naomi.

"Hee! haya ongea yote ukimaliza niruhusu na mimi niongee maana naona sikuizi wewe ndio kichwa cha familia. si unataka kunipanda kichwani haya ongea!"

"Sio hivyo baba Naomi, tatizo lako huambiliki, ukielezwa ukweli kidogo tu unasema nataka kukupanda kichwani . Agness uliyekuwa umemuoa si huyu pengine ndio sababu inakufanya unidharau, urembo ulionikuta nao ndio uliokuzuzua, sasahivi nishakuwa dubwana kama vile mcheza miereka, huoni tena thamani yangu. Sawa bhana"

"Ninakuelewa sana mke wangu, wala hunipi tabu. Yani ukianza kuongea humezi hata mate utadhani muhubiri injili. Nishakueleza yaishe lakini bado unachimbua chimbua sijui ni kitu gani unanitaka wewe mwanamke? Labda nikuambie haya maneno yako yote ni sawa na kelele za mlango, kama mwanaume ni mzizi atabaki kuwa mzinzi tu hata ufanye nini, lakini mimi sipo hivyo mke wangu ila kwakua una ubongo mdogo kama wa sisimizi kitu kidogo unataka kukikuza."

"Hebu nipe simu yangu bwana, siwezi kubishana na mwanamke mimi" Nilimueleza huku nikiikwapua simu yangu mkononi kwake na kuingia chumbani kwangu.

Mama Naomi alinifuata kitandani na kunipiga busu nzito.
"Nisamehe mume wangu kama nimekukwaza" Alinieleza.
"Nilishakusame mke wangu" Nilimjibu kisha tukakumbatiana mpaka usingizi uliponipitia.
**************
Hatimaye siku iliyofuatailikuwa ni ijumaa iliyotawaliwa na kiubaridi cha asubuhi. Hakukuwa na dalili zozote za kuchomoza kwa jua ingawa mida hiyo ilipata saa nne za asubuhi. Anga lote lilifunikwa na mawingu lakini pamoja na hali hii ya hewa wakazi wa Moshi walikuwa wakiendelea na shughuli zao kama kawaida.

Tofauti na ilivyo kawaida yangu Sudy Chinga, muda huo nilikuwa bado kitandani. Mwili ulikuwa umekataa kata kata kuachana na kitanda.
Muda huo mke wangu alikuwa akipika chai jikoni. Ndio ukaingia ujumbe wa kuruthumu kwenye simu yangu.
"Mambo Sudy , naomba tukutane makabrini Manyema mda huu " . Sikuwa wa kuswaki wala kukoga mwili. Asubuhi hiyo niliongoza hadi makaburini kusikiliza wito wa Kuruthumu.

Nilipokuwa nakaribia makaburini, kwa mbali nilimuona dada aliyekuwa amevalia vazi la baibui akiwa ameketi juu ya kaburi. "Vipi Kuruthumu? kulikoni umeniitia makaburibini. " Nilimuuliza baada ya kumfikia.
"Hapa ni sehemu inayojulikana kama kaburi la wapendanao . Sehemu hii ni sehemu ni sehemu ambayo watu wengi walio na uhusiano na majini hupenda kufika hapa kwa lengo la kukutana na wapenzi jini wao na kuwekeana ahadi mbali mbali mbali katika safari yao nzima ya mapenzi" Alieleza Kuruthumu kisha akaingiza mkono kwenye mfuko wa baibui lake na kutoa pete.

"Unaiona hii pete? ukitaka kitu chochote utakuwa unakipata ila kwa shariti moja tu, hutakiwi uwe na uhusiano na mwanamke wa asili yako namaanisha binadamu sawa?"

"Mh.. hapana , mimi nampenda sana mke wangu mama Naomi sitaweza kuvumilia kuishi bila yeye" Nilimueleza kuruthumu.
" Sawa! ni vizuri. Mke wako utaendelea kuishi naye lakini lakini hutakiwi kushiriki nae tendo la ndoa sawa? ..... na endapo utanisaliti nikijua utapata mateso makali kwanza ndipo kifo kifuatie. " Alinieleza Kuruthumu kisha akainivisha ile pete kiganjani mwangu na kupotea kiajabu katika eneo lile. Sikufanikiwa kuona japo sehemu aliyopitia.

Nini Kitaendelea? Usikose......
 
STORY : JINI KURUTHUMU

EPISODE 3

Wiki mbili ziliyeyuka kama mshumaa bila kumtia kuruthumu machoni tokea aliponipa pete ya ajabu pale makaburini na kisha akapotea kimazingira. Kuanzia siku hiyo na siku iliyofuata nikaanza kuona maajabu ya ile pete kama alivyonieleza Kuruthum.

