Muuza simu used
JF-Expert Member
- Aug 23, 2017
- 4,393
- 7,108
Mafanikio ni kitendawili kinachoweza kutegulika,kama unafanya biashara fulani na unaona haikulipi fanya nyingine,kama unaishi mkoa fulani na mambo yanazidi kuwa magumu hamia mkoa mwingine,kama wewe ni Mtanzania na unaona Tanzania hufanikiwi nenda nchi zingine sababu hao wanaotuongoza leo wanaotuaminisha Tanzania ni nchi Tajiri wamesomea nchi nyingine, upo na marafiki wanaokuletea hasara badala ya faida achana nao kuwa na marafiki wengine,umeona mbinu zako zinafeli basi tumia mbinu nyingine,Ili tufanikiwe inabidi tutumie akili nyingine na nyingine na nyingine tena