Habari njema kwa Wanafunzi: Elimu bure kiganjani kwako

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
23,539
21,567
UTANGULIZI

Malkia wa Nguvu, Madam Faraja Kotta Nyalandu, mnamo tarehe 18.03.2016 alizindua rasmi huduma ya elimu itakayokuwa ikipatikana kwa njia ya simu ya mkononi kwa wanafunzi wa shule za sekondari (O-level) kama anavyoongea kwenye VIDEO HII HAPA .

.

UPATIKANAJI WA HUDUMA

Huduma hii adhimu ijulikanayo kama MAKINI SMS itakuwa inapatikana kupitia kwenye simu ya kiganjani ambapo mwanafunzi au raia yeyote anayependa kujifunza atatuma neno MAKINI kwenda namba 15397 kujisajili. Baada ya kujisajili atatumiwa somo (LESSON) pamoja na maswali (QUESTIONS). Kila lesson itaambatana na maswali matano (Hii inaitwa QUIZ). Quiz moja ni sawa na lesson moja na maswali matano. Unaweza kujibu quizzes nyingi zaidi kadri utakavyotaka kujifunza. Masomo haya huandaliwa na walimu wazoefu na waliobobea katika masomo husika kwa lengo la kutoa elimu endelevu kwa vijana wa kitanzania. Kwa kuanzia, huduma hii itakuwa ikipatikana kupitia mtandao wa TIGO pekee lakini kadri mahitaji yatakapokuwa makubwa itasambaa hadi kwenye mitandao mingine.

.

USAHIHI

Naomba kuwafahamisha kuwa masomo haya SIO kwa wanafunzi wa O-level tu. La hasha! Masomo haya yanamhusu kila mtu anayejifunza au anayefunza. Nitafafanua. Ikiwa wewe ni mwanafunzi unayesoma shule, mwanafunzi unayejiandaa ku-reseat masomo yako, mwalimu, mwalimu mwanafunzi (student teacher), mtafiti, mdadisi nk, masomo haya yanakuhusu. Kimsingi kila raia wa nchi hii anaweza kujisajili na kuanza kupata elimu hii sasa. Kwa mfano, hakuna haja ya mwalimu kuumiza kichwa kutafuta maswali ya kuwatungia wanafunzi wake wakati maswali hayo na majibu yake anaweza kuyapata kwa ufasaha kabisa kupitia MAKINI SMS. Aidha, masomo haya yanaweza kusomwa na wanafunzi wa elimu ya juu kwa lengo la kujinoa zaidi kielimu. Vivo hivyo, hata watafiti wa masuala ya elimu wanaweza kutumia masomo haya ya makini kufanya utafiti wao. Kwa uchache, huu ndio ufafanuzi wa walengwa wa MAKINI SMS…kila raia katika nchi hii ni mlengwa na mhusika!

.

SAMBAMBA

Sambamba na huduma hii ya MAKINI SMS pia Madam Faraja amebuni njia nyingine mujarabu ya kuwasaidia wanafunzi bure. Punde si punde, wanafunzi watawezeshwa kuuliza maswali mtandaoni na maswali hayo yatakuwa yakijibiwa na walimu mashuhuri wanaojulikana kwa jina maarufu la TICHA KIDEVU. Kutakuwa na fursa ya wanafunzi kuuliza maswali online na kujibiwa haraka kupitia feature inayojulikana kama ASK TEACHER KIDEVU. Wanafunzi kaeni mkao wa kula kwani chakula kishaiva tayari….mtaanza kulishwa hivi punde!

.

MSHANGAO!

Kwa bahati mbaya (au makusudi?) habari hii nzuri haijapata media coverage ya kutosha. Baada ya uzinduzi, nilitegemea taarifa muhimu kama hii ingekuwa ya kwanza kutangazwa kupitia runinga na kuwekwa kwenye kurasa za mbele za magazeti lakini haikuwa hivyo. Tatizo matukio ya kisiasa huchukua nafasi kubwa kuliko kitu chochote katika nchi hii.

.

MADAM FARAJA ALIPOANZIA

Madam Faraja ameanza kujishughulisha na masuala ya elimu kwa muda mrefu ambapo mpaka sasa anaendesha tovuti ya www.shuledirect.co.tz ambayo humuwezesha mwanafunzi kusoma bure masomo yote ya O-level. Hii ni baada ya kugundua kwamba wanafunzi wengi hushindwa masomo yao kwa sababu ya kukosa nyenzo muhimu za kujifunzia. Ndipo akaja na wazo la kufungua tovuti hii ili kila mwanafunzi katika taifa hili apate haki yake ya msingi ya elimu. Ukifungua tovuti hii utakuta masomo mbalimbali ya O-level yaliyoandaliwa na walimu wabobezi katika masomo husika. Hakuna haja kusumbuka kununua vitabu wakati elimu yote inapatikana hapa.

.

