Habiba Kawawa afariki Dar

Habiba ni mmoja tu ya wanawake maelfu wanaopoteza maisha kutokana na uzazi hapa Tanzania na Africa kwa ujumla,Tanzania ukibeba ujauzito yaani ni riski ya kufa wewe mwenyewe wakati unapotegemea kukipa maisha kiumbe kilichopo tumboni,yaani ni mguu mmoja kaburini.Sijui hili tatizo litaisha lini wenzetu wamefanikiwa kulitatua.
Pumzika kwa amani Habiba.
 

WoS ni kweli kabisa katika nchi za wenzetu vifo vya akina mama wajawazito ni vichache mno ukilinganisha na Tanzania. Hata kwetu hali ingeweza kuwa hivyo lakini Serikali zetu zilizo madarakani hasa hizi za miaka ya karibuni hazikuona/hazioni umuhimu wowote wa kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na matokeo yake wengi wataendelea kufa kila mwaka. Miezi michache iliyopita Naomi Campell alipotembelea chumba cha akina mama waliotoka kujifungua aliangusha machozi kutokana na hali ya kusikitisha aliyoiona ya chumba kidogo cha kulala mama mzazi mmoja wamerundikwa (kama magunia ya mkaa) akina mama 20 au zaidi na wengi wakishare kitanda kimoja au tandiko moja kati ya watano au zaidi.
 
Mkuu naona umebadili jina!

Ndugu yangu anambwe mbwe sana SteveD kuwa SteveDII

Huu ni umasikini wa hali ya juu Maternal And Child Mortality ni moja wapo ya ajenda kwenye Millennium Dev Goals kupunguza. Priority zetu ziko kwenye kukuza ufisadi na kusahau mambo ya msingi. I do not know if Tanzania we are progressing in a right way.

Poleni sana wafiwa na Mungu ampumzishe Habiba mahali pema peponi.
 
rip habiba. mola awape faraja wote wakupendao.
 
What a pity! My the Almighty God rest her soul in eternal peace. Amen
 
Poleni wafiwa kwa msiba uliokuja siku chache tu baada ya kumpoteza mzee wetu Simba wa vita! Mungu awe nasi wakati huu mgumu wa maombolezo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…