*********
"Sudy amka darling unajua inakaribia saa sita sasa?" Alisema Agness mke wangu kwa sauti laini ya kubembeleza.

"Mmmmmh" Nikaguna kisha nikajigeuza upande wa pili na kulivuta zaidi shuka.

"Amka mme wangu, kumekucha ujue?" Mke wangu alizidi kunibembeleza. Nikafumbua macho na kutazama saa ya ukutani "Ah! yani nimelala mpaka saa sita " Nikatahamaki !. kisha nikaamka na kuelekea bafuni kuoga. Baadaye nikarejea chumbani kwangu, nikavaa .
Nilipokwisha kuuwa tayari, sikuwa na nafasi tena ya kupoteza muda. Nikamuaga mke wangu na kundoka.

********
Nilipofika kazini nilikutana na taarifa ambayo ilinishangaza mno.
" Sudy kuna dada amefika hapa asubuhi akaacha huu mzigo na kutoa maelezo kwamba ukija upewe " Alinieleza Masawe wakati akinikabidhi bahasha kubwa yenye rangi ya kaki. Kwakua nilielezwa kwamba ule mzigo ni wangu nikaifungua taratibu ile bahasha pale pale, nusura nipatwe na wazimu baada ya kuangalia kilichomo ndani, niliona noti nyekundu nyekundu tupu ndani ya bahasha ile, ikanilazimu kumuuliza tena Masawe.

" Masawe huyu Dada aliyekuachia huu mzigo alijitambulisha kwa jina gani?"

"Jina lake alisema anaitwa Kuruthumu. Akasema nikikueleza jina hilo utamfahamu na pia akasisitiza mzigo apewe Sudy chinga.".

"Sawa nimeshamfahamu" Niliongea kisha nikaondoka.
**************
Nikiwa bado katika mizunguko yangu, mke wangu akanitumia text "Nakuhitaji mume wangu mwili wangu unakutamani mno. Tafadhali leo usichelewe kurudi kazini my honey"
Nilikosa cha kumjibu, moyoni nikaanza kujisikia vibaya kwani tayari Kuruthumu alikwishanionya kutoshiriki tendo la ndoa na binadamu. Nikajikuta najutia ni kwanini niliacha kumshirikisha mke wangu habari za Kuruthum kuanzia mwanzo, Pengine
nikajiona ni jinsi gani nisivyoyathamini mawazo ya mke wangu kwa kutomshirikisha kwa lolote juu ya masahibu yangu.

"Sudy kuna kitu gani kibaya mbona tokea wiki hii imeanza unaonekana haupo sawa kabisa isitoshe hata nikikutumia text zangu hujibu. Darling una matatizo gani eti?" Aliniuliza mke wangu Agness.

"Usiogope Agness. Mimi nipo sawa kabisa, kaa chini tuendelee kupanga mipango yetu ya maisha"
"Ni sawa lakini mimi sipendezwi na hali hiyo uliyo nayo. Relax my dear. Jitahidi usiumize kichwa chako kwa mawazo. Kama ni ugumu wa maisha unapaswa kuzoea hali uliyonayo mume wangu kwasababu matatizo tumeumbiwa sisi wanadamu na hayakwepeki” Akanieleza mke wangu lakini ndani ya moyo wake alifahamu kabisa kwamba kuna jambo ambalo linanisumbua lakini namficha.

“Usijal mke wangu, nimekuelewa ” Nilijibu kisha nikaitoa ile bahasha yenye pesa na kumkadhi mke wangu. “ Hizo ni milioni 20. ni pesa za mkopo, mke wangu naomba tuzifanyie biashara kwa uangalifu ” Mke wangu akabaki amegandisha macho yake kwa mshangao juu ya ile bahasha.
“Eeh! lakini mume wangu ndio maana nakuambia umebadilika.Umekuwa msiri mno. Mbona hukunishurikisha habari mkopo. Aa’h ama kweli wahenga hawakukosea waliposema “Kuishi na mwenza msiri ama mbinafsi ndani ya nyumba ni sawa na kuishi na muuwaji bila kujua.”
“Hembu tusifike mbali mke wangu. Kuteleza kupo katika maisha. ”
“Oky Darling tuachane na hayo SMS yangu niliyokutumia mchana uliipata ” Akauliza Agness.
“Niliipata ndio, lakini sikuwa kwenye mood.”

