Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 39,802
- 71,229
Kweli homa ya uchaguzi mkuu ni mkali kuliko malaria au tishio kuliko huu ugonjwa wa sasa.
Serikali wakati huu wa janga la corona huku ikipita kuomba misaada kutoka kwa kina Rostam Aziz lakini imekumbuka kuwa uchaguzi waja na kura za watumishi ambao kwa miaka minne haijapata kuwaongeza mishahara wala annual increments zilizopo kisheria kamwe haiwezi kuzipata.
Hivyo imekuja na mkakati wa kuwapoza kwa kuwaambia yaweza kuwapa mikopo ya muda mrefu pesa za kununua magari au pikipiki.
Hivi watumishi wanahitaji magari na pikipiki au kuboreshewa maisha yao kwa kipato? Mbona serikali hii ya awamu ya tano inahusudu sana VITU kuliko maendeleo ya watu na maisha bora?
Hadaa hii kwa kweli ni ya kushangaza maana hata kupambana na gonjwa hili la sasa serikali inategemea kuchangiwa wakati wao wanajitapa kutaka kukopesha watumishi eti magari!
Je, hii sio hadaa ya kutaka kupata huruma ya kura za watumishi walio kasirishwa na kuonewa, kupuuzwa na kukandamizwa?
Watumishi mnasemaje, jee mko tayari kupokea hadaa hii kwa kuuza utu wenu na kutoyaona mapungufu yote ya awamu hii na kuipa support katika mitindo yake ya "bao la mkono"?
Sent using Jamii Forums mobile app