Habari njema kwa wanaozaa uzeeni

Habari njema kwa wanaozaa uzeeni

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,274
Reaction score
25,322
Utafiti huo uliofanywa na Chuo cha Kings, London na kuchapishwa Mei mwaka huu, umebaini kuwa hata umri mkubwa wa mama si tatizo kwa mtoto bali humuongezea mtoto anayezaliwa kinga ya mwili.

Wanasayansi waliofanya utafiti huo wanasema kuwa iwapo mwanaume atachelewa kupata mtoto huenda jamii ikaendelea kuwa na watoto werevu.

Matokeo ya utafiti huo ni habari njema katika sayansi na dhana ya kuchelewa kuanzisha familia.

Tafiti za awali zilizowahi kufanywa zilionyesha kuwa mbegu za kiume za mwanaume mzee hukumbwa na matatizo ya jeni na kwamba watoto huzaliwa na ugonjwa wa kiakili.

Watafiti waliwafanyia utafiti watoto pacha 15,000 walioshiriki katika utafiti uliokuwa ukichunguza ukuaji wao.

Baadaye watafiti hao walichapisha tabia za watoto hao wakati wakiwa na umri wa miaka 12.

Wale waliochunguzwa walionekana kufanya vyema shule hususan katika masomo ya sayansi, teknolojia, uhandisi na uhasibu.


Chanzo: Mwananchi
 
Kwa hiyo wanaume wazee tuwahimize wake zetu wafyatue watoto....Hahahah utafiti mzuri huu
 
Back
Top Bottom