“ ok nakutamani mume wangu twende chumbani”. Akanieleza mke wangu kwa sauti ya chini iliyojaa msisimko wa huba.
“ No!Utanisamehe mke wangu kwa leo, tutafanya kesho”
Kauli hiyo ilileta mzozo wa ajabu. “Nimechoka tabia yako uliyoanzisha. Naona umepata bibi mwingine wa kucheza nae bao. Sudy acha nichukue likizo ya ndoa kidogo maana sikuelewi wewe mwanaume. Mambo yako unafanya hunishirikishi. Huna furaha na mkeo, huniweki wazi matatizo yako . Naondoka!” Alisema Agness kisha akaingia chumbani na kutoka na begi lake la nguo
"Nimekupisha umlete huyo mpenzi wako mpya” Alinieleza huku akiondoka.
“Camon, Agness my wife. mbona unachukua maamuzi magumu mapema ivyo ?” Nilijaribu kumzuia lakini hakuzuilika. Aliondoka usiku ule ule.

**********
Wiki mbili zilikatika, nikawa nikimtafuta Agness kwenye simu yake hapatikani. Nikapiga simu kwa wazazi wake; wakanieleza kwamba alifika nyumbani. Akakaa kwa muda wa siku tatu kisha akaondoka. Sikuweza kuamini kabisa kwamba nimempoteza Agnes kirahisi namna hiyo lakini cha ajabu hata Kuruthumu mwenyewe sikufanikiwa kumtia machoni tokea nilipoupata mzigo wake.

Miezi sita iliyeyuka kama siagi kikaangoni. Hatimaye nikakutana na Vaileth rafiki yake Agness akitokea jijini Dar es Salamu. Nikamuomba namba za mke wangu Agness kwa bahati akawa nazo. Nikachukua simu yangu na kuandika namba zile kisha niliporejea nyumbani nikapiga huku mapigo ya moyo wangu yalikuwa yakinienda kwa kasi ya aina yake. Nilipoiweka simu sikioni nikaisikia ikiita. Mikono ilianza kuloa jasho kwa wasiwasi . Sikujua ningeongea nini baada ya kuisikia sauti ya Agness mke wangu. Sikujua Agness angekuwa katika ha li gani mara atakapoisikia Sauti yangu.Wakati nikisuburi kujibiwa na sauti ambayo nuliamini moja kwa moja ingekuwa ni ya Agness nikasikia kitu ambacho hakika sikukitarajia.

Nini kitaendelea!!!!!!
 
STORY: JINI KURUTHUMU

EPISODE; 4


INAENDELEA.

Wakati nikisubiri kusikia sauti ambayo moja kwa moja niliamini ingekuwa ni ya Agness mke wangu, ndipo nikasikia kitu ambacho sikukitarajia kabisa . "Hallo" Ikasema sauti upande wa pili wa simu. ilikuwa ni Sauti nzito ya mwanaume ambaye ndiye aliyeipokea ile simu ya Agness. Nikapatwa na kigugumizi cha gafla kilichonifanya nishindwe kuongea. Nikakata simu.

"Oooh my god. Kwanini mimi lakini?. I love
Agness. Na yeye ndiye mwanamke ninayempenda kwa dhati ya moyo wangu. Nimetengana naye muda mrefu sana na sielewi maisha yake kwa sasa nadhani tayari ana mume. “Agness I’ll fight for you and I must win you back.You are mine Agness .I lost you once and now I’ve found you I’ll never loose you again " Ni maneno yaliyonitoka kinywani kwangu huku machozi yakinichuruzika.
**********
Siku iliyofuata ilikuwa ni siku ya Jumatano, ambapo Saa kumi na mbili asubuhi ilinikuta nikiwa njiani naelekea kituo cha mabasi Moshi mjini. Kitendo kile cha kupiga simu ya Agness halafu apokee mwanaume kiliniuma sana. Nikaamua kusafiri kwenda nyumbani mkoani tanga kijiji cha Lushoto nikaongee na wazazi.
Baada ya kufika stand. Jamaa mmoja alinikimbilia na kuniuliza kwa ukarimu
"Kaka unaelekea wapi leo" Aliniuliza yule jamaa. "Naenda Lushoto" . Nikamjibu . "Gari lile pale linaondoka muda si mrefu tunasubiri watu wawili watatu halafu tunaondoka" Akanieleza yule jamaa huku akinisaidia mzigo wangu mpaka kwenye gari. "Mbona hakuna abiria yeyote?" Nikaukiza baada ya kulikuta gari likiwa tupu.

