FELIX MSILIKALE
Member
- Aug 19, 2018
- 14
- 2
HABARI NJEMA YA UFALME WA MBINGUNI
Je duniani mna habari kwamba yupo nabii wa MUNGU Mtakatifu? Kama hamna habari basi nabii huyo yupo hapa duniani, na biblia imemuelezea ya kwamba atakuja kutayarisha ujio wa mara ya pili wa Mtakatifu BWANA YESU KRISTO. Nabii huyo ametabiliwa katika biblia hatua mbalimbali. Hatua ya kwanza ya mabadiliko ya nabii huyo alibadilishwa macho yake mwaka 1988 kama nabii Zakaria alivyotabiri, Zakaria3:8-10. Hatua ya pili mwaka 1989 alianza kuongea na Mtakatifu BWANA YESU KRISTO muda wa usiku akiwa amelala na kupokea habari mbalimbali za MUNGU Mtakatifu na kuwajulisha jamaa zake wa karibu. Hatua ya tatu alianza kuongea mwaka 1990, alianza kuongea na MUNGU Mtakatifu muda wote mchana na usiku jambo ambalo liliwashangaza watu wa karibu yake na kuamua kufatilia katika biblia juu ya mabadiliko ya maono hayo biblia inafafanuaje, kama Kumb18:15-22, Malak4:4-6, Math11:2-15, Yoh16:12-15, Math17:10-13 na Yoh1:19-23. Watu wa karibu yake walianza kufuatilia katika biblia na kufahamu kua ni kweli kuhusu mafungu haya yanayo mtambulisha nabii wa MUNGU Mtakatifu na mafungu mengine mengi kama Isaya41:3.Njia anayotumia kuongea na MUNGU Mtakatifu ni ya kufumba macho, nabii huyu anapofumba macho anaona moja kwa moja juu MBINGUNI na kumuona MUNGU Mtakatifu na watakatifu wote walio juu MBINGUI kama nabii Isaya alivyotabiri Isaya42:18-21. Nabii huyu aliendelea kuongea na MUNGU Mtakatifu na maono hayo yakazoeleka ya kwamba anaona MBINGUNI, duniani na sehemu yoyote ile ambayo MUNGU Mtakatifu anapenda kumuonesha kama vile baharini majini chini ya dunia ambako ndiko makazi ya shetani yaliko. Hivyo watu wakaribu wamezoea wanauliza shida zao mbalimbali na ndoto zao na kupata majibu ya shida zao na tafsiri ya ndoto zao mbalimbali kutoka kwa MUNGU Mtakatifu wa MBINGUNI kupitia kwa Mwonaji wake nabii.
Baada ya maono hayo kuwa wazi kiasi hicho MUNGU Mtakatifu alimuagiza Mwonaji nabii na watu walio karibu yake wajenge kanisa, kanisa lilijengwa mwaka 2000 miyomboni Misugusugu wilaya ya kibaha mkoa wa Pwani Tanzania, ambalo limepokea habari njema ya ufalme wa MBINGUNI kuwa ushuhuda kwa watu wote kama Mtakatifu BWANA YESU KRISTO alivyotabiri katika Math24:14, pia kumekuwa na mafundisho mbalimbali yanayopokelewa kila sabato na nyimbo mpya kutoka MBINGUNI zimepokelewa kutoka kwa MALAIKA GOGBAM muimbaji wa MBINGUNI.
Lengo hasa la MUNGU Mtakatifu kuleta maono haya kwa nabii huyu ni kuwaandaa watu kwamba Mtakatifu BWANA YESU KRISTO yuko karibu kurudi duniani, watu wote wajiandae kuacha dhambi ili waweze kumpokea mawinguni. Hivyo maandalizi unayotakiwa uwenayo mwanadamu sasa, unatakiwa ushike amri kumi kama yeye Mtakatifu BWANA YESU KRISTO alipokuwa hapa duniani Yoh15:9-10, pia lazima uwe msabato kama yeye alivyokuwa msabato Luk4:16-18, Math12:8. Mtakatifu BWANA YESU KRISTO anasisitiza kwamba watakao kwenda MBINGUNI watakwenda kuabudu sabato kama alivyosema katika Biblia Isaya66:22-23. Kwahiyo watu wote karibuni tumsikie Mtakatifu BWANA YESU KRISTO anasema nini kwa wakati huu duniani
MAWASILIANO
Mwonaji/NABII: 0758408348 au 0712838675
Mtumishi wa kiroho: 0752092911
Mzee wa kanisa: 0754993241 au 0715993241