IZENGOHADITHI
Member
- May 5, 2017
- 21
- 39
FISADI WA KUZALIWA
Ni kwa miaka mingi nchi ya Chamongo iligubikwa na wimbi zito la ufisadi na kujilimbikizia madaraka,tena kwa wale wasio na sifa ya kuwa na madaraka hayo.
Wasomi na baadhi ya wananchi waliyaona hayo na kupaza sauti zao kupitia vyombo vya habari,lakini kelele zao hazikumzuia ng’ombe kunywa maji.
Kwa kuwa raia wa nchi hii walinyimwa elimu ya demokrasia na utawala bora hawakuweza kuona kwa urahisi madudu yaliyokuwa yakifanyika ndani ya serikali yao.
Wananchi walilalamika hali ngumu ya maisha,ambayo ilienda sambamba na mfumko wa bei za vyakula. Umuhimu wa kuwa na serikali katika nchi hiyo haukuonekana kwani gharama za maisha zilipanda kila kukicha.
Wananchi walilazimishwa kulipa baadhi ya madeni ambayo serikali yao iliingia mikataba mibovu na kuonekana kuwa mikataba hiyo ilikuwa ni ya mafisadi waliokuwa na jina la kutukuka wakiitwa waheshimiwa.
Watu hawa hawakufaa kuitwa jina hilo kwani jina ‘mheshimiwa’ ni jina ambalo huitwa watu ambao ni wazalendo wenye machungu na nchi yao,wenye kutetea wanyonge kama wamachinga,madaktari, walimu na wote waliokata tamaa na maisha.
Jina hili limekua likitumika kwa matapeli,wezi,wachoyo na wasio na uchungu wa mali za nchi yao. Ulikua ukijiuliza mafisadi ni watu gani na chanzo cha kua fisadi ni nini?Jibu linapatikana katika mfululizo wa hadithi hii ya fisadi wa kuzaliwa.
Hebu sasa tuangalie chanzo cha ufisadi kwa kupitia Soni kijana aliyekua fisadi tangu alipozaliwa mpaka kufa kwake.
Soni ni mzaliwa wa kijiji cha Lwanande Mkoani Ardhini wilayani Kapuuzi.
Soni aliishi na wazazi wake tangu kuzaliwa mpaka alipofikia miaka ya kujitegemea,aliyaanza maisha ya ujana kwa kumiliki mali kedekede na pesa lukuki.
Soni alikua na tabia ya uchoyo tangu utoto wake,hali ya ubinafsi ilimfanya achukizane na wenzake.
Katika hali ya kushangaza alipenda sana kuomba vya wenzake lakini vya kwake alikuwa mgumu kutoa.
Baba na Mama yake walikuwa ni wakulima na wafugaji katika wilaya ya kapuuzi.
Katika hali ya kushangaza Soni aliingia mahakamani akiwa mwenye umri wa miaka kumi, kwa kosa la kumtapeli mfanya biashara wa duka la nguo kiasi cha shilingi laki mbili na nusu.
Hali hii iliwashtua sana wazazi wake,kwa kuwa alikuwa ni hodari wa kuzungumza alishinda kesi hiyo.
Alifanikiwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Mwan’ganda na kufanikiwa kushika nafasi ya juu ya uongozi katika shule hiyo.
Akiwa shuleni alitumia vibaya pesa ya shule ambayo alipewa kwa ajili ya manunuzi madogo madogo ya shule kama vile sabuni za chooni,chaki na mifagio.
Soni alionekana kuwa na pesa kuliko wanafunzi wote shuleni kwani haikupita wiki aliomba pesa kwa wazazi wake akiwadanganya kuwa kavunja maabara,wanachangia mishahara ya walimu,amepoteza biolojia,ameibiwa chemistry na amevunja hesabu.
Kwa kuwa wazazi wake Soni waliogopa umande(hawakusoma) waliuza kuku,mayai na maziwa ili kuzilipa hizo biolojia alizokuwa akizivunja mtoto wao.
Hayo yote waliyafanya ili kuepusha asisimamishwe masomo.
Soni alifanikiwa kujiunga na kidato cha tano,akiwa katikati ya masomo yake alikuwa na ndoto za kuongoza nchi ya Chamongo iliyojaa maziwa na asali.
Aliamini kuwa siku moja ndoto zake zitatimia alikua na uwezo mkubwa wa kujielezea na aliweza kushawishi wakubwa na wadogo kufanya jambo Fulani.
Akiwa shuleni hali ya ubinafsi ilikuwa ndani ya moyo wake,hakupenda kushirikiana na mtu yeyote kwa lolote lile.
Maisha yake yalikosa taa ya mwongozo wa taa ya Mungu kwa kifupi aliishi maisha ya kupenda anasa na tamaa za kuwa na mali nyingi. Nini kitaendelea tukutane kesho kwenye mwendeleza wa hadithi hii