"Abiria wapo si unaona mizigo yao hiyo hapo.Wote wanasubiri muda ufike .Nikipiga honi tu watakuja wote.Wale wote unawaona ni abiria wengine wanakunywa chai kule na muda wa kuondoka ukifika basi watakuja..Unaweza kwenda kupumzika pale kwa yule dada naye ni msafiri anaelekea huko huko Lushoto wakati tunasubiri watu wawili watatu”

Nikasogea hadi kwenye kibanda kimoja cha biashara kilichokuwa hakitumiki. Msichana msichana mmoja alikuwa amekaa akisoma kitabu chake cha hadithi kilichoandikwa na mwandishi mahiri nchini Simba Mpole. Alikuwa amekiinamia kitabu hali ilionyesha kuwa amenogewa na kilichoandikwa kitabuni.

"Dada habari yako" Nilimsabahi. Akashtuka. Kwa sekunde kadhaa alibaki kimia akinitizama tu. Sijui ni kwanini alifanya vile lakini ni dhahiri alionyesha mshtuko fulani. "Nzuri habari yako?" Akajibu kwa sauti laini na ya taratibu sana. Sauti ile ilionyesha kuwa dada yule hakuhitaji kusumbuliwa kwa wakati ule kwani baada tu ya kuitikia salamu ile akainama na kuendelea kusoma kitabu chake.

Ningali bado nimesimama kando yake nikimtizama. Nikagundua ni kwanini dada yule amefanya vile. Dada yule alikuwa na uzuri wa kipekee.Alikuwa mweupe ,mwenye nywele ndefu zilizorudishwa nyuma vizuri na kumfanya avutie zaidi.Alikuwa na umbo nzuri lenye mvuto, kipotabo kama lile la Daina Nyange.

Binti huyu alijaliwa sura nzuri yenye mvuto wa kipekee. "Mmh! mambo ya Tanga hayo, natamani konda anipe siti ya karibu naye. Lakini anaonyesha ana nyodo kweli ila ngoja nimchokoze kwa maswali mawili matatu." Niliwaza akilini mwangu kisha nikaponyokwa na sauti.

"Dada Samahani kitabu chako kinaonekana kizuri kinaitwaje eti? Samahani lakini" Nikauliza.
"Kinaitwa My First Lover. Mwandishi ni simba mpole kwani vipi?" Akauliza. "Hamna tatizo nilitaka tu kufahamu, maana hata mini ni mpenzi wa hadithi mno. Dada yule akainua uso wake na kunitumizama kama alivyofanya mwanzo . .Macho ya binti huyu yalikuwa meupe na makali kiasi kwamba akikutizama unaweza ukakwepesha macho yako asikuangalie. "Kwani wewe unaelekea wapi? " Akaniuliza. "Naelekea Lushoto" nikamjibu.
"Ooh kumbe tupo pamoja, basi nitakuachia usome gari likianza kuondoka" Akanijibu yule binti. Taratibu tukaanza kuzoeana . Binti yule kumbe alikuwa mcheshi na muongeaji mzuri tu. Kwa upande wake naye alifurahia sana uchangamfu wangu . "Vipi maisha lakini? " Aliniuliza yule binti. "Maisha yako poa, tunashukuru Mungu kwakua bado tunahema".
"Kweli kabisa ni jambo la kushukuru"

Alinijibu yule binti. kimia kidogo kikachukua nafasi, nikaamua kuuvunja ukimia ule kwa kuuliza "Kwani wewe dada unaitwa nani?"
Binti yule akatabasamu kisha akanitizama kama mtu anayejishauri aseme au asiseme. Akajikuta akitamka "Naitwa Lola Kipingu wewe unaitwa nani ?".

"Naitwa Sudy. Lola nimefurahi sana kukufahamu na kama hutojali nitafurahi ikiwa utakuwa mmoja wa marafiki wa kubadilishana mawazo" Nikamueleza.
"Hilo tu usijali. Napenda marafiki wa kiume maana najifunza vitu tofauti tofauti kutoka kwao". Alinieleza kisha Dereva akapiga honi akiwaita abiria. Muda wa kuondoka ulikuwa umewadia.

Tukiwa garini Utingo akaanza kuchukua nauli. Lola akatoa noti mbili nyekundu na kumlipa yule utingo.
"Kata nauli ya watu wawili"
"No Lola nina nauli yangu hapa" Nikaeleza.
"Usijali Sudy Just keep it" Akasema Lola huku akitabasamu. Abiria wote waliokuwamo katika ile gari macho yao yalikuwa kwa binti huyu mrembo.Kwa muonekano wake alionyesha dhahiri kuwa alitoka katika familia yenye uwezo mkubwa kifedha.

Je nini kitaendelea....? Hungana na mi katika simulizi hii ya JINI KURUTHUMU.
 