PONGEZI KWA MADAM FARAJA

Napenda kuchukua fursa hii kumpongeza Malkia wa Nguvu, Her Excellency Madam Faraja Kotta Nyalandu, kwa jitihada zake za kuhakikisha kuwa kila kijana wa taifa hili anapata elimu bora na yenye viwango. Hivi ndivyo kila raia mzalendo anavyotakiwa kulitumikia taifa lake. Madam Faraja, nakuombea kwa Mungu uendelee na moyo huu wa kizalendo wa kulitumikia taifa lako leo, kesho na hata milele. Amina.

.

USHAURI KWA WANAFUNZI

Ili kufaidi vizuri elimu hii kupitia MAKINI SMS wanafunzi wanashauriwa kutumia simu zao kwa ajili ya masuala ya manufaa kama haya badala ya kutumia muda mrefu kuchat na kujishughulisha na mambo yasokuwa na tija. Wanafunzi wengi wanamiliki simu lakini utafiti unaonyesha kwamba huzitumia simu hizo katika masuala yasiyokuwa ya msingi. Ni matumani yangu kwamba sasa wanafunzi watabadilika na kuanza kujikita katika masomo tofauti na ilivyokuwa zamani. Hakuna kisingizio sasa…ukifeli utakuwa umejitakia mwenyewe. Umeletewa elimu hadi kiganjani mwako halafu unafeli ili iweje? Wanafunzi changamkieni fursa hii. Ukipata taarifa hii mjulishe na mwenzako. Kufeli sasa basi. #HapaKusomaTu!

.

HITIMISHO

Ile fursa adhimu iliyokuwa ikisubiriwa na wanafunzi kwa muda mrefu ndio hii hapa. Kuanzia mwaka huu mwanafunzi yeyote atakayefeli atakuwa amejitakia mwenyewe. Hakuna haja ya kuendelea kulialia kwamba shule yako haina walimu. Kama shule yako haina maabara, walimu na vifaa vya kutosha kujifunzia, MAKINI SMS ndio suluhisho la matatizo yako ya elimu. Aidha, hakuna sababu ya mwalimu kulialia na kuumiza kichwa kutunga maswali kwa wanafunzi wako wakati maswali yote na majibu yake yanapatikana kupitia MAKINI SMS. Kana kwamba hii haitoshi, hakuna haja ya NECTA kuumiza vichwa kutafutaa maswali wakati maswali yote ya NECTA yanapatikana kupitia MAKINI SMS. Changamkia fursa….saa ya ukombozi wa elimu ni sasa! Nawatakia kila la kheri katika kujifunza.

.

#HapaKusomaTu!
 
asante ila naomba kujua, ghalama za hizo sms, lakin pia mwanafunzi atafaidika kwa masomo yapi, na majib yake yatasahihishwa vip?
 
asante kwa swali zuri mkuu. suala la gharama bado halijaanza kuzingatiwa. muda wa kulipia ukifika utaarifiwe. kwa sasa huduma hii inapatikana bure kabisa kama ulivyomsikia Malkia wa Nguvu akisema kwenye video hapo juu. mwanafunzi atafaidika kwa masomo 9 yanayofundishwa sekondari na majibu utayapata kwa njia ya sms mara baada ya kujibu na ku-submit for grading.
 
naweza kuwa mteja wako hasa kwa watt wangu, npe ufafanuzi mhim, ghalama, mwanafunzi na mwalim wankutana vp,?
mkuu asante kwa swali zuri. mwalimu na mwanafunzi hawakutani physical...wanakutana online tu. majibu ya maswali tayari yameishasetiwa kwenye mtandao. ukichagua jibu sahihi au la ukweli utapatiwa jawabu sahihi automatically kutoka kwenye mtandao (MAKINI SMS) au kupitia email (ASK TICHA KIDEVU). tuko pamoja mkuu?
 
ghalama zake zikoje, maana nliuliza sijapata majib
 
Mwanafunzi mnunulie kitabu.

kusoma kwa simu kwa teenagers kunahitaj nidhamu ya hali ya juu sana.
utakuta mwanao yupo busy na simu ukadhani kuwa anasoma kumbe ni Admin wa magroup nane ya Watsapp.
 
Good,nimefungua hiyo website naona inafunguka ila vilivyomo havifunguki?Mf:past papers.
 
Mkuu wakipata usimamizi mzuri kutoka kwa wazazi, walimu na jamii kwa ujumla watasoma.
 
Good,nimefungua hiyo website naona inafunguka ila vilivyomo havifunguki?Mf:past papers.
mkuu kuna baadhi ya past papers bado hazijawekwamo ila kumbuka kwamba awali ya yote ni lazima kwanza ujisajiri.
 
Ndo maana nchi yetu vilaza wengi
mkuu matatizo mengi ktk nchi hii huchangiwa na ukosefu wa vifaa vya kuifunzia. naamini mpango huu wa MAKINI SMS utawakomboa wengi.
 
Back
Top Bottom