Habari ya Uumbaji.Version 3

Habari ya Uumbaji.Version 3

ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
2,262
Reaction score
4,445
Habari za muda huu;
Kuna hadithi,simulizi na tafiti nyingi sana kuhus uumbaji,na mwanzo wa ulimwengu.Hadithi hizo zimesisitiza mengi sana na kwa kiasi zina ushawishi wa kipekee.

Leo niweke hoja mezani tujadili hoja ya uumbaji kwa kutazama dhana ya uwepo (Existence)

Nimewahi kukutana na msemo wa mwanafalsa mmoja nafikiri ni wa kifaransa akiitwa Descartes ambaye nafikiri alisema "Corgito ergo Sum" akimaanisha "kwa kuwa nafikiri basi nipo"(Sio tafsiri rasmi) kwamba a uwepo ni fikra.

Sasa kwa kuwa alishaibua hoja ya uwepo kwa msingi wa Fikra basi leo nataka kujadili iwapo fikra kweli ipo,au kwa kimombo "Does thinking really exist?"

Hapo ulipo unaweza ukaanza kujijibu mwenyewe,unaweza kusema ndio au hapana na yote yakawa majibu.Kwa kawaida unapojenga hoja za kifalsafa ni muhimu kujenga hoja za pande mbili ili kumwezesha hadhira wako kuibua mtazamo wa tattu kwani kifalsafa hilo ndio lengo la msingi,kuamsha fikra.

Nitaanza kwa kusisitiza tena kataka nadharia ya Desartes kuweso dhana ya uwepo kwa msingi wa fikra.Nikijaribu kuthibitisha kwamba fikra ipo.Katika kuthibitsha uwepo wa fikra nitazingatia hasa uwezo wa fikra kuthibitisha uwepo wake wenyewe bila kutegemea mtu au hali ya pili yaani fikra ina uwezo wa kuwepo au kutokuwepo bila kutegemea kitu,mtu au hali nyingine.

Uwezo huu wa fikra wa kuthibitisha uwepo wake bila kuhusishwa na vitu au hali zingine una fanya fikra kuwa jambo la kipekee.Uwezo huu wa fikra ndio unafanya fikrakuwa reference point ya uthibitisho wa uwepo wa masuala au vitu vingine.

Nitatoa mfano rahisi kwa wale ambao hawajawahi kuona meli au ndege.Watu hawa unawezakuwasimulia jinsi ndege ilivyo na siku wakiiona wakajua kuwa hii ndio ndege bila hata kuambiwa.Hivyo hivyo hata mtazamo wetu kuhusu masuala mengine katika maisha.

Uthibitisho wa vitu vingine huwa ni relative yaani huwa na uhusiano au ulinganifu.Mara nyingi uwepo wa vitu vingi huthibitishwa na fikra ndio maana watu wengi huwezi kushawishiwa ili kubadili fikra zao kwani kimsingi ukiweza kumfanya mtu afikiri tofauti basi unakuwa umemaliza yote.

Niendelee kutazama hoja hii kwa kujariba kukinzana kwamba Thinking does not exist.Katika kukinzana nitachukulia fikra kama mambo mengine ambayo yanahitaji kuthibitishwa uwepo wake relatively yaani kwa kuoanishwa na maswala mengine.Kiuhalisi katika kuitaza hakuna namna unaweza kuonyesha muundo wa fikra,labda imaginations.Ni vigumu hata kujua namna fikra zinavyofanya kazi kwa hakika au hata kujua uwezo wa kifikra unapimwaje.Tunaweza kupima kumbukumbu ila sio fikra.Hivyo basi kitu hiki ambacho hatuwezi kukielezea kwa hakika wala kukipima hakiwezi kuwa ndio msingi wa kuthibitisha uwepo wa mawazoo na vitu vingine.

Kwa mujibu wa uzi huu napenda kusisitiza kwamba,kwa mtazamo wangu,Fikra ni sanaa tu na kwamba ni sanaa ambayo mtu akiweza kuimudu basi anaweza kumudu aina nyingi za sanaa lakini swala la uwepo haliwezi kuthibitishwa kwa uwezo wa kifikra.

Nirudi kwenye hoja ya msingi inayohusu Uumbaji.Kwanza niweke msimamo wangu wazi,kwa mujibu wangu nafikiri Hakuna chochote kilichoumbwa wala hakuna mwanzao wala hakutakuwa mwisho.Uwepo sisi bibi na bwana ni wa kifikra tu na kwamba sisi kama binadamu,We exists in our own imaginations au kwa lugha nyepesi sisi ni sehemu ya ndoto tunayoiota sisi wenyewe.Hivyo basi hakuna namna tunaweza kuwa tuliingia katika ndoto hiyo wala hakuna namna ambayo tunaweza kutoka katika ndoto hiyo.

Yaani kwa kimombo.'We are part of our imaginations,therefore we cannot exist outside our imaginations and our imaginations cannot exist outside us.'

KaribuniTuendelee na mjadala
 
Mada Ngumu sisi watu Wa dar tunapenda vitu laini laini tu. Langu jicho
 
Back
Top Bottom