Hili jini lina mawivu ya kijinga afu libabe....Ila huyo Soudy inaonyesha ni mzoefu wa kugegeda majini mbona hata hajaogopa wala kushtuka
 
STORY : JINI KURUTHUMU

EPISODE;5

ILIPOISHIA.
Abiria wote waliokuwamo katika ile gari macho yao yalikuwa kwa binti huyu mrembo. Kwa muonekano wake alionyesha dhahiri kuwa alitoka katika familia yenye uwezo mkubwa kifedha.

SONGA NAYO.
"Jamani abiria tumefika. Poleni na Safari" Akasema utingo wa lile gari tulimokuwa tumepanda mimi na Lola.
Mida hiyo ilipata saa saba mchana. safari ilikuwa ni ndefu kidogo hasa kutoka na barabara.
" Sudy tushuke" akasema Lola akiwa wa kwanza kushuka kisha akaanza kupokea mizigo yangu.
" Brother hujanilipa hela ya mizigo" Akanisemesha utingo.
"Usijali namtolea " Akasema Lola kisha akatoa pesa na kumlipa yule utingo.
" Poa mrembo karibu tena siku nyingine eh?" Akasema utingo huku akimminyia Lola jicho moja baada ya kupokea pesa.
Idadi kubwa ya watu waliokuwa pale stand walisimama wakitushangaa.
"Lola mbona watu wanatushangaa sana?"
"Just ignore them (wapotezee) si unajua huku bado ni kijini" Akasema Lola huku akinisaidia mizigo aliyoimudu kuibeba.
" Unaona pale juu kwenye geti la rangi nyeusi? " Akaniuliza Lola huku akinielekeza kwa kunyoosha kidole chake.
"Ndio nimepaona" Nikamjibu.
"Basi pale ndio kwetu, baba yangu anaitwa Mathius shirima na mama yangu anaitwa Upendo Shirima. Mda wowote njoo utanikuta." Akanieleza Lola kisha tukaagana kwa kubadilishana namba za simu.
" Byeee...eh mmmmwaaa!" Akasema lola huku akinipeperushia busu la mbali na kuonyesha meno yake meupe na mwanya wa kupendeza katika meno ya juu.
"nashukuru sana Lola, Mungu akipenda kesho jumapili nitakuja kukuona."
"Usijali karibu sana"
*************
Nilifika nyumbani kunako saa tisa alasiri. Ujio wangu uliwashangaza sana mama na baba pamoja na dada zangu Manka na Dativa.
"Sudy huko mjini utokapo ni kwema. Maana sio kawaida yako kuja nyumbani kwa kushtukiza?" Aliniuliza baba.
"Sio kwema baba. Mama Naomi kanikimbia, kambilia huko Dar es Salam?"
"Toka lini mbona hujatuambia? " Aliuliza mama kwa mshangao.
"Miezi sita sasa inaisha toka aondoke" Nilieleza.
"Ah! lakini mwenetu umezidi kuwa msiri mno, miezi sita yote unaishi bila mke? Hao wajukuu zangu Naomi na Vick wanapikiwa na nani?" Mama alizidi kunihoji.
"Nilikuwa napika mwenyewe nikitegemea mama Naomi atarudi. Juzi nimepiga simu yake akapokea mwanaume"
"Haa! yani huyu mwanamke kumbe ni malaya. Lazima arudi hapa! Kwanza ngoja nimpigie Sheik Sharifu"
Akasema baba huku akitafuta jina Sheikh Sharifu kwenye simu yake. Sekunde chache tu baadae alimpata kisha akapiga.
"Hallo shehe kwema. Nina kijana wangu kakimbiwa mkewe sasa nilitaka umvute mkewe tena umvutie hapa nyumbani. Yani na mahari tumeshalipa kabisa sheikh wangu halafu mke anakimbia Ah!" Alieleza baada ya kusalimiana na Sheikh Sharifu.
"Sawa nitahitaji kuku mweupe asiye na doa, mayai viza mawili, nazi mbili, nyembe mbili na mchele kilo moja". Sauti upande wa pili wa simu ilisikika ikieleza.
"Ahsante Sheikh wangu na je itagarimu shilingi ngapi?" Baba akauliza.
"Kupiga ramli peke yake ni elfu kumi na kutatua tatizo ni elfu hamsini" Alieleza Sheik sharifu kwenye simu ya baba.
"Sawa sheikh. Jumatatu tutakutembelea" Akasema baba kisha akakata simu.
"Usijali mwanangu lazima arudi atueleze huko Dar es salamu ndiko alikoozeshwa na wazazi wake?"
Alinieleza baba kisha tukaendelea na maongezi mengine.
*************
Basi masaa yakakatika na giza likachukua nafasi,
Usiku huo ukawa mgumu sana kwangu. sikujua ni kwanini Lola alikuwa ameniingia moyoni mwangu kwa kasi ya ajabu namna ile.
"Sielewi ni kwanini binti huyu amenigusa gafla hivi. Ni binti mpole, mtaratibu na mwenye kuvutia kwa tabia zake. Ingawaje baba anataka kumrudisha mama Naomi, lakini hata asiporudi nitajifariji na Lola, lakini mh...wait.. vipi kuhusu Kuruthumu, naye ni mwezi wa sita sasa sijamtia machoni wala kuwasiliana nae au keshanipotezea?. Nisije nikajiingiza kwenye mapenzi na lola badaye Kuruthumu akanidhuru.?" Niliwaza wakati nikiwa katika mawazo mazito mno kitandani kwangu.

