Hackers waingilia ATM za Standard Chartered, wakwapua pesa

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,504
upload_2016-4-10_21-57-42.png

Wahalifu wa mitandao wamedaiwa kuingilia akaunti za wateja wa Benki ya Biashara ya Standard Chartered na kuiba fedha kiasi ambacho hakijajulikana.

Mkuu wa Uhusiano na Masoko wa benki hiyo, Joanita Mramba alisema wamechukua hatua ikiwamo kuzuia kadi za kutolea fedha na kuanza mchakato wa kutengeneza kadi mpya ili kudhibiti wizi huo.

“Kwanza kabisa nawahakikishia wateja wetu fedha zao ziko salama na wasiwe na wasiwasi waendelee kufurahia huduma ya benki yetu.

Alisema tukio hilo lilianza kujitokeza mwanzoni mwa wiki iliyopita na benki iliwataarifu wateja wake kwa simu kuwa kuna jaribio la kuingilia akaunti zao ili kuibiwa fedha zao.

Mkazi wa Kimara, Method Makumvi aliyekumbwa na mkasa huo alisema alibaini kuwa ameibiwa baada ya kukosa fedha kwenye akaunti yake jana.

“Nilifika katika moja ya mashine za ATM, iliyopo Mwenge, kutoa fedha ya mafuta ya gari langu.Bahati mbaya sikukuta kitu na akaunti ilikuwa na kiasi cha Sh800,000,” alisema Makumvi.

Aliongeza kuwa baada ya kubaini tukio hilo alikwenda moja tawi la benki hiyo maeneo ya Shoppers Plaza na kuwaelezea mkasa huo.

“Wahudumu wa benki waliniambia siyo mimi pekee niliyekumbwa na mkasa huu. Wakanishauri nijaze fomu kwa ajili ya kuzipata fedha zangu zilizokuwa katika akaunti,” alisema.

Kutokana na tukio hilo, Makumvi alielezwa na wahudumu wa benki hiyo kuwa wameamua kuzuia kadi za ATM za wateja wote na kuamua kutoa kadi mpya lengo likiwa ni kupambana na wizi huo.

Source: Mwananchi.

My take: Wateje wa Standard Chartered mkaangalie taarifa za akaunti zenu.
 
wamerudi tena hawa jamaa kwani ni muda walitulia vyombo vya ulinzi shime watu hawa wafatiliwe na kukamatwa haraka wakiachiwa watatuharibia uchumi wa nchi
 
wamerudi tena hawa jamaa kwani ni muda walitulia vyombo vya ulinzi shime watu hawa wafatiliwe na kukamatwa haraka wakiachiwa watatuharibia uchumi wa nchi
Wanaumiza sana watu aisee.

Ila mara nyingi wanakuwa na uhusiano na watumishi wa ndani wasio waaminifu wa hizi benki zetu
 
Huu ujinga mimi nasema unafanywa na watu wa humo humo kwenye hizo taasisi... Hakuna loop ya ku hack hizo system labda mtu wa humo ndani ndiyo afanye huo ujinga...
 
Huu ujinga mimi nasema unafanywa na watu wa humo humo kwenye hizo taasisi... Hakuna loop ya ku hack hizo system labda mtu wa humo ndani ndiyo afanye huo ujinga...
yap, mara nyingi wahujumu wa hii mifumo huwa wanatoka humo humo ndani, hasa watu wa IT na data security
 
Sasa hapo kaambiwa aandike barua ya kurudishiwa pesa zake, lakini huo mchakato wa kurudishiwa pesa ni mrefu kweli yaani inaweza kuchukua miezi mitatu mpaka sita. Sijui kwa nini hata benki za biashara zinakuwa na urasimu mkubwa kiasi hiki. Yaani ni kama unawaomba msaada vile
 
Bank tunazozipapatikia bongo hazina huduma madhubuti na zile tunazozidharau kama bank ya makabwela ndio za kuaminika zaidi. Wachache wanaelewa hilo
 
Kuna Jamaa tulikuwa nae Msibani akapokea msg kuwa amefanikiwa kutoa pesa kwenye ATM... akajua keshaliwa haukupita muda msg nyingine pesa zimetolewa akijisachi ATM card anayo mfukoni.... Upande wa Mitandao tupo down sana
 
Bank tunazozipapatikia bongo hazina huduma madhubuti na zile tunazozidharau kama bank ya makabwela ndio za kuaminika zaidi. Wachache wanaelewa hilo
Unamaanisha nmb?hao ndio mabingwa wa kuibiwa kwa sim banking
 
Mhh
Kuna Jamaa tulikuwa nae Msibani akapokea msg kuwa amefanikiwa kutoa pesa kwenye ATM... akajua keshaliwa haukupita muda msg nyingine pesa zimetolewa akijisachi ATM card anayo mfukoni.... Upande wa Mitandao tupo down sana
Mhh hiyo mbaya unaweza jikuta unalia ghafla watu wakajua unalia kwa ajili ya msiba
 
hiyo kauli ya huyo mkuu wa masoko ni tata kweli: yaani anasema wateja wasiwe na wasiwasi fedha zao ziko salama wakati wameshaibiwa? haya ni maajabu ya karne.
 
Huuu mchezo ni rasmi
Watu wa IT wa Banks husika wanahusika
Huu utoto mtupuu,Standrad Charted ni Brand kubwa sana na sio rahisi kuingia kwenye mtego huo kizembe namna hiyo.
Hachers ni nyie kwa nyie msituzingue,mbona ATM zenu zoote zina Cameras,sasa inakuwaje mshindwe ku trace wahusika?
Hapo pia kuna deal la Tender ya kutengeneza kadi hizo watu wanapiga tena,aiseee
 
Back
Top Bottom