Hatimaye siku niliyopanga kwenda kumsalimu Lola nyumbani kwao ikawaidia.
Nipofika nyumbani nyumba yenye geti la rangi nyeusi kama Lola alivyonielekeza kuwa ndio ndio kwao, nikaona kitufe ambacho mgeni akitaka afunguliwe geti, basi kinabonyezwa kisha mgeni anafunguliwa.
Ilikuwa ni nyumba ya kifahari, kwa mtizamo tu ungejua kuwa wanaoishi humo ndani sio wachovu au watu wa mchezo mchemzo hahahaa..
Nikabonyeza kitufe kile, mara moja akatoka kijana wa makamo yangu.
Alipofungua mlango, akaniuliza " vipi kijana unamtafuta nani?"
"Mimi ni mgeni wenu" Nilimueleza hivyo tu kwa kifupi.
"Twende ndani basi" akaniambia.
Tukaongozana mpaka kwenye chumba cha kupumzikia cha nyumba hiyo, nyumba ambayo ilionekana ni ya watu wenye ahueni na maisha.
Mara baada ya sekunde kadhaa alikuja mzee mmoja ambaye kimuonekano alionekana kuwa ndiye baba wa nyumba hiyo.
"Karibu kijana. habari yako? "Akaniuliza
"Salama baba".
"Enhee nimeambiwa na mlinzi wewe ni mgeni wetu je ulikuwa unamuhitaji nani?" akaniuliza.
"Namuhitaji Lola " Nikamjibu.
"Lolaaa!" Mzee yule akaonyesha mshangao kisha akaendelea.
"Kijana upo sawa sawa kweli?" Akaniuliza kana kwamba ananichulia kama mtu aliyevurugwa.
"Ndio nipo sawa mzee. Lola kanielekeza hapa ndio kwao, baba yake anaitwa Matiasi shirima na mama yake ni Upendo Shirima.!"
Akanitumbulia macho kisha akatamka.
" Matiasi Shirima ni mimi, na Upendo Shirima ni mke wangu. Sasa huyo Lola unayemzungumzia wewe ni mwenetu na hatunae tena. Alipoteaga zamani sana katika mazingira ya kutatanisha akiwa anasoma kidato cha nne. Na jina lake sio Lola. Lola ni jina la shule. Jina lake yeye anaitwa kuruthumu. Sasa wewe huyo Kuruthumu (lola) umemuona wapi?". Kufuatia swali hilo nilibaki kimia ningali bado katika mshangao.

Je nini kitaendelea?
 
Aiseee
Hapo mwisho mmh
 
STORY : JINI KURUTHUMU.

EPISODE; 6


" Matiasi Shirima ni mimi, na Upendo Shirima ni mke wangu. Huyo Lola unayemzungumzia wewe ni mwenetu na hatunae tena. Alipoteaga zamani sana katika mazingira ya kutatanisha akiwa anasoma kidato cha nne. Na jina lake kamili sio Lola. Lola ni jina la shule. Jina lake yeye anaitwa Kuruthumu. Sasa wewe huyo Lola umemuona wapi?". Nilibaki kimia ningali bado katika mshangao.

SONGA NAYO.

Mzee yule akaingia ndani kisha akatoka na picha mbili akiwa amezishika mkononi Akaniuliza.
"Huyo Lola uliyemuona wewe anafanana na huyu hapa kwenye picha?"
"Hapana, mbona huyu namfahamu. Huyo niliyekutana naye hafanani na huyu?"
"Je huyu unamfahamuje kwasababu ni marehemu?"
Kufuatia swali hilo taswira ya miaka 11 iliyopita ilinijia kichwani mwangu, na wakati taswira hiyo inapita ubongoni mwangu ilikwenda sanjari na picha halisi ya maisha yangu ya kipindi hiko nikiwa mwanafunzi.
*********
Mwaka 2009 baada ya wazazi wangu kukamilisha ujenzi kijijini , tulihama mjini na kwenda kijijini ambako niliendelea na masomo yangu ya kidato cha pili katika shule ya secondary LWANDAI iliyopo Mlalo wilaya ya Lushoto mkoani Tanga.

Siku moja kabla ya siku ambayo nilianza kwenda shule, nilikutana na msichana mzuri kisimani ambaye alijitambulisha kwangu kwa jina la Lola.
"Lola , mimi ni mgeni na kesho nitaanza kwenda shuleni kwenu hivyo nilihitaji kuyafahamu mazingira ya shule yenyewe kabla sijafika"
"Kwani wewe unatokea wapi?" Akauliza yule msichana.
"Natokea Majengo Secondary"
"Uko kidato cha ngapi?"Akauliza tena yule msichana.
"Kidato cha pili?" Nikamjibu.
"Hata mimi niko kidato cha pili" Akanieleza yule msichana.
"ooh! Kumbe tuko kidato kimoja?"
"Yeah. Ila pale kuna michepuo miwili mimi niko mchepuo wa sanaa (arts) wewe je?"
“hata mimi ninasoma sanaa.Vipi unaionaje shule kwa ujumla ? ufundishaji wao ukoje ? Nikauliza.
“wanajitahidi kufundisha.Kumetulia na ni sehemu nzuri kwa kusoma.Mi napapenda sana”akajibu yule binti.
"Mimi nitakaa bweni? Mabweni yao si yapo vizuri?"
"Yapo vizuri, hata mimi nipo bweni ila leo jumapili niliomba ruhusa ya kurudi nyumbani" Akanieleza yule binti.
“aisee kumbe wazazi wangu wamefanya chaguo nzuri kunihamishia kijijini." Nikasema.

‘Mimi mwenyewe mwanzoni nilidhani kuwa nilikosea kuhamia shule hii .Mwanzoni nilipata shida sana kuzoea lakini mpaka sasa nimeshazoea na nimetokea kupapenda sana ”Akajibu yule binti.
“Kumbe hata wewe ulihamia?" Nikamuuliza
“Yes .Nilikuwa nasoma Mbezi secondary nikahamia huku. Sikutaka kusoma mjini nilitaka kusoma mahala tulivu mbali na nyumbani ” akasema yule binti kisha akaibeba ndoo ya maji kichwani na kuniaga.
"Haya mwaya ngoja nikuache tunaonana kesho shuleni"
"Sawa, lakini ni matumaini yangu kwamba utanisaidia kuyazoea mazingira ya shuleni au vipi " Nikamueleza.
"Usijali, karibu Sana"
**********
Siku iliyofuata nilipelekwa na baba shuleni. Mkuu wa shule hiyo akaniandikisha na baadaye akamuita mwanafunzi mmoja na kumuomba anipeleke katika bweni la Mandela.
Mwanafunzi huyo akanisaidia mizigo yangu na kumpeleka katika bweni hilo lililo upande wa juu kabisa wa shule.
Pale bwenini nikapata kitanda kilichokuwa wazi nikaweka mizigo yangu. Nikajilaza kitandani huku nikijaribu kuwaza jinsi nitakavyoweza kuyakabili maisha mapya ya shuleni pale. Sikuwahi kusoma katika shule ya bweni na hii ilikuwa mara yangu ya kwanza.

“lakini Lola yupo atanisaidia kuyazoea maisha ya hapa. Kama yeye mtoto wa kike amezoea kwa nini mimi nishindwe ? Nitazoea tu. Halafu shule hii inaonekana ina wanafunzi wababe mbona kuna visu huku bwenini? " Niliwaza baada ya kutupia macho yangu kitanda cha pili na kuona kisu kidogo.

Mawazo yake yakastuliwa na sauti ya mwanafunzi mmoja aliyeingia bwenini humo kwa kelele. Akanisogelea naa kunisalimu kisha akaelekea katika kitanda chake kupumzika.

Wakati wa prepo (masomo ya usiku) Nikatembelea madarasa ya kidato cha pili.
Yalikuwa ni madarsa yaliyofuatana.Yaani kidato cha pili A B na C. Mimi nilikuwa nimepangiwa kusoma kidato cha pili C. Nikayapita madarasa ya A na B nikaelekea katika darasa la C .Mlango haukuwa umefungwa nikaingia ndani na mara macho yake yakagongana na macho ya Lola.
“Lola !! ..” nikaita kwa mshangao. Sikutegemea kama ningemkuta Lola mle darasani.
“Sudy! Naona umeshaanza kuwa mwenyeji" akasema Lola huku akitabasamu.
Nikacheka.
"Karibu tusome. Kwani umepangiwa darasa gani" Akaniuliza.
"Nimepangiwa darasa hili hili je wewe?" Nikamuuliza.
"Hata mimi ninasoma humu humu" akanieleza.

Urafiki wangu na Lola ukazidi Kukomaa, lakini cha ajabu kila wakati nilipokuwa na Lola wanafumzi walikuwa wakitushangaa mno. Nikaamua kumuuliza Lola.
"Lola mbona kila mtu hapa shuleni anatuangalia Sana ni kwanini" Nikamuuliza.
"Achana nao Sudy , Jali mambo yako. Kamwe usiwasikilize wanafunzi wa hapa wana mambo ya kipuuzi sana. wakiona mtu mgeni sijui wanakuwaje. ukitaka kuishi kwa amani mahala hapa jitahidi kufuata kile kilichokuleta yaani masomo” Lola akasema kwa sauti ambayo haikuwa ile yake ya kawaida. Nami sikutaka kuuliza tena kuhusu suala hilo.

Siku za mwisho wa wiki, nilikaa pamoja na Lola. Tukisoma pamoja. Na hata wakati mwingine tulishiriki pamoja chakula. Urafiki wetu ukawa na nguvu sana. Darasani tulikaa pamoja lakini bado tabia ya wanafunzi kutushangaa ilikuwa endelevu.
Siku moja wakati nimekaa na Lola, akaja binti mmoja kwenye dawati letu.
"Lola naomba daftari lako la kiswahili nimalizie kazi ya mwalimu shayo"akasema yule binti.
"Mi daftari langu siwapi tena. Nikiwapa hamrudishi kwa wakati... aka! Kamuombe mtu mwingine" Akasema Lola.
"Heee! bibi unaringa wewe. Asiyekujua kwamba wewe ni mgonjwa ni nani, unaumwa ugonjwa wa kufa na kufufuka halafu unaleta maringo" Kufuatia kauli hiyo Lola hakujibu chochote bali akaanza kulia.
"Nyamaza Lola !, nipo hapa kwa ajili yako"
"Mimi sijui nimewafanyaje wanafunzi wa shule hii. Yani wananichukia tu bila sababu na kunitamkia maneno ya fedheha." Akasema Lola kwa sauti iliyotawaliwa na machozi.
"Dont wory Lola. Hata kama wakikuchukia na kusimama mbali na wewe mimi nipo kwa ajili yako". Nikambembeleza Lola huku yule binti akiwa ananishangaa.
" Na wewe usipende kushobokea shobokea tu wasichana usiowajua, utashobokea wafu" akanieleza yule binti kauli ambayo ilininyanyua kwenye dawati langu na kumnasa kibao.
Wakati najiweka sawa ili nimuongeze kibao cha pili. Mwanaume mmoja akaukamata mkono wangu. Ingawaje alikuwa ni mwanafunzi lakini alikuwa na mwili mkubwa uliojengeka vyema kama mnyanyua vyuma. Inasadikika kwamba yeye ndie aliyekuwa anapiga shule nzima licha ya kwamba anasoma kidato cha pili.
"Apigweeeee huyoooo! . Anaringa sana acheni afunzwe adabu. Kahamia tu juzijuzi tu hapa anataka kututawala wazawa. " Yalikuwa ni maneno ya wanafunzi wakishangilia wakati nikiwa nimepigwa kabali na yule jamaa.
Nikajikakamua mpaka akaniachia. Wakati naliweka shati langu sawa. Akaituma ngumi nzito usoni mwangu. Nikapandwa na hasira isiyo na kifani.
Nikamsuma kwa nguvu. Moja kwa moja akaelekea sakafuni huku akiwa ametanguliza mkono wake wa kulia.
Kilichosikika baada ya hapo ni kilio cha nguvu huku akilalamika nimeuvunja mkono wake.
Kelele zikawa nyingi na zikamfikia mwalimu aliyekuwa darasa la karibu ambaye alifika haraka kuona kuna nini akakuta kuna ugomvi mkubwa. Wanafunzi walipomwona mwalimu wakakimbia kila mmoja katika kiti chake kasoro mimi ambaye nilikuwa nimesimama bado nisijue ni nini cha kufanya.
ITAENDELEA......
 
Apa amna ktu amekop na kupaste miss Tanzania